Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako wa Miezi Mitatu

Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako wa Miezi Mitatu

The first year of a newborn's life is one of the fastest in human development, so what exactly can your tiny 3 month old baby do now?

Kwa sasa una mtoto wa miezi mitatu! Wakati kweli wapepea. Ilikuwa tu hivi majuzi alipozaliwa. Hivi sasa, mwanao wa miaka tatu anajulikana kama mtoto mchanga wala si mzaliwa wa hivi punde.

Mwanao mchanga amekua sana ila ana mengi ya kusoma bado. Kupitia kwa utunzaji mwema na kumshika kwa mkono ipasavyo, utashangazwa na ukuaji wake katika mwezi wake wa tatu maishani na miezi ijayo. Haya ni baadhi ya mambo ya kuazimia kutoka kwa mtoto wako wa miezi mitatu.

Ukuaji na Hatua Muhimu za Mtoto Wa Miezi Mitatu: Je, Anakua Ipasavyo?

tabasamu la mtoto

Ukuaji wa kifizikia

Kwa sasa, mwanao mchanga amezoea kutumia mikono yake, ataanza kuifahamu dunia inayomzingira kwa kutumia mikono na vidole vyake. Ataanza kuvigusa, kuvihisi na kuvishika vitu vingi. Pia ataweza kuwajua watu wengi tofauti walio karibu naye. Ataanza kuitumia nguvu yake ya kunusa kama njia ya tofautisha watu anaowafahamu na watu wageni.

Kifizikia, kwa sasa anakaa kibonge cha kupendeza. Kichwa chake na mwili wake wanaonekana kutoshana na utaanza kuona miviringo ikionekana kwenye mapaja yake ya kupendeza na mikono yake.

Katika hatua hii, urefu na uzito wa mwanao wa kimo* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 61.4 cm (24.2 inchi)
  – Uzito: 6.4 kg (14.1lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 59.9 cm (23.6 inchi)
  – Uzito: 6.0 kg (13.3lb)

Kipenyo cha kichwa cha mwanao* kinapaswa kuwa:

 • Wavulana: 40.5 cm (15.9 inchi)
 • Wasichana: 39.5 cm (15.6 inchi)

Huenda miezi mitatu ikawa si muda mrefu, ila mwanao mchanga anakuwa kwa kasi kuliko unavyo mdhania. Kwa mfano, mtoto wako wa miezi mitatu anaweza kuitembeza mikono yake kupitia anacho kiona na pia na nguvu za misuli za kutosha kukishikilia kichwa chake.

Hasa, mwanao anapaswa kuwa:

 • Akipata nguvu sawa za mwili wake wa juu, hasa misuli ya shingo na katika wakati wa tumbo (ama anapolazwa kwa tumbo). Anapaswa kuweza kukishikilia kichwa chake na kifua kwa kutumia mikono yake.
 • Kupata nguvu za mwili wa chini. Mwishoni mwa mwezi huu, anapaswa kuweza kuinyoosha miguu yake na kurusha mateke kwa urahisi anapolala tumbo ikiwa chini.
 • Nguvu yake ya kuishikilia na kuidhibiti shingo yake inapaswa kuwa bora. Unapomshika vyema, kichwa chake hakisongi sana kwani anakishikilia kwa kutumia shingo yake.
 • Uwezo wa kimsingi wa kuambatanisha mikono na macho yake, kama vile kuifunga na kuifungua mikono, kuileta pamoja na kuvifuata vifaa vyenye rangi tatanishi vinavyopita mbele ya macho yake.
 • Ilete mikono yake karibu na mdomo wake. Anaweza kuileta mikono yake karibu na mdomo wake, kwa wakati mwingine hata kuvichukua vidoli. Kumbuka kumpa vijidoli vilivyo salama kwa watoto wa umri wake na pia bila ya sehemu ndogo. Vijidoli vidogo huenda vikamezeka kwa ajali na kusababisha hatari ya kukabwa.
 • Kuviringika kwa mgongo. Katika wiki chache, mwanao huenda akaanza uwezo wa kujiviringisha kwa tumbo unapo mlaza kwa tumbo. Kuwa makini unapo m-badili diaper ama iwapo unamchezesha kwenye kitanda.

Utafurahikia kujua kuwa sio mwendo pekee ambao mwanao ana uwezo wa kufanya. Uwezo wake unaokua unamsaidia kuifahamu dunia vyema zaidi, hasa uwezo wake:

 • Uguso. Katika umri wa miezi mitatu, mwanao mchanga anaweza kuvifahamu zaidi vitu vinavyo mzingira. Atakuwa na hamu ya kugusa na kuhisi vitu tofauti. Kando na kuvileta vitu karibu na mdomo wake, mwanao atajua jinsi ya kuileta mikono yake karibu kwa muda wa wiki moja. Huenda pia wakaanza kuvibonyesha vidoli wanavyo vigusa.
 • Sauti. Katika siku chache, mtoto wako anapaswa kuanza kuonyesha hisia anapoisikia sauti yako, kwa kukigeuza kichwa chake upande wako na kutabasamu. Pia, ataanza kuonyesha upendo wake wa kusikiza muziki wa aina tofauti na ataanza kuangalia upande wa kelele nyingi.
 • Kuona. Mwangalie mwanao. Kuna uwezekano kuwa atakuangalia machoni unapo mwangalia. Huenda tayari anaufahamu uso wako, harufu yako, mama! Huenda pia anafurahikia kuitazama sura yake kwenye kioo.

mtoto mchanga

Vidokezo

 • Mpe pete za vijidoli zenye rangi kama vile nyekundu, vijidli vya kutoa sauti ama vyovyote vilivyo sawa katika umri huu ili ajaribu kufikia. Mwangalie anapo jaribu kuvinyoosha kwenye mkono wake na kujaribu kuvileta mdomoni wake.
 • Mpe mwanao vitu tofauti vya kugusa vilivyo tengenezwa na vitu tofauti kama vile velvet, pamba laini. Atafahamu jinsi ya kutofautisha vitu mbali mbali kwa kutumia vidole na misuli yake.
 • Jaribu kuvikusanya vitu vyenye harufu ya kupendeza kama vile maua, keki na kuzipitisha chini ya mapua yake. Kila kitu katika wakati wake ili kuona harufu anayoipenda.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Havishiki vyombo
 • Hawezi kukishikilia kichwa chake vyema
 • Hana juhudi za kuvifikia na kuvishika vyombo kando yake
 • Havileti vyombo kwenye mdomo wake
 • Ana matatizo kusongeha jicho moja ama macho yote mawili katika pande tofauti
 • Anatazama pande tofauti (ila jambo hili huwa kawaida katika miezi ya kwanza michache)

Ukuaji wa Kiakili

Miezi mitatu baada ya kuzaliwa, mwanao mchanga anaanza kuelewa dunia inayo mzingira. Akili yake inayokua inafanya juu chini kuelewa kinacho endelea.

Anaelewa zaidi kisa na athari, kwa kawaida zaidi kwa kuto kipiga kidoli-na kusababisha mwendo wa kidoli hicho. Ataanza kuelewa mambo ya kimsingi ya kisa ( kukigonga kidoli) na athari( kusababisha mwendo wake) katika vitu. Akili yake itaviunganisha vitu vingi anapojaribu kuwa makini kwa gunduo hili lipya.

Katika miezi mitatu, mwanao anauwezo zaidi wa kuvifuata vyombo. Macho yake yanapaswa kufanya kazi kwa pamoja ili kuwa makini na kuvifuata vitu, hasa kitu kinapo tembea mbele yake kama vile mkono wako ama kijidoli.

Vidokezo

 • Mpee mwanao chanzo cha kujua seheu tofauti za mwili. Chukua kidoli kisha umtajie majina ya sehemu tofauti za mwili.
 • Mchokoze. Ufanye mchakato wa kumbadili diaper uwe wa kupendeza kwa kumchezea huku ukisema "beep!" Mwanao mchanga ataufahamu zaidi mkono wako na kutazamia guso lako.
 • Ongea na mwanao. Hakikisha kuwa wakati wote unaongea na mwanao kwa kutumia majina mepesi ama sentensi fupi fupi hata kama bado hakuelewi. Anapenda kuisikia sauti yako!
 • Mpatie shughuli tofauti za kufanya. Kama vile kumueka katika chumba tofauti ili apate vitu tofauti vya kuangalia.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Haonyeshi hisia zozote kunapokuwa na kelele nyingi (kama vile mlango kugongeshwa ama honi za gari)
 • Haigundui mikono yake
 • Hafuati vyombo kwa kutumia macho

miguu ya mtoto

 

Ukuaji wa mwingiliano na hisia

Iwapo mwanao mchanga bado hajaanza kuenda shule ama kupatana na watoto wengine wenye umri sawa, ana maarifa tosha ya kuelewa jinsi ya kuingiliana na wengine kwa kupitia ishara zako za uso, mama na baba!

Utagundua kuwa ataanza kutabasamu anapowaona watu wengine. Tabasamu lake la kupendeza sio lako pekee mama ama baba kwa sasa! Ataanza kuwa mkarimu zaidi kwa yeyote yule anaye tabasamu anapo mwona.

Utu wa mtoto wako wa miezi mitatu unaanza kudhibitika kwa upole, anapozidi kutaka kujua na kuwa na urafiki na wengine. Mchanga wako ataanza kupendezwa na watoto wengine wanao mzingira ama sura yake kwenye kioo.

Anajaribu kuelewa hisia na mazungumzo. Ataanza kuunganisha unachosema na ishara za uso unazo onyesha.

Vidokezo

 •  Mwonyeshe mwanao picha za marafiki na jaa (ama watu kwenye magazeti pia ni sawa), pia mwonyeshe watu wanao tabasamu.
 • Mwangalie mwanao anapo kuangalia na umwongeleshe kwa upole. Jaribu kuiga anacho fanya ama sauti anazotoa.
 • Mwonyeshe tafakari ya sura yake. Eka kioo mbele yake. Kisha ukiashirie na useme jina lake. Hatimaye, mwanao mchanga atajua sura iliyo kwenye kioo.
 • Mwimbie ama ucheze muziki.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hatabasamu anapowaona watu
 • Hatabasamu anapo isikia sauti yako
 • Si makini kwa nyuso mpya, ama anaonekana mwenye woga anapo ona sura ama mazingara mapya

miezi mitatu ya maisha

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Furahikia mama! Malaika wako mdogo anasoma jinsi ya kuingiliana na watu kwa njia zingine mbali na kulia.

Katika umri huu, kulia hakutakua njia ya kipekee ya mwanao ya kuongea. Katika siku zijazo, ataanza kujieleza kwa njia zingine kama vile sauti za kitoto, kucheka, na sauti za voweli kama vile: Oh, Ooh, Ah.

Vidokezo

 • Mhusishe mwanao katika mazungumzo ya kitoto. Unavyo zidi kumwongelesha unamhimiza kuanza kuunda maneno yake hivi karibuni na pia kufanya ishara anapo kuongelesha.
 • Msomee kwa sauti. Mtoto wako mchanga huenda asielewe maneno unayo yasema wala kuyasoma. Ila, kusoma kwa sauti kwa mwanao mchanga kutamsaidia kutofautisha kati ya sauti mbali mbali, maneno na lugha. Pia, kutamsaidia kuvienzi vitabu katika umri mdogo. Chagua vitabu vya watoto vyenye michoro yenye rangi tatanishi ili iiteke macho yake.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hatoi sauti za kitoto
 • Analia kwa sana kwa muda mrefumtoto wa miezi mitatu

Afya na Lishe

Miezi mitatu baada ya kuzaliwa, mwanao mchanga anapaswa kuwa na urefu wa 56.4 -60.4 cm na uzito wa kilo kati ya 4.9 na 6.3.

Kinyume na imani nyingi, watoto katika umri huu hawafai kuvianza vyakula vigumu bado. Masomo yamedhibitisha kuwa kumpa mwanao chakula mapema katika umri huu huenda kukahatarisha maisha yake.

