Tofauti na dunia ya hapo awali, ambapo walimwogopa Maulana na kujitenga na mambo ambayo hayakubaliki katika jamii, katika dunia ya leo, hali ya kumwogopa Mungu imepungua. Vitu vinavyokubalika katika jamii vimebadilika na hata ingawa hapo awali havikukubalika, leo hii vyaonekana ni vitu vya kawaida. Je, ni tabia zipi ambazo nyanya zetu hawakukubali ila leo zaonekana za kawaida? Wazazi wanao mcha Mungu wangependa kuendeleza imani hii ya kumwamini Mungu katika watoto wao. Ni muhimu kwa wazazi kuelewa mtoto ni nani kibibilia na jinsi ambavyo wanaweza kuwalea watoto wanao mwamini Mungu.
Kuwalea Watoto Wanao Mwamini Mungu

- Kuwa mfano mwema wa kuigwa
Sawa na nyanja zingine za kimaisha, mtoto huiga anachowaona wazazi wake wakifanya na wala sio wanacho mwambia. Kuwa mtu mwenye utu, kama bibilia inavyohimiza. Kuwa mkarimu na mwenye moyo mkunjufu kwa watu walio karibu nanyi. Kuwa mkristo na kumwamini Mungu sio suala la kwenda kanisani na kusoma bibilia, mbali ni utendaji wa unachosoma katika bibilia na kuwa na vitendo chanya.
Bila shaka mtoto wako atakua akifahamu jinsi ambavyo mtu anaye mcha Mungu anavyopaswa kuwa.
2. Omba pamoja na watoto wako
Fanya mtindo wa kuomba na watoto wako kila mara. Anza siku kwa maombi kabla ya kuanza siku na baada ya kutamatisha siku kabla ya kulala kama familia. Maombi yataongeza imani yao na kuwasaidia kujitenga na mambo yasiyo mpendeza Mungu. Maombi yanasaidia watoto kuwa na imani moyoni na kufahamu kuwa kila kitu kinachotendeka maishani huwa mpango wa Mungu.
3. Wafunze watoto wako

Kama bibilia inavyosema kuwa, mfunze mtoto wako kutembea kwa njia zinazo mpendeza Mungu na kamwe hawatatoka katika njia hizo. Wazazi wanaotaka kuwalea watoto wanao mwamini na kumwogopa Mungu wanapaswa kuangazia somo hilo. Wazazi wanapaswa kuwafunza watoto neno la Mungu. Tenga wakati kila wiki kusoma bibilia pamoja na watoto wako, kusikiliza neno la Mungu pamoja kwa televisheni.
Kwa kufanya hivi, watoto hawa watakuwa wakitenga muda wa kusoma bibilia na kuomba hata wanapokuwa watu wazima.
4. Zingatia sinema wanazotazama
Kuna sinema za aina tofauti, na zingine sio sawa kwa watoto, zingine hazikubaliki katika jamii, ila bado zinapatikana. Iwapo ungetaka kulea watoto wanaomcha Mungu, kuwa mwangalifu kwa sinema na nyimbo ambazo watoto wako wanasikiliza. Sinema zinachangia pakubwa katika upotovu ulioko. Wafunze kutizama sinema zisizo na mambo kadri ya matakwa ya Mungu.
5. Washauri kuhusu urafiki
Shinikizo kati ya marafiki ni changio kubwa la kupotoka katika watoto na hata watu wazima. Kwa wazazi wanao fahamu mtoto ni nani kibibilia na anavyopaswa kuwa, watakuwa makini na marafiki wa watoto wao. Ikiwa mwanao ni mzuri ila ana marafiki waliopotoka, atafuata mkondo wao. Kuwa na marafiki wenye tabia chanya na wanaomcha Mungu kutawasaidia kubaki katika njia zinazompendeza Maulana.
Chanzo: Christianbook.com
Soma Pia: Kudumisha Uhusiano wa Kibinadamu na Familia Baada ya Kufunga Ndoa