Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Minne

Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Minne

Your 4-month-old baby is becoming more curious, adventurous, and quite the taster! So here's what you should be prepared for now.

Mtoto wako wa kupendeza kwa sasa ni "mkubwa", miezi minne na ni miongoni mwa hatua za kupendeza zaidi ya maisha yake machanga. Kwa sasa, anaweza kujieleza, na utampata akitabasamu, akitoa sauti za kitoto ama hata kucheka.

Kama mzazi mchanga, utaona mabadiliko mengi ya kifizikia kwake.

Katika mwezi wa nne, mwanao ana unono wa kupendeza, na huenda utashindwa kujidhibiti kuto yachuna mashavu yake yaliyo jaa. Ila, huu pia ni wakati unapopaswa kujitayarisha kuwa na hisia nyingi - nyingi zaidi kwa kiwango ambazo ukifikia kitambaa cha mkono uyapanguze machozi yako.

Je, nini kitaendelea, utauliza? Haya ni baadhi ya mabadiliko utakayo yaona mtoto wako anapofikisha mwezi huu!

Mtoto wa miezi minne, ukuaji wake na hatua muhimu: Je, mtoto wako anakua ipasavyo?

 

hatua za ukuaji

Ukuaji wa kifizikia

Katika mwezi wake wa nne, ukuaji wa mwanao wa kifizikia utakuwa wa kasi zaidi. Katika wakati huu, uzito aliozaliwa nao unapaswa kuwa umeongezeka mara mbili.

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mwanao* unapaswa kuwa ifutavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 64.0 cm (25.2 inchi)
  – Uzito: 7.0 kg (15.4 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 62.2 cm (24.5 inchi)
  – Uzito: 6.6 kg (14.6 lb)

Na kipenyo cha kichwa cha mwanao* kinapaswa kuwa:

 • Wavulana: 41.6 cm (16.4 inchi)
 • Wasichana: 40.6 cm (16.0 inchi)

Utagundua kuwa anajaribu kukishikilia kichwa chake bila kutumia msaada wowote. Iwapo mwanao anapenda kuwa hai wakati wote, utamwona akijaribu kuisukuma miguu yake chini unapomwekelea mahali pagumu.

Kwani bado ndio ameanza kujua jinsi ya kutembea zaidi katika mwezi huu, utakuwa unaikimbilia kamera yako ili uweze kurekodi anapogeuka kutoka kulala kwa tumbo na kujilaza kwa mgongo. Kwa sasa, utamwona akijaribu kuileta mikono yake karibu na mdomo wake ama kuvisukuma viwiko vyake anapolala kwa tumbo.

Katika hatua hii, chochote ambacho mwanao atakiokota huenda akakipeleka mdomoni. Kwa hivyo, iwapo una kijidoli kinacho toa sauti ama kinacho toa mwangaza, mwanao atajaribu kukishikilia, kukitikisa ama kukiweka mdomoni. Unapaswa kuwa tayari kuwa huenda ikawa ni nywele zako!

Huenda mwanao akaanza kujiviringisha kwa sasa. Baadhi ya watoto wa miezi minne huenda wakapata jino lao la kwanza!

Kwa wakati huu, macho ya mwanao yataambatana anapo kitazama kitu kinacho tembea ama kifaa chenye rangi ya kupendeza. Hii ni kwa sababu uwezo wake wa kuona utafika 20/40. Pia ataweza kuchukua rangi tofauti na kuzilinganisha. Kwa hivyo unapo gundua kuwa mtoto wako bado ana matatizo ya kuyaambatanisha macho pamoja, ama ana angalia pande tofauti, mwelezee mtaalum wako wa watoto.

Vidokezo
 • Usalama kwanza! Kumbuka kuwa unapomshika mwanao, unapaswa kutoa vifaa vyenye ukali wowote kama vile herini, ama mikufu. Kwa sababu iwapo vina meta meta, bila shaka atajaribu kuvivuta na kuviweka kwenye mdomo wake. Atafanya hivi kwani ameigundua mikono yake na anajaribu kuitumia.
 • Huenda anageuka na kujilaza kwa tumbo bila msaada, ila, iwapo bado hajaanza, endelea kumpa wakati wa tumbo.
 • Mtafutie zoezi za mtoto. Atafurahikia jambo hili. Huenda akataka kukaa ama kusimama kwa kupitia msaada wako. Ila, kumbuka kuto msimamisha ama kumkalisha kwa wakati mrefu kwani huenda akapata matatizo ya magoti.
 • Mpe mwanao vifaa vingi vya kugusa kama vile vitabu na vijidoli laini. Huu ni wakati ambapo huenda akakiangusha hiki na kuchukua kijiko. Mpe kijiko cha mbao. Hakikisha kuwa kifaa chochote kile si kidogo sana ambacho anaweza meza. Na wala si kikubwa sana cha kumwumiza. Cha muhimu zaidi, hakikisha ako kando yako wakati wote anapocheza.
 • Anza kutayarishia mtoto ambaye ako tayari kuanza kutembea kwenye nyumba. Unaweza ongeza milango kwenye ngazi iwapo unazo kwenye nyumba, hakikisha nyumba haina vifaa ambavyo huenda vikamwumiza.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hapendi kuhusika katika shughuli zozote
 • Haonyeshi ishara zozote kwa sauti yako
 • Haurushi mkono wake hewani ama kujaribu kuupunga
 • Ana matatizo kukigeuza kichwa chake

Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Minne

Ukuaji wa Kiakili

While you notice all these physical changes in him, you’ll also be surprised to notice his fast cognitive development during this month.

Your 4 month old baby will also respond to your affections more often. So when you call out to him he may look at you and smile, in recognition or your affection for him.

Also, his hand and eye coordination will have improved by this time. So this means he will spot objects and reach for them more effectively. Since his motor skills have developed further, you will also notice him spotting an object and moving his eyes along with it.

Vidokezo
 • Cheza mchezo maarufu wa 'peek-a-boo' na mtoto wako wa miezi minne na utazame anapokupa tabasamu la kupendeza!
 • Shiriki uwezo wake vyote uwezavyo. Jaribu kumwita ukiwa pembe tofauti za nyumba
 • Msomee vitabu vilivyo jaa miundo na marangi
 • Mtembeze kwa kutumia kifaa cha watoto cha kutembelea chake! Epuka wakati mwingi wa kutazama televisheni
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hatabasamu ama hapendi kuingiliana nawe ama na wengine
 • Havishiki vitu ama vijidoli
Ukuaji wa muingiliano na hisia

Katika ukuaji wa mwanao wa hisia na uingiliano, utafurahikia kugundua ukuaji fulani katika mwezi huu. Mwanao ana uwezo wa kujieleza kihisia, atatabasamu kwa urahisi. Je, una uhakika jambo hili halitaifanya siku yako kuwa njema?

Ila mwitiko kwa hisia zako na uwezo ulio ongezeka wa kujieleza utaandamana na kiwango cha machozi yao.

Iwapo unapenda kucheza na mwanao kisha uwache, huenda ukamkasirisha. Ila usiwe na shaka, jambo hili ni geni kwake. Katika umri huu, anapendelea kucheza nawe na pia ataweza kukujulisha anapotaka uwache ama uendelee.

Pia unapo mwonyesha miigo ya uso, usiwe na shaka anapo jaribu kukuiga. Katika umri huu wa kupendeza, watoto huwa na uraibu wa kuiga wanacho kiona. Miongoni mwao ikiwa miigo ya kufurahisha ya uso.

Baada ya yote yale, aliyasoma kutoka kwa mamake!

Vidokezo 
 • Mtoto wako mwenye mashavu huenda anavifanya vitu kupata mwitikio wako, kama vile kuzivuta nywele zako ama kukuuma anapo nyonya. Kusema "apana" kwa udhibiti na kwa sauti ya upole imetosha kuashiria hauja furahikia jambo lile.
 • Anza kutumia michoro yenye rangi zingine mbali na rangi tatanishi (nyeupe, nyeusi, nyekundu) na pia kelele.
 • Ingiliana na mtoto wa miezi minne unapo msomea ama kumwimbia.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Haonyeshi ishara zozote (za furaha/ kukasirika/ uwoga) kwa sura mpya

mtoto mchanga

Ukuji wa Mazungumzo na Lugha

Mwanao anapofikisha umri wa miezi minne, uwezo wake wa kujielezea utaongezeka. Ataweza kukueleza iwapo anafuraha ama amekasirika na mengineyo. Hata kama haitakuwa kwa kutumia maneno, ila kupitia tabasamu lake, sauti za kitoto ama machozi.

Najaribu kuelewa jinsi atakavyo kua, tusisahau kwamba mwanao mchanga atayafuata yote uyafanyayo.

Kwa hivyo unapo mwita mwanao "kipenzi changu" kwa kutumia sauti ya kuimba wimbo, fahamu kuwa mwanao atajaribu kuiga ulichosema - hata kama hata sema hasa ulicho kisema. Huenda pia akaanza kuyatamka maneno kwa sasa.

Vidokezo
 • Kuhimiza ukuaji wa mwanao wa lugha, jaribu kuongea naye kama unavyo ongea na mtu mzima. Utafiti umedhibitisha kuwa kutumia sauti ya kuimba wimbo ni njema kwa watoto. Inawasaidia kujua kuongea kwa urahisi.
 • Tumia sentensi kamili na lugha sanifu. Tumia maneno kama vile "tafadhali" na "asanti." Hata kama mwanao bado haielewi lugha na maana ya maneno haya, ataweza kuelewa kulingana na utumizi wake katika sentensi na kujua maana yake katika wakati ujao.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hatoi sauti za kitoto ama sauti zozote zile
Afya na Lishe

Kwa sasa, mtoto wako anapaswa kuwa na uzito wa kati ya kilo 6.2 na 7.8. Urefu wake kati ya 58 na 66 cms. Kwa kuyasema hayo, huenda kuna tofauti katika mtoto aliye na afya bora. Kwa hivyo, fuata ukuaji wake kwa kutumia chati za asilimia. Kwa kawaida, watoto hufuata asilimia wanapokua.

Kwa chakula, mwanao anahitaji maziwa ya mama peke yake yanayo badilika mwezi baada ya mwingine kuyakimu mahitaji yake ya virutubisho.

Kwenye mwezi huu wa nne, mwanao mchanga huenda ana ratiba maalum ya kulala anayo ifuata. Kwa kawaida, mtoto hulala kwa masaa masaba au nane katika umri huu. Na ukitia akilini kulala mara kama moja ama mbili, utagundua analala kwa masaa yasiyo pungua 12 ama 13 kila siku.

Katika umri huu, mwanao atapata dosi ya pili ya 5 ndani ya 1, dosi ya pili ya chanjo ya Rotavirus na dosi yake ya kwanza ya PCV.

Vidokezo
 • Endelea kunyonyesha kama kawaida. Mwulize daktari wako iwapo mwanao anahitaji tembe za vitamini D za kuongeza
 • Usiwakubalishe wanao m-beba mwanao kumlisha vyakula vigumu bado, haija lishi ushauri watakao kupa
 • Mwulize mtaalum wako wa watoto kuhusu kumpa mwanao dawa za mafua
 • Endelea kufuata mwongozo salama, unaohusisha kumwekelea mtoto chini kwa mgongo anapolala, na kutoa blanketi za ziada ama vijidoli kwenye kijitanda chake.
 Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hakui kulingana na kimo kinacho hitajika, ama anapo anguka chini ya asilimia 5 cha ukuaji wa miaka yake
 • Ana joto jingi ya 38 degrees Celsius ama zaidi
 • Iwapo ana upele, kukwaruzwa ama ameshuhudia ajali ya kugongwa kichwani
 • Anatapika mara kwa mara.

Source: Web MD

Mwezi uliopita: Baby development and milestones: your 3 month old

Mwezi ujao: Baby development and milestones: your 5 month old

Republished with permission from theAsianparent

*Tahadhari: Hiki ni kimo cha urefu na uzito, na kipenyo cha kichwa kulingana na vipimo vya WHO)

Written by

Risper Nyakio