Ukuaji na Hatua Muhimu za Mtoto: Mtoto Wako wa Miezi Mitano

Ukuaji na Hatua Muhimu za Mtoto: Mtoto Wako wa Miezi Mitano

Your baby will start to roll over, crawl, and sit upright. Here's what else you can expect in your baby's fifth month.

Hongera! Mtoto wako ameipita hatua ya miezi minne ambayo ingehakikisha unakimbia wakati wote! Na unapo sherehekea kuwa mtoto wako mchanga anakaribia kufikisha miezi sita, kuwa tayari kuviona vitu vipya kwani huu ndio wakati ambapo mtoto wako wa miezi mitano ataanza kuyatamka maneno, kujiviringisha ama hata kutambaa!

Haya ni baadahi ya mambo ya kuazimia mwanao anapofikisha miezi mitano.

Ukuaji na Hatua Muhimu Kwa Mtoto wa Miezi Mitano: Je, mwanao anakua ipasavyo?

Ukuaji na Hatua Muhimu za Mtoto: Mtoto Wako wa Miezi Mitano

Ukuaji wa Kifizikia

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mwanao* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 65.9 cm (25.9 inchi)
  – Uzito: 7.5 kg (16.6 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 64.0 cm (25.2 inchi)
  – Uzito: 6.9 kg (15.2 lb)

Na kipenyo cha kichwa cha mwanao* kinapaswa kuwa:

 • Wavulana: 42.6 cm (16.8 inchi)
 • Wasichana: 41.5 cm (16.3 inchi)

Kuna idadi ya hatua muhimu unazo azimia kuanza kuziona katika wakati huu wa mapema katika mwezi wa tano wa maisha ya mwanao. Katika wakati huu, watoto wengi huanza kukaa chini kwa muda mrefu.

Ila, huenda wakahitaji msaada kidogo. Kwa hivyo tumia mto kumpa mtoto wako wa miezi mitano msaada anapojaribu kukaa. Hatimaye, unapo ona kuwa mtoto wako anastarehe akikaa chini, jaribu kumfunza kukaa kwenye kiti chake cha juu na umsaidie kukaa na jamii wengine wakati wa mlo.

Iwapo mwanao hajaanza kubiringika bado, kuna uwezekano ataanza kujaribu kufanya hivi katika mwezi wa tano na baadaye kulifanya jambo hili kwa urahisi. Ina maana kwamba unapaswa kuwa makini zaidi unapo mwacha peke yake. Tuna kushauri kuwa ingekuwa bora zaidi unapo mwacha mwanao kwenye mkeka unapofanya kazi zako za kinyumbani kuepuka visa vyovyote vyake kuanguka.

Watoto wengi wa miezi mitano huanza kutambaa na kuchuchumaa iwapo bado hawajaanza tayari. Watoto pia huanza kuifanya miguu yao kazi, kuishikanisha pamoja, kwa machache, juhudi nyingi za kutembea tembea.

Uwezo muhimu ambao mtoto wako hupata katika miezi mitani ni wa kukumbatia. Utagundua kuwa mtoto wako anaweza kuvikumbatia vidoli vyake ama kijikombe chake kwa urahisi. Pia kupitisha vyombo kutoka mkono mmoja hadi mwingine. Hii ni hatua kubwa!

Vidokezo

 • Hakikisha kuwa humwachi mwanao anayetembaa na kujibiringisha, kwani mtoto wako wa miezi mitano ako hai zaidi na huenda akajiumiza.
 • Kumlinda mwanao ni muhimu, kuhakikisha ako salama wakati wote.
 • Mhusishe katika shughuli zitakazo mhimizia kutembea, kama vile kukiweka kidoli chake mbali naye anapokuwa amelala kwa tumbo. Huenda akawa mkubwa zaidi wa kumfanyisha mazoezi wakati wowote, hakikisha umeyafanya yote uwezavyo.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Ana matatizo ya kukiweka kichwa chake vizuri
 • Aba tatizika kukipindua kichwa chake kutoka upande mmoja hadi mwingine

 

mtoto wa miezi mitano

Ukuaji wa kiakili

Katika umri wa miezi mitano, mtoto huanza kuwa na fahamu yake, na kwa kugusilia, kukuonyesha aina ya mtoto ambaye atakuwa kwa miezi michache ijayo- furaha, kujieleza, kukasirika ovyo ama mwenye hisia nyingi. 

Mtoto wako wa miezi mitano anajieleza zaidi na pia kuonyesha hisia. Atajaribu kukuangalia kwa muda mrefu, huenda akijaribu kuisoma midomo yako na kuelewa unacho kisema.

Baada ya muda, utagundua kuwa mtoto wako anajaribu kuelewa sauti zote anazo zisikia, kama vile kuimba kwa nyuni, sauti ya vidole na mbwa kubweka kwa jirani.

Vidokezo

 • Himiza kila mmoja wa familia yako kuongea na mtoto wako ili kuukuza uwezo wake wa kuongea.
 • Mtafutie mtoto wako wa miezi mitano vidolo vinavyo toa sauti ama vinavyo mshirikisha katika njia zinginezo.
 • Ambatanisha sauti na kielezo. Kama vile mbwa unaye mueka nyumbani anaopo bweka, sema " Sikiza mwanangu! Sammy ana bweka.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Haonyeshi ishara za kusikia makelele ama anapokuwa katika mazingara mapya
 • Hana ishara za hisia zozote

mtoto wa miezi mitano

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Wakati ambapo mtoto wako bado hajakua ipasavyo kueleza kukasirika, kufurahikia ama kuhuzunika kwake, katika miezi mitano, anapaswa kuwa akijieleza zaidi. Kuonyesha hisia zake za upendo, kupendezwa ama kuwafurahisha watu.

Huenda akachekeshwa na kila jambo ndogo, kama vile unavyo mwita jina lake ama unapo mchezesha.

Vidokezo kwa wazazi

 • Mfanye mtoto wako acheke kisha urekodi jambo hili! Hakuna wakati ambapo tabasamu lake na vicheko vyake vitakuwa vingi kama wakati huu.
 • Mchekeshe mwanao!
 • Tafuta michezo ya kuigiza ya watoto kisha umshirikishe mwanao.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Iwapo mwanao kamwe hajishirikishi nawe ama na wengine.
Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Uwezo wa mtoto wako wa kuzungumza utakua juu zaidi katika mwezi huu. Pia huenda akapata kipawa cha kuchekesha.

Kwa ghafla, utagundua kuwa sauti za kitoto za mwanao zimeongezeka na ataanza kutamka maneno yake ya kwanza ya "da-da," "ba-ba," na "ma-ma." Pia ataanza kuitikia unapomtaja ama unaposema kitu ambacho anakitambua, huenda pia akatoa kicheko cha kitoto cha kufurahia.

Vidokezo

 • Iwapo bado hujaanza, huu ni wakati ambao unaanza kumsomea mtoto wako ili kuongeza matamshi yake kwa kusoma vitabu vya watoto.
 • Pia huenda ukajaribu maneno ya kawaida kwa mwanao unayo yatumia kila siku kama vile "maziwa" na "lala."
 • Fahamu kuwa unapo waongelesha wanao, tumia maneno yaliyo sahihi na sio ya kutungwa kama vile "mazi" badala ya "maziwa" kwani mtoto wako hatajuwa ni ya kutungwa wala si ya kweli.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hatoi sauti zozote.mtoto wa miezi mitano
Afya na Lishe

Mtoto wako anakua kwa kasi sana na njaa yake pia imeongezeka kwa sana kutoka mwezi uliopita akijitayarisha kwa vyakula vigumu mwezi ujao. Anapaswa kuwa na uzito kati ya kilo 6.7 hadi 8.4 na anapaswa kuwa na urefu wa kati ya 60 hadi 68 cm. Hayo kusemwa, ni jambo la kawaida mtoto kuwa na tofauti kidogo iwapo amekuwa akifuata asilimia ya ukuaji inayofaa kutoka kuzaliwa kwake.

Katika miezi mitano, mwanao anapaswa kuwa na mfumo mwafaka wa kulala na huenda akalala vyema usiku iwapo amelishwa ipasavyo na hakuna jambo linalo msumbua. Ina maana kuwa utapata muda mwingi kama mama mchanga wa kulala na kupumzika unapo pendezwa na hatua hii. Walakini, ina maana kuwa mtoto wako hatalala wakati mwingi mchana na atakuweka katika hali ya kukimbia kimbia ukimfuata kila mahali.

Hongera kwa kuendelea kumnyonyesha mtoto wako wa miezi mitano! Bila shaka, anapata virutubisho mwafaka zaidi kwa njia hii.

Katika mwezi huu, mtoto wako anapaswa kupata chanjo zifuatazo:

 • Hepatitis B - dosi ya tatu: Chanjo dhidi ya Hepatitis B
 • DTaP - dosi ya tatu: Chanjo dhidi ya Diphtheria, Pertussis & Tetanus
 • IPV - dosi ya tatu: Chanjo dhidi ya Poliomyelitis
 • Hib - dosi ya tatu: Chanjo ya Haemophilus influenza type b
 • Pneumococcal Conjugate - dosi ya pili: Chanjo dhidi ya Pneumococcal Disease

Vidokezo

 • Wakati ambapo watoto wengine hulala vyema usiku, wengine bado wanasumbua, jambo hili ni la kawaida. Msaidie mwanao kwa kucheza muziki wenye upole na kuzima sitima usiku.
 • Kunyonyesha ni njia nzuri ya kukabiliana na uchungu wa sindano. Mnyonyeshe mwanao anapo pewa chanjo.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Anaonyesha kupunguka kwa uzito ama kuanguka chini ya asilimia ya 5 ya ukuaji wa mtoto.
 • Ana joto zaidi ya 38 degrees C.

Wakati wa miezi mitano ya ukuaji wa mtoto ni wakati ambao wazazi hupendelea sana kwani mtoto huanza kujieleza na kuitikia kwa mara ya kwanza. Ifurahikie hatua hii kabisa!

Reference: Web MD

Mwezi uliopita: Baby development and milestones: your 4 month old

Mwezi ujao: Baby development and milestones: your 6 month old

*Tahadhari: Hiki ni kipimo cha uzito, urefu na kipenyo cha kichwa kulingana na WHO

Republished with permission from theAsianParent

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio