Ukuaji wa Mtoto na Hatua Muhimu: Mtoto wako wa miezi kumi

Ukuaji wa Mtoto na Hatua Muhimu: Mtoto wako wa miezi kumi

Get to know your baby at 10 months, a stage where he becomes more chatty, curious, and adventurous!

Mtoto wako mchanga anapo fikisha miezi kumi, utashangazwa na hali ya kujitegemea atakayo kuwa nayo. Mtoto wako wa miezi kumi kwa sasa anaanza kuwa mwenye mazungomzo mengi, na matamshi pia, anapo jaribu kuongea na kila mtu.

Katika umri huu, utaweza kuhisi utu wa mwanao. Je, aibu ama ni jasiri? Pia wanaanza kuvichagua vitabu, muziki na vitu vingine wavipendavyo.

Ukuaji na hatua muhimu kwa mtoto wako wa miezi kumi: Je, mwanao anakua ipasavyo?

10 months old baby development and milestones infographic

Ukuaji wa kifizikia

Kwa sababu anataka kuyajua mengi, mtoto wako wa miezi kumi kwa kiasili ataanza kutembea kujua mazingira yake. Ni vyema kwani uwezo wake wa kutembea unaendelea kukua katika umri huu! Ana uwezo wa kutambaa na pia kujisimamisha. Anaweza kujikalisha chini na kuchuchumaa kwa kutumia msaada wako. Pia, anafahamu jinsi ya kuvitembeza vitu kutoka mkono mmoja hadi mwingine kwa urahisi.

Kuanza kutembea kwake kunakaribia katika hatua hii, miezi michache ijayo!

Ni muhimu kwako uwe makini zaidi na vitu vyenye hatari ya kumkaba, kwa watoto wa miezi kumi wana uraibu wa kuokota vifaa vidogo vidogo, kwa kupitia uwezo ulio imarika wa kuviokota vitu.

Vidokezo
  • Katika umri huu, usalama wa nyumba wa mtoto ni wa muhimu zaidi.
  • Je, utamihiza ukuaji wa kutembea katika mtoto wako kivipi? Ongeza sauti ya muziki na umhimize mwanao kucheza kulingana na muziki! Hii itakuwa salama kwa uwezo wake wa ukuaji.

Wakati wa kuongea na daktari wako:

Kama ilivyo katika hatua zote za ukuaji wa mtoto wako, ukiangazia hatua muhimu za ukuaji, itakusaidia kujua wakati ambapo mtoto wako anawachwa nyuma.

Tazama iwapo mtoto wako analemewa na uzito wake ama anashindwa kukaa chini na kujisitiri ama kutembeza vitu kutoka mkono mmoja hadi mwingine. Iwapo unagundua mojawapo ya mambo haya, pata ushauri wa mtaalum wa watoto kwa kasi.

 

nini mtoto wako anachofanya siku hizi?

Ukuaji wa kiakili

Mtoto wako wa miezi tisa anataka kuyajua mengi, na ni muhimu kuikuza hali hii ya kutaka kujua mengi kwa kumkubalisha aijue dunia iliyo kando yake. Mtembeze nje na umkubalishe kucheza na vifaa vya nyumbani kuhimiza ukuaji wake wa kiakili.

Atakuwa pia na hamu ya kucheza mchezo wa kujifichiwa, kwani kutamihiza hamu yake ya kuvitafuta vitu vilivyo fichwa. Atapenda pia kuviona vitu vinavyo anguka.

Vidokezo:

Katika hatua hii, watoto wanafahamu jambo la vitu kuwa hapo milele (kuwa hata kama hawakioni kifaa, bado kiko). Himiza jambo hili kwa kumfichia vitabu na vidoli ili avitafute.

Wakati wa kuongea na daktari wako:

Wakati unao paswa kuwa na wasiwasi. Iwapo mwanao anatatizika kuwafahamu watu ambao kwa mara nyingi huwa karibu naye ama ana matatizo ya kuvifuata vitu na macho yake unapo mwelekeza. Ashiriana na daktari wa watoto ili kujua mbona ukuaji huu umechelewa.

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

social development

Watoto wa miezi kumi hupenda kuwaiga watu! Tumia uso wako kama kifaa cha kumfunza. Fanya ishara za uso za kuchekesha na maneno yenye mkazo - hii ni njia bora ya kukuza uwezo wake. Katika umri huu, mtoto wako huenda akaanza kuwa na uwoga wa watu wageni na kuanza kulilia watu wanao wapenda.

Katika wakati hasa, huenda akadhihirisha tabia fulani. Kama vile kujigongesha kichwa, kubingirika, kuvuta nywele, kama njia ya kuashiria mazingira yasiyo mpendeza.

Vidokezo:

Kuwa mwangalifu zaidi. Ataanza kuwa na machozi mengi ambayo hakuwa nayo hapo awali, kama vile anaposikia kelele nyingi ama radi.

Wakati wa kuongea na daktari:

Katika miezi kumi, watoto wanapaswa kuashiria kusikia sauti ama matendo, lugha ya watoto na kuwaangalia watu kwa urahisi. Iwapo unapata kuwa mwanao hana ishara ya vitu hivi, ni wakati mwema uongee na mtaalum wa watoto.

Mazungumzo na Lugha

Akili ya mtoto wako inayo kua kwa kasi inamsaidia kubainisha maneno zaidi. Kwa mfano, majina kama "mama, dada" huenda yakawa ni majina yake ya kila siku.

Vidokezo: 

Himiza uwezo wa kuzungumza wa mwanao kwa kumhusisha katika kuongea naye, kumsomea na  kumwimbia. Watoto wengi huweza kuyaelewa maneno zaidi yanapo semwa kwa kuimba.

 Wakati wa kumwona daktari:

Usitie shaka iwapo mtoto wako anaonekana kuwa mtulivu zaidi. Ni asili kwake kuwa na hisia mbali mbali katika umri huu. Ila, unapaswa kuwa na shaka iwapo ana tatizika kusema maneno kama "mama", "baba" ama "dada".

 Afya na Lishe

Kwa sasa, meno ya kwanza ya mtoto wako ya kwanza inapaswa kuwa imetokea, kwa hivyo ako tayari kukila chakula kitamu kilicho kikubwa kuliko alivyo zoea, kama vile uji! Vipunguze vyakula vigumu, huenda ikawa ni fikira njema. Chakula kipya ni kitamu, pia kinasaidia mtoto wako kuimarisha uwezo wake wa kuvichukua vyakula na kuviweka mdomoni.

Kama tulivyo sema katika makala yaliyo pita, ni kwako mama (na watoto) kuamua wakati wa kumwanzishia mwanao chakula. Katika umri huu, ni wakati mwema kuongeza aina za matunda, mboga, nafaka na nyama unazo mlisha.

Vidokezo:
  • Kuwa makini kwa chakula ambacho kina hatari ya kumkaba kama vile zabibu na vitamu tamu vinginevyo.
  • Chukua kijiko kilicho rahisi kushika na umkubalishe mwanao kujikulisha.
  • Kumbuka kukiekelea kipande cha nguo juu ya meza ama chini ya kiti kwa urahisi wa kusafisha, kwani itakuwa kazi ngumu inapo anza! Lakini kumkubalisha mtoto wako kuwa huru zaidi ni muhimu katika hatua hii ya uzazi.
  • Kwa ukuaji wa mwanao, fahamu kuwa urefu wa kimo katika mtoto wako wa miezi kumi ni 69.7 hadi 74.2 na uzito wa kilo 8.0 hadi 9.9.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo urefu wa mwanao na uzito wake ni chini ya unaohitajika katika hatua hii, shauriana na daktari maalum wa watoto anaye mshughulikia mwanao ili ushauriwe jinsi ya kuuimarisha ukuaji wake kwa njia bora zaidi.

Ni matumaini yetu kuwa makala haya yatakuwa yenye umuhimu kwako. Je, nini ambacho mtoto wako wa miezi tisa anaweza kufanya?

Sources: WebMD, MayoClinic

*Disclaimer: This is the median length and weight, and head circumference according to WHO standards.

Previous monthBaby development and milestones: your 9 month old

Next month: Baby development and milestones: your 11 month old

Republished with permission from theAsianparent

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio