Ukuaji na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi minane

Ukuaji na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi minane

What might your baby be doing and learning this month?

Naam, huu ni umri wa kupendeza! Mtoto wako wa miezi minane ana mashavu ya kupendeza na huenda ukataka kumbusu siku yote!

Ni mwezi wa kufurahisha kwenu nyote kwani karibia wakati huu, mtoto wako anatembea kwa sana. ( fikiria kuhusu usalama wa mwana0)

Huenda anazitoa sauti nyingi za kupendeza, na hata ingawa hataanza kwa kuyasema maneno mwafaka, itikia miito yako kwa sauti ya kizazi utakayo chagua. Walakini, anawaogopa watu wageni anaopatana nao. Kwa hivyo hata tabasamu kwa nyanya barabarani, kwa sababu wasiwasi umemuingia.

Je, una azimia nini kutoka kwa mtoto wako mwezi huu katika ukuaji na hatua muhimu? Tuna angazia!

Ukuaji na hatua muhimu za mtoto wako wa miezi minane: Je, anakua ipasavyo?

 

8 months old baby development and milestones infographic

Ukuaji wa Kifizikia

Watoto wengi wameanza kutambaa kwa sasa, ila, usiwe na wasiwasi iwapo mtoto wako hajaanza bado. Baadhi ya watoto huanza kutambaa mapema, na wengine huenda wakairuka hatua hii na kuanza kutembea.

Badala ya kutambaa, mtoto wako huenda akatembea kwa tumbo, kuchuchumaa, ama kubingirika.

Mtoto wako wa miezi minane ameimarisha uwezo wake wa kutembea. Kwa hivyo, huenda ukagundua kuwa mtoto wako mdogo anajaribu kufika chumbani kukifikia kidoli chake, ama kucheza na vidoli kwa urahisi na mipira ya watoto.

Kwa kujitayarisha kwa hatua hizi zote muhimu, mtoto wako huenda anatayarisha kusimama kwa kujishikilia kwenye kiti ama meza iliyo chini. Kumbatio lake - anapo tumia kidole cha gumba na kidole cha pili kuviokota vitu- kumekua kwa sasa.

Kupiga mikono na kukitikisa kichwa pia kumekua katika mwezi huu. Usisahau kupiga mikono na kukitikisa kichwa pamoja naye!

Vidokezo

 • Vijidoli vyema vya mtoto wako kuimarisha uwezo wake wa kutembea ni vikombe vya plastiki vinavyo ingiana, na vitu vya kupanga.
 • Kwa sababu ni mwerevu sana na ukumbatiaji wake, kuwa makini na vifaa vidogo ambavyo anaviokota na kuviweka kwenye mdomo ama kuvisukuma kwenye mapua yake.
 • Kumbuka kuwa iwapo kitu ni kidogo sana, huenda kikawa na hatari ya kukabwa na koo na kuhatarisha maisha yake.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako:

 • Hawezi simama kwa miguu yake anapo patiwa msaada
 • Hawezi kaa bila ya msaada

mtoto anatambaa

Ukuaji wa Kiakili

Mtoto wako wa miezi minane anapenda kuviangusha vitu sakafunikisha kuviokota? Iwapo huenda jambo hili likawa la kuchosha linapo rudiwa mara nyingi, ina onyesha ukuaji wa kiakili wa mwanao kwa kuelewa kwa jambo la kusababisha na athari. Nikiangusha hiki, mama anakiokota.

Ishara zingine za ukuaji wa kiakili huenda analeta tabia alizo zizoea kwa njia mpya kukubana na tatizo analo kabiliana nalo. Kwa mfano, huenda akakifikia kidoli chake anacho kipenda zaidi na kutambaa katika wakati ule ule.

Kwa wakati huu, zidi kucheza michezo naye ili kukuza uwezo wa kujua vitu vinadumu.

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

ukuaji na hatua muhimu

Usiwe na shaka iwapo mtoto wako hana urafiki na watu wageni ama watu asio wafahamu kamwe. Ni kwa sababu anaanza kutofautisha kati ya mambo anayo yafahamu na asiyo yafahamu, na si la kushangaza kuwa huenda akaonekana mwenye woga anapokuwa miongoni mwa watu wageni.

Vidokezo kwa wazazi

Mtoto wako anaanza kuwaogopa watu wageni, hii ni hatua kubwa katika ukuaji wa hisia na uingiliano wake.

 • Kufuati hatua hii, usimlazimishe kwenda kwa watu asio na starehe kwenda kwao, hata wanapo mwuliza aende kwao ama wanapo jaribu kumbeba ama kumpakata. Jaribu kumwelezea kwa upole na kwa udhibiti! Kuwa mtoto wako anapitia hatua ambayo hana starehe kuwa miongoni mwa watu asiowafahamu.
 • Wahimize wampe mtoto wako muda ili aweze kuwajua, huenda akawa pongeza kwa tabasamu ama kuwapakata!

Tabasamu la kupendeza zaidi, kicheko cha kufurahisha, kwa sasa, zimehifadhiwa za watu anao wapenda zaidi -  familia yake!

Wakati wa kuwa na wasiwasi

Iwapo mtoto wako wa miezi minane hatambui sura za kawaida, haonekani kuitikia anapoitwa, unapaswa kuongea na daktari wako.

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

mtoto wako wa miezi minane

Uwezo wa kuongea unaonekana bila fiche katika mwezi huu katika njia ya sauti za kitoto za kupendeza!

Usiwe na shaka sana kuwa mtoto wako anamwita kila mtu 'mama'. Kwa wiki fupi zijazo, atasoma jinsi ya kulisema jina hilo kwa mtu anaye faa. Jaribu kumwuliza mtoto swali. Hata kama hatajibu kwa kutumia maneno, huenda ukashangazwa kwa kuona ishara ndogo kuonyesha kuwa anaelewa na ameitikia.

Vidokezo kwa wazazi

Huu ni wakati murua kabisa wa kuingiliana na mtoto wako na kumsaidia kukuza uwezo wake wa lugha. Unaweza chagua lugha moja, mbili ama zaidi za kumwongelesha mtoto wako, na ni sawa!

 • Endelea kuzungumza na mtoto wako mchanga, hata ingawa mwitikio bora zaidi utakao upata kwa swali lako ni "BA BA DA DA"! Muingiliano zaidi utamsaidia mtoto wako kukuza uwezo wake wa lugha kwa upole na utaratibu.
 • Huu ni umri ambao baadhi ya wazazi huwaanzishia watoto wao lugha ya ishara. Ambayo huenda ikawa kifaa muhimu kwa mtoto wako anapo taka kujieleza kama vile anavyo kasirika kwani ana lugha duni.
 • Huenda mwanao akaonyesha hamu na upole anapo sikiza hadithi mwezi huu. Kwa hivyo iwapo hakuwa na hamu na vitabu mwezi uliopita, jaribu tena sasa.
 • Huenda ukagundua kuwa mtoto wako anavipenda vitabu vingine zaidi ama hadithi fulani. Huenda lika husishwa na rangi anazo penda zaidi, michoro ama jinsi unavyo soma hadithi zingine. Kumsomea mtoto ni njia ta kupendeza ya kuingiliana naye na pia kumsaidia kukuza uwezo wake wa kuongea na lugha.
Wakati wa kutia shaka

Iwapo katika wakati huu, mtoto wako wa miezi minane bado hajaanza kujaribu kuyatamka maneno. Haonyeshi ishara za kutaka kuingiliana nawe unapo jaribu kumwongelesha, hakikisha umemwuliza daktari wako unapo enda kumtembelea.

Afya na Lishe

Ukuaji na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi minaneKatika umri huu, mtoto wako anapaswa kuwa na uzito wa kilo 7.7 hadi 9.6 na mwenye urefu kati ya 64.4 na 72.8 cms. Usitie shaka, iwapo mtoto wako ana uzito ulio chini borake hatua zinginezo muhimu ziko sawa.

Katika umri huu, mtoto wako ana uwezo wa kula vyakula vya vidole.

Vidokezo kwa wazazi

 • Kwani mtoto wako anaweza kukumbatia vizuri kwa sasa, jaribu kumpa vyakula ajishikie kama vile ndizi ama parachichi ambazo anaweza kushika mwenyewe.
 • Kwa wakati wote, hakikisha kuwa unakata vipande vidogo na usimpe chakula kilicho kigumu zaidi, wala si vipande vikubwa, kwani huenda vikamfanya akabwe. Epuka vyakula kama zabibu na karanga kwani huenda vikamfanya akabwe koo.
 • Masaa ya lishe yanaanza kuwa ya kuvutia kwa sasa na unapaswa kuanza kumpa vyakula mbali mbali. Usiwe na wasiwasi iwapo idadi ya maziwa anayo yakunywa yanapungua - ni kawaida kwani anakula vyakula vinginevyo.

Mama na baba, kumbuka usidhubutu kumwacha mtoto wako bila ya kutunzwa anapo kula.

mtoto wako wa miezi minane

Wakati wa kutia shaka

Iwapo mtoto wako anaakunguka chini ya asilimia ya 5 ya ukuaji, kiurefu na uzito, pata ushauri wa daktari.

Vidokezo zaidi
 • Hakikisha kuwa usalama wa mtoto umeangaziwa kwenye nyumba yote kwani mtoto anatembea kwa sana. Ni muhimu kuvifunga vyumba vilivyo hatari kwake kama vile jikoni na bafu.
 • Mtembeze mtoto wako mara nyingi iwezekanavyo. Naam, hewa safi ni bora kwake, pia matembezi haya yatamwelekeza kwa vitu vingi vipya vitakavyo athiri ukuaji wake wa kiakili.
 • Watoto wanapenda kutazama televisheni ila, usihimize tabia hii katika umri huu mdogo. Iwapo unahisi kuwa mtoto wako anahitaji kuburudishwa, mpe kwa njia ya kusoma, kuimba ama kupiga ngumzo na kuingiliana naye.

Iwapo mtoto wako hajaanza hatua muhimu zilizo tajwa kwenye makala haya, usitie shaka. Kila mtoto hukua katika wakati wake.

Walakini, iwapo una wasiwasi, pata ushauri wa mtaalum wa watoto unaye husika naye.

Source: Web MD

*Disclaimer: This is the median length and weight, and head circumference according to WHO standards.

Previous month:

Next month: Baby development and milestones: your 9 month old

Republished with permission from theAsianparent

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio