Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

Mtoto wa miezi mitatu ana nguvu zaidi za shingo na pia anaanza kufahamu kinacho tendeka kwenye mazingira yake.

Kwa sasa mtoto wako amefikisha miezi mitatu. Najua unajiuliza wakati umeenda wapi kwani anazidi kukua kwa kasi sana. Inaonekana kama alizaliwa siku ingine na kwa sasa ashakuwa mtoto wa miezi mitatu.

Mtoto wako mchanga amekuja njia ndefu, na bado ana mengi atakayo zidi kusoma. Na utunzi unao faa na ujumbe sahihi, utashangazwa na ukuaji na maendeleo yake mwezi huu, na miezi ijayo. Haya ndiyo mambo unayo yatarajia mwezi mtoto wako akiwa na miezi mitatu.

Ukuaji na Maendeleo Ya Mtoto Wa Miezi Mitatu: Je, Mtoto Wako Anakua Ipasavyo?

Ukuaji wa fizikia

Ukuaji Na Maendeleo Muhimu Katika Mtoto Wa Miezi Tatu

Kwa sasa, mtoto wako ana ueledi wa kusongesha mikono yake, na ataanza kutaka kujua kinacho endelea karibu naye kwa kutumia mikono na vidole vyake. Atakuwa akigusa na kushika vitu vingi. Atajua zaidi watu walio karibu naye na kutumia uwezo wake wa kunusa kama njia ya kutambua tofauti kati ya watu anao wajua na wageni.

Kifizikia, ataonekana ana ufuta zaidi na kunenepa. Na kichwa chake kita toshana na mwili wake. Katika hatua hii ya kukua, uzito na urefu wa mwanao unapaswa kuwa hivi:

 • Wavulana

- Urefu: 61.4 cm (inchi 24.2)

- Uzito: kilo 6.4 (14.1 lb)

 • Wasichana

- Urefu: 59.9 cm (inchi 23.6)

- Uzito: kilo 6.0 (13.3 lb)

Na upana wa kichwa chake unapaswa kuwa:

 • Wasichana 40.5 cm (inchi 15.9)
 • Wavualna 39.5 cm (inchi 15.6 )

Huenda ikawa miezi mitatu sio wakati mrefu, lakini mtoto wako mchanga anakua kwa kiasi cha kasi zaidi ya unavyo dhani. Kwa mfano, mtoto wa miezi mitatu anaweza songesha mikono yake kwa muingiliano pamoja na vidole na anacho kiona. Na pia misuli yake ina nguvu tosha kusitiri kichwa chake.

Katika kipindi hiki, mtoto wako anapaswa:

 • Kuwa ana pata nguvu za upande wa juu wa mwili wake, hasa kwenye misuli yake ya shingo na wakati wa tumbo (ama anapo lazwa kwa tumbo). Anapaswa kusitiri kichwa chake na kifua kwa kutumia mikono yake.
 • Kupata nguvu za mwili wa chini. Katika mwisho wa mwezi, anapaswa kuweza kunyoosha miguu yake na kurusha mateke kwa urahisi akiwa amelala kwa tumbo
 • Kupata nguvu ya kichwa. Unapo mshika, kichwa chake kiko wima
 • Utangamano unao imarika wa mikono na macho, kama vile kufungua na kufunga mikono yake na kuileta pamoja na kujaribu kufikia vidoli vya rangi zinazo ng'aa mbele yake
 • Kuleta mikono yake karibu na mdomo wake. Katika mwezi huu, anajaribu kuleta mikono yake kwenye mdomo wake. Hata anapo shika vidoli, anajaribu kuvitia mdomoni.
 • Kugeuka kwa mgongo. Baada ya wiki chache, mtoto wako anaweza anza kugeuka unapo mlaza kwa tumbo. Kwa hivyo kuwa makini na mahali unapo mlaza kwani anaweza geuka aanguke chini.

Uwezo wake utakaozidi kukua katika hatua hii ni kama vile:

 • Kugusa. Mtoto wako anapo fikisha miezi mitatu, ana pata fahamu zaidi kuhusu mambo yanayo mzingira. Atakuwa na hamu ya kugusu vitu tofauti vinavyo mzingira.
 • Sauti. Baada ya siku chache, mtoto wako ataanza kuitikia sauti yako, kugeuza kichwa chake na kutabasamu anapo kuona ama unapo muita.
 • Kuona. Mtazame mtoto wako. Nafasi kubwa ni kuwa ataendelea kukutazama machoni. Atajua uso wako, na harufu yako.

Vidokezo

 • Unapo mpa vidoli vya rangi zinazo ng'aa, mtoto wako atanyoosha mikono kujaribu kuzifikia na kuzileta mdomoni.
 • Mpe vitu tofauti awe ana guza ili ajifunze jinsi ya kutumia misuli na vidole vyake.
 • Jaribu kukusanya vitu vyenye harufu tofauti za kuvutia kama vile maua, viungo na vitu vingine. Kisha upitishe chini ya mapua yake kisha uangalie kuona harufu anayo ifurahia zaidi.

Wakati wa kumpeleka hospitalini

Ikiwa mwanao:

 • Hajaribu kufikia na kushika vitu
 • Hawezi egemeza kichwa chake vizuri
 • Hashiki vidoli unapo mpatia
 • Haleti vitu mdomoni
 • Ana shida ya kupeleka jicho moja ama yote mawili pande zote
 • Ana macho kengeza

Ukuaji wa akili

mtoto miezi mitatu

Katika mwezi wake wa tatu, mtoto wako anaanza kuelewa dunia inayo mzingira. Akili yake inayo kua inafanya kazi kuelewa kinacho tendeka.

Anaweza kufuata kwa makini vitu vilivyo na mwendo. Anapo ona kitu chenye mwendo mbele yake, atakuwa makini zaidi kukiangalia.

Mambo muhimu:

 • Jaribu kumfunza mtoto wako mapema. Chukua kidoli kisha uanze kumfunza kuhusu viungo tofauti vya mwili
 • Fanya wakati wa kumbadilisha nepi uwe muda wa kufurahisha kwa kucheza naye
 • Ongea na mtoto wako. Tumia maneno rahisi na sentensi fupi fupi. Hata kama bado hakuelewi

Wakati wa kumpeleka hospitalini

Ikiwa mtoto wako:

 • Hasikii sauti zenye kelele nyingi kama vile mlango kubishwa kwa nguvu
 • Hagundui mikono yake
 • Hafuati vitu kwa macho yake

Ukuaji wa hisia na muingiliano

Hata kama mtoto hajaanza kutangamana na wengine shuleni na kujua jinsi ya kuingiliana nao. Ana uwezo wa kuingiliana na familia na jamaa walio karibu.

Utangundua kuwa ana tabasamu kwa watu alio zoea kuona. Pia huenda akaanza kufurahia anapo ona watoto wengine karibu naye. Ana jaribu kuelewa hisia na mazungumzo na kuhusisha unacho sema na uso wako.

Mambo muhimu:

 • Mpe picha za wanafamilia na marafiki na umwonyeshe watu wanao cheka
 • Mwongeleshe kwa upole na ujaribu kurudia anacho fanya
 • Mwonyeshe anavyo kaa kwa kioo
 • Weka muziki ama ujaribu kumwimbia

Wakati wa kwenda hospitalini:

Ikiwa mtoto wako:

 • Hatabasamu anapo waona watu
 • Hatabasamu anapo sikia sauti ya mamake/babake
 • Hako makini kuona uso mpya na anaonekana kuogopa uso wa mgeni

Vyanzo: WebMd

Healthy WA, pathways

Soma Pia:Ukuaji Na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 7

Makala haya yalichapishwa tena na ruhusa ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio