Ukuaji wa Mtoto na Hatua Muhimu: Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja

Ukuaji wa Mtoto na Hatua Muhimu: Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja

What's your child going to amaze you with this month? Read on to find out.

Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja amekua kwa kasi sana. Siku zake za kukaa nyumbani zimeisha na anakaribia kwenda shuleni. Kwa sasa anaonyesha hali ya kuwa huru zaidi. Iwapo unashangaa mambo ya kutarajia kutoka kwa mtoto wako mwezi huu, tuko hapa kukusaidia.

Tuangazie hatua muhimu za mtoto wa miaka mitano na mwezi mmoja unazopaswa kujua na kutarajia mwezi huu.

Kama ilivyo kawaida, tafadhali jua kuwa huu ni mwongozo tu kwani kila mtoto hukua na mwendo wake. Iwapo una maswali yoyote kuhusu ukuaji wa mtoto wako, pata ushauri wa mtaalum wa watoto wadogo.

Hatua Muhimu na Ukuaji wa Mtoto wa Miaka Mitano na Mwezi Mmoja: Mtoto wako Anakua Ipasavyo?

5 year 1 month

Ukuaji wa Kifizikia

Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja kwa sasa anaweza kuongea kwa urahisi na anaonyesha kufurahi kwake kwa njia za kisarakasi. Kuambatanisha kwa macho na mikono yake kumeimarika na kwa sasa na uwezo wa kujifanyia mambo ya kimsingi kama vile kujilisha ama kujipeleka msalani.

Uwezo wake wa kutembea umeimaraka sana kwa sasa ikilinganishwa na miaka yake ya hapo awali. Ni dhahiri kwa sasa kuwa anajitgemea kwa sana kufanya mambo yake.

Watoto wote hukua kwa mwendo wao, ila kwa sana wao hupata vipawa vingi vya kifizikia. Wanaweza kuruka juu, kukimbia kwa ujasiri na pia huanza kufanya michezo migumu kama vile karate na ballet.

Katika hatua hii, mtoto wako ana uwezo wa kufanya yafuatayo:

 • Anaweza kuiinua miguu hewani na kupinduka
 • Ujasiri wa kupanda miti ama viti
 • Uwezo wa kusimama kwa mguu moja kwa sekundu kumi
 • Huenda akajivalisha nguo ama kujitoa bila usaidizi
 • Confident in swinging and climbing
 • Anaweza tumia uma kukula ama wakati mwingine kisu kukula
 • Kutumia msalani bila ya usaidizi wowote

Haijalishi kiasi ambacho mtoto wako anakaa yuwapendeza, bado yuakua! Hata kama anaweza kudhibiti mahitaji yake ya msalani, kukojoa kitandani huwa bado jambo la kawaida na usiwe na shaka yoyote.

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mtoto wako* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  - Urefu: 109.7 cm (43.2 inchi)
  - Uzito: 18.7 kg (41.2lb)
 • Wasichana
  - Urefu: 108.5 cm (42.7 inchi)
  - Uzito: 18.2 kg (40.2 lb)

Vidokezo:

Kumpa mtoto wako nafasi tosha na wakati wa kujaribu vitu vipya kutasaidia kukuza uwezo wake wa mwendo zaidi.

 • Mpeleke kwenye kiwanja ama mahali ambako kuna vyombo vya kucheza navyo.
 • Msajilishe mtoto wako kwa vikundi vya kufunzwa kuogelea ama mchezo wowote wa kifizikia anao upenda. Hakikisha kuwa anaangaliwa kwa wakati wote.
 • Mhimize mtoto wako anapo jaribu kujifanyia mambo kwa kipekee kama vile kuvalia nguo ama kwenda msalani.
 • Punguza utumiaji wa vifaa kama rununu vyumbani vya kulala. Toa simu na mwangaza ili kuepuka vitu vya kumfanya asilale.
 • Mhusishe katika shughuli rahisi za kinyumbani. Zitamsaidia kukuza uwezo wake wa kuandamanisha mikono na macho yake..

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo unashuhudia kuwa mtoto wako haonyeshi uwezo inavyopaswa. Unashauriwa kumwona daktari afanye vipimo vinavyo hitajika. Baadhi ya ishara za kuwa mwangalifu ni kama vile:

 • Kushindwa kushika penseli vyema
 • Matatizo ya kula, kulala ama kwenda msalani peke yake
 • Tatizo la kujivalisha nguo mwenyewe

your child's cognitive development at 61 moths or 5 years 1 month

Ukuaji wa Kiakili

Shule inakaribia! Mtoto wako amekuwa akisoma mengi na kuhifadhi mambo mengi.

Uwezo wa mtoto wako wa kukumbuka mambo unaimarika kwa kasi sana. Anakumbuka mambo mengi na una ufahamu zaidi kuhusu vifaa vya kila siku vya nyumbani na majina yao pia. Baadhi ya hatua muhimu unazo weza kuona kwenye mtoto wako ni kama vile:

 • Muundo wa pembe tatu na miundo mingineyo
 • Uwezo wa kuchora watu wenye sehemu sita za mwili ama zaidi
 • Ana uwezo wa kuhesabu hadi ishirini ama zaidi
 • Uwezo wa kutaja vifaa vya nyumba kama vile chakula
 • Kutaja majina ya marangi angalau manne
 • Anaelewa kuhusu wakati
 • Kuandika baadhi ya herufi na nambari

Vidokezo:

 • Mhimize mdogo wako kuchora. Kuna saidia kuimarisha uwezo wake wa kufikiria na uwezo wake wa mwendo.
 • Anza kumhimiza awaandikie marafiki wake barua. Kuna saidia kuimarisha uwezo wake wa kufikiria na pia ni zawadi njema kwa marafiki wake.
 • Kufanya shughuli za kipekee kwa kutumia makasi na bidhaa zingine. Ni jambo la kufurahisha kwa mwanao na kunamsaidia kujua miundo tofauti.
 • Punguza wakati wa mtoto wako wa kutazama runinga hadi kwa lisaa limoja kwa vipindi vinavyo elimisha. Iwapo kipindi kina burudisha, kuna njia nyingi za kuhimiza ukuaji wa akili wa mwanao.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Mwanao anaonekana kana kwamba anataabika sana
 • Anashindwa kupea jambo moja umakini wa angalau dakika tano

a child playing with hoops

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Uwezo wake wa kuwa na mawazo mengi kuna maana kuwa huenda akajipata akicheza michezo baada ya kutekwa kiakili na mafikira ya dunia isiyo kuwa kweli. Utagundua kuwa anaweza kucheza na wengine huku anafanya kazi kufikia lengo fulani. Kama vile kuepuka kufika sehemu fulani.

Mtoto wako kwa sasa anakubaliana na mambo mengi na anatazamia kucheza na watoto wengine.

Huenda ukagundua kuwa kwa sasa anagawia marafiki wake vidoli vyake na wacheze pamoja na hahisi vibaya iwapo kuna mtu hataki kucheza. Ila, kuwa makini kwani huenda akawa na hisia nyingi iwapo mambo hayaendi anavyo taka.

Vidokezo:

 • Mwache mtoto wako achague shughuli anazo taka kufanya na marafiki wake. Anapata nafasi ya kuingiliana na watoto wengine wanapo jadiliana na marafiki wake!
 • Iwapo kuna matatizo yatajitokeza kati ya mtoto wako na marafiki wake, waache watambue njia nzuri ya kukabiliana na tatizo lao. Jambo hili linamsaidia mtoto wako kujua jinsi ya kuwapa wengine nafasi.
 • Ongea na mtoto wako na umsikize kwa makini. Unapo husiana naye, mwulize anacho taka, pia alicho fanya siku hiyo. Atahisi anapendwa na kuthaminiwa.
 • Mtoto wako anapenda kujieleza! Mhimize mtoto wako akatike ama kuimba ama kuigiza- Jiunge naye pia!

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako ana uwoga mwingi ama hasira nyingi ama hana ujasiri
 • Ana shaka nyingi asipo kuwa karibu na wewe
 • Anakataa kucheza na watoto wengine

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja ana ongea kuhusu anachotaka kwa kutumia maneno. Ni mwema zaidi katika kuelewa anacho kisema na amepata ujuzi zaidi kuhusu maneno bora zaidi ya kutumia kama "juu ya" ama "chini".

Wakati wa hadithi umekuwa wa kuingiliana zaidi na mtoto wako mdogo na huenda akakumbuka baadhi ya sehemu za hadithi. Kwa hivyo unapomsomea, sio mtu mmoja tu anaye husika- mtarajie akwambie kwa furaha kitakacho tendeka ama mawazo yake kuhusu baadhi ya watu kwenye hadithi hiyo.

Je, nini mojawapo ya ishara za ukuaji na hatua muhimu kwa mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja unazo paswa kujua?

Mtoto wako anaweza:

 • Kuyafanya maneno yaambatane.
 • Kulisema jina lake.
 • Kumbuka nambari yako ya simu.
 • Kuongea kwa urahisi na kutunga sentensi yenye maneno matano ama zaidi.

Utashangaa na kufurahi kujua kuwa mtoto wako ana zaidi ya maneno 20,000 na zaidi. Sio jambo jipya kuwa anajieleza vyema zaidi na kwa urahisi. Ila, utumiaji wake wa maneno haya ni muhimu katika kukuza uwezo wake wa lugha na kuongea.

Anapo anza darasa la kwanza, atajua jinsi ya kujisomea mwenyewe. Hapa ni baadhi ya vidokezo vya shughuli za kumshughulisha mtoto wako kumsaidia kuimarisha uwezo wake wa kusoma.

Vidokezo kwa wazazi:

 • Endelea kumsomea mtoto wako. Kuza mapenzi yake ya vitabu na umpeleke kwenye maktaba. Uwezo wake wa kutamka maneno utaendelea kuimarika kadri anavyo zidi kusoma vitabu vingi!
 • Sisitiza majina yanayo tumika kwa sana unapokuwa unamsomea mtoto wako. Kurudia kunamsaidia mwanao kukumbuka majina mapya unapo yaashiria.
 • Zungumza na mtoto wako kuhusu mazingira yake na umhimize kukueleza yalivyo ama anacho ona.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Ana tatizika sana kutumia ngeli iliyopita
 • Hatumii wingi
 • Ni kigugumizi

Afya na Lishe

mtoto wa miaka mitano na mwezi mmoja

Mtoto wako wa miaka mitano na mwezi mmoja atakua ameongeza kilo 2.25 na kukua sentimita 5.5 kwa urefu kutoka siku ya kuzaliwa kwake ya nne! Watoto wengi huwa na kilo 17 hadi 20.3 na urefu wa sentimita 106 hadi 112.2. Meno yake ya watu wakubwa itakuwa imeanza kumea na uwezo wake wa kuona u 20/20.

Kwa wakati huu, mtoto wako mdogo anacheza kwa sana na ni muhimu kwako umpe lishe bora ili aendelee kukua katika njia bora. Hukula karibia asilimia 1300, ila inategemea na jinsi anavyo cheza mchana.

Kwa kawaida, kalori wavulana na wasichana wanao kula katika umri huu ni ifuatavyo:

 • Wavulana: 1,670 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,564 Kcal/kwa siku

Kiwango cha chakula ni kulingana na mwongozo ufuatao:

Aina ya chakula
Kiwango kinacho shauri
Nafaka (vijiko 6 vidogo kila siku) Kipande 1 cha mkate

1/2 kikombe cha wali /pasta (80g)

Mafuta (3-4 kila siku) kijiko kimoja cha mafuta/ siagi
Matunda na Mboga (mara 5 kwa siku) 1/2 - 1 tunda ndogo

1/2 kikombe kilicho pikwa ama la(80g)

 

Nyama (mara 2 kwa siku) 1-3 vijiko vidogo vya nyama, kuku, ama samaki

1 yai

5 vijiko vidogo vya peas na maharagwe

Maziwa (mara 3 kwa siku) 3/4 kikombe cha maziwa ama yoghurt (177ml)

3/4 ounsi ya cheese (22g)

Tuna angazia virutubisho mwanao anazo hitaji kila usiku unazopaswa kumlisha kila siku:

Protini

Katika miaka mitano na mwezi mmoja, mtoto wako anahitaji vijiko viwili vya protini (kwa ujumla karibia gramu 32.4) kila siku. Jaribu kumpa vijiko angalau vitatu vya kuku, nyama ama samaki, vijiko vinne ama vitano vya maharagwe ama yai la kuchemsha.

Matunda

Pia anahitaji vikombe vitatu (gramu 100) vya matunda kila siku. Kikombe kimoja cha matunda ni sawa na yaliyo toka shambani, yaliyo gandishwa ma kukaushwa. Nusu (1/2) tofaha moja kubwa, 1/8 ya ndizi, na zabibu.

Iwapo mtoto wako anataka kunywa maji ya sharubati, hakikisha kuwa ni asilimia 100 ya maji matamu bila sukari za kuongezwa. Pia, jaribu kumlisha matunda kutoka shambani iwezekanavyo, hasa na ngozi yake ya nje.

Mboga

Katika hatua hii, mtoto wako anahitaji vikombe visivyo pungua viwili vya (gramu 100 kila moja) vya mboga kila siku. Jaribu kumpa fiber na mboga zilizo na iron nyingi kama vile spinachi, karoti zinginezo.

Pia, unaweza kumpa kikombe kimoja cha mboga kinacho toshana na kikombe kimoja cha mboga zilizo pikwa, mboga za majani, nyanya moja kubwa na karoti mbili.

Mpe mwanao mboga tofauti za rangi nyingi kutoka kijani, nyekundu, rangi ya machungwa, maharagwe kila wiki. Unapo chagua mboga zilizo hifadhiwa, chagua zilizo na kiwango cha chini cha sodium.

Nafaka

Mwanzishie mwanao ounsi nne za nafaka katika lishe zake. Ounsi moja ya nafaka ni sawa na kipande kimoja cha mkate,kikombe kimoja cha nafaka zilizo tayari ama nusu kikombe cha wali uliopikwa.

Unaweza chagua kutoka kwa nafaka nzima kama vile, mkate usio wa mtama mweupe, mchele wa hudhurungi. Ila, usisahau kupunguza kiwango cha nafaka zilizo tayarishwa kama vil mkate mweupe ama mchele.

Maziwa

Katika umri huu, mtoto wako anapaswa kunywa maziwa angalau ounsi 17 hadi 20 za maziwa kila siku. Huenda ukampa maziwa yaliyo hifadhiwa ama yogurt badala ya maziwa, na ounsi mbili za cheese iliyo tengenezwa.

Kwa ufupi, haya ni baadhi ya mahitaji ya mtoto wako ya kila siku (tazama viwango tulivyo angazia hapo juu)

 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Chanjo na maradhi ya kawaida

Mtoto wako hana chanjo yoyote inayo karibia kwa wakati huu. Soma makala haya kuhakikisha kuwa ratiba ya mtoto wako wa miaka mitano imefuatiliwa. Shauriwa na mtaalum wa watoto hukusu kumpa mtoto wako dawa ya mafua.

Maradhi ya kawaida ya watoto katika umri huu ni kama vile ugonjwa wa Hand, Foot and Mouth, na kikohozi na mafua.

Wakati ambapo huwezi epuka maradhi haya, unaweza imarisha uwezo wa mwanao wa kupigana na maradhi kwa kumpa lishe bora na vinywaji vingi, matunda na mboga. Zingatia hali ya juu ya usafi kama vile kunawa mikono ambayo huenda ikasaidia sana katika kumlinda mwanao kutokana na magonjwa.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kati ya magonjwa haya ya kawaida ambayo huenda yakamshika mwanao, ya kawaida kabisa huenda yakawa ni kukohoa, homa na joto jingi. Tuangazie jinsi ya kuyatibu nyumbani.

 • Kutibu homa: Kwa ujumla, unashauri kuepukana na madawa ya kununua bila ya kuidhinishwa na daktari. Homa husababishwa na viini kwa hivyo dawa nyingi hazisaidii kuponyesha. Walakini, iwapo homa hii inazidi na kuwa joto jingi na maumivu na kuumwa, ni vyema upate ushauri wa daktari.
 • Kutibu joto jingi: Mpatie mwanao vinywaji vingi, iwapo na joto inayo zidi 38°C (100.4°F)hakikisha kuwa anapata mapumziko ya kutosha. Pia, huenda ukampangusa na maji vuguvugu kwenye utosi wake, chini ya makwapa na sehemu nyeti kupunguza joto ile. Walakini, iwapo joto yake inaongezeka zaidi ya 38°C (100.4°F),unapaswa kumpeleka kwa daktari akupe mawaidha jinsi ya kudhibiti afya ya mtoto wako.
 • Kutibu kikohozi:Kukohoa ni kawaida kwa watoto. Huenda kukawa kwa kusinya na kufuatiwa na homa kali. Ni bora kuwa ujaribu kutibu maradhi haya kinyumbani kwa kutumia kitunguu saumu, asali, maji ya vuguvugu na ginger. Pia unaweza mwuliza mtoto wako anywe maji glasi nane za maji kutuliza kutokuwa na starehe. Iwapo kikohozi hakipungui kwa siku tatu ama tano, pata ushauri wa daktari.

Ni muhimu kujua kuwa baadhi ya dawa huenda zikanunuliwa bila ushauri wa daktari. Ni vyema zaidi kwa mwanao kuwa matibabu anayo pata ya kwanza kwa shida zake za kiafya ni matibabu rahisi ya kinyumbani.

Mpe vinywaji vingi vilivyo pashwa joto iwapo ana kikohozi ama homa. Unaweza msaidia kuweka maji ya chumvi kwenye mdomo wake kisha kutema kabla ya kumeza.

Wakati wa kumwona daktari:

 • Iwapo mtoto wako anaongeza uzito mwingi ama ana kilo za chini zaidi, pata ushauri wa daktari kuhusu lishe bora
 • Ana joto ya zaidi ya 38 degrees Celcius

References: WebMD, Healthy Children, Mayo Clinic

Mwezi uliopita: 5 years

Mwezi ujao: 5 years 2 months

Republished with permission from theAsianparent

(*Disclaimer: This is the median height and weight according to WHO standards)

Written by

Risper Nyakio