Kwani ufumo wake wa utumbo bado haujakomaa, kuna uwezekano hata weza kukichakata chakula kile. Kumwanzishia chakula kigumu katika umri wa mapema huenda kukamfanya awe na uzito mwingi zaidi ama apate mzio, matatizo ya ufomo wa utumbo ama kukabwa na chakula na kuhatarisha maisha yake.

Kwa kawaida, watoto  hukua tayari kuvila vyakula vigumu  wanapokuwa umri wa miezi sita. Kwa sasa, maziwa yako ya mama yanampa mtoto wako wa miezi mitatu virutubisho vyote anavyohitaji.

Pia, ni muhimu kukumbuka kuwa watoto wanaokua hawahitaji chakula peke yake kukuza mili yao, pia wanahitaji kupata usingizi wa kutosha. Baadhi ya watoto huenda wanalala kwa muda mrefu zaidi wakati wa usiku katika umri huu. Kila mtoto hukua kwa njia tofauti. Kwa hivyo ni sawa ikiwa mwanao bado hajafikisha hatua hii muhimu ya kulala.

Katika umri wa miezi mitatu, mwanao anapaswa kupata chanjo zifuatazo:

 • DTaP - dosi la kwanza: Chanjo dhidi ya Diphtheria, Pertussis na Tetanus
 • IPV - dosi la kwanza: Chanjo dhidi ya Poliomyelitis
 • Hib - dosi la kwanza: Haemophilus influenza type b vaccine
 • Pneumococcal Conjugate - dosi la kwanza: Chanjo dhidi ya ugonjwa wa Pneumococcal

Fahamu kuwa mwanao bado ni mchanga sana, huenda bado akaathiriwa na maradhi yaliyo kawaida kwa watoto kama vile:

 • Virusi vya kupumua (Respiratory Syncytial virus), ishara zake ni kama vile kuwa na homa, kufungana kwa mapua na kupumua kwa nguvu ama sauti ya juu.
 • Maradhi ya mikono, miguu na mdomo (Hand, Foot and Mouth Disease), ishara zake ni kama vile joto jingi, kushikana koo, upele kwenye viganja vya mikono, na sehemu ya kujifunga diaper.
 • Joto nyekundu (Scarlet fever), ishara zake ni kama vile kushikana koo, upele mwekendu kwenye sehemu ya shingo na uso.

Fahamu: Usidhubutu kumpa mwanao dawa kabla ya kuagizwa na daktari maalum wa watoto.

Vidokezo

 • Njia bora zaidi ya kumtuliza mwanao anapo pewa chanjo ni kumnyonyesha.
 • Baadhi ya watoto hupata joto jingi baada ya kupewa chanjo- ongea na daktari wako kuhusu njia bora ya kuepuka jambo hili.
 • Si lazima kumpa mwanao maji iwapo angali ananyonya. Katika siku zenye jua kali, hakikisha unamnyonyesha siku zaidi.
 • Wakati nguvu za mwanao za kujikinga dhidi ya maradhi zinaongezeka kila siku, hazijakomaa sana. Epuka kumpeleka mahali ambapo kuna watu wengi na watu wanapaswa kunawa mikono kabla ya kumbeba.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Ana upele wa kushangaza
 • Ana matatizo ya kupumua ama ana pumua kwa nguvu
 • Ameipoteza hamu ya kula
 • Ana joto jingi ya 37.8 degrees Celsius ama zaidi
 • Anaonyesha ishara za kukohoa ama kuharisha kwa siku nyingi

Ukuaji wa watoto ni tofauti kwa kila mmoja, ila kuna hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miezi mitatu anapaswa kufikisha katika hatua hii. Iwapo una wasiwasi kuhusu ukuaji wa mwanao, hakikisha kuwa umemtembelea daktari wako haraka iwezekanavyo.

References:

WebMD (Baby Development), WebMD (Childhood Illnesses),  HealthyWA,  pathways.org, CDC

Jarida lililo pitaBaby development and milestones: your 2 month old

Jarida lifuataloBaby development and milestones: your 4 month old

Republished with permission from theAsiaparent

*Disclaimer: This is the median length and weight, and head circumference according to WHO standards)

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio