Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

You won't believe what your baby can do at just six months old! She will be chattier, more active and even sleep all night.

Unaamini kuwa mwanao amefikisha nusu mwaka? Najua unacho fikiria - je, wakati umeenda wapi? Una mtoto wa miezi sita!

Miezi sita ni hatua kuu kwako na kwa mtoto wako mchanga. Kando na kuona mabadiliko mengi katika jinsi anavyo ingiliana nawe, daktari wako ataku shauri kumwanzishia mtoto wako chakula kiguma katika wakati huu.

Na mabadiliko haya makubwa, mwezi wa sita huwa wa kuingiliana na mwanao. Katika hatua hii, atakuwa makini zaidi kwa mazingara na kuchukua muunda kuelewa mwitikio wako kwa tabia yake. Azimia kicheko kingi anapo jitahidi kukufurahisha.

Mtoto wa miezi sita na hatua muhimu: Je, mwanao anakua ipasavyo?

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

Ukuaji wa Kifizikia

Utapenda kumwona mtoto wako wa miezi sita akianza safari yake ya kutembea katika mwezi huu ambapo watoto wengi huanza kujibingirisha kutoka kwa mgongo hadi wanapolala kwa tumbo.

Baadhi ya watoto wa miezi sita husoma kujibingirisha, iwapo wengine bado hutatizika hapo mwanzo na wanakasirishwa na jambo hili. Na kubingirika huku kote, utakuwa na amani kusikia kuwa watoto wengi hulala kutoka masaa sita hadi masaa nane wakati wa usiku katika umri huu.

Huu ni mwezi ambao unaazimia ataanza kutambaa.

Ila, usiwe na shaka iwapo mwanao atapita hatua hii ya asili ya kutambaa. Wengine hutumia sehemu zao za nyuma kutembea ama kuivuta miguu kwenye sakafu. Bora wanatoka sehemu moja hadi nyingine, na hakuna jambo la kukutia wasi wasi.

Katika umri huu, mtoto wako anapaswa kuweza kuvishika vitu na kuvileta mdomoni mwake, kukaa chini bila msaada wowote, anapo simama, anapenda kuruka ruka juu na chini, na kuinua mwili wake anapolazwa tumbo chini.

Katika umri huu, urefu na uzito wa mwanao* unapaswa kuwa ifuatvyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 67.6 cm (26.6 inchi)
  – Uzito: 7.9 kg (17.5 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 65.7 cm (25.9 inchi)
  – Uzito: 7.3 kg (16.1 lb)

Na kipenyo cha kichwa cha mwanao* kinapaswa kuwa:

 • Wavulana: 43.3 cm (17.1 inchi)
 • Wasichana: 42.2 cm (16.6 inchi)

Vidokezo

 • Wakati ambapo mtoto wako wa miezi sita anapo bingirika kwenye tumbo yake, ni wazi kuwa una furaha! Kuona furaha hii itamhimiza mwanao kuendelea kulifanya jambo hilo.
 • Kumpa vidoli anapokuwa amelala na tumbo kutamsaidia kuzoea mhemko huu mpya. Ina maan akuwa pia unapaswa kumtizama kwa makini wanapokuwa mahali juu. Unapo m-badili nepi, huenda ukataka kumwekelea mahali sakafuni pasipo na hatari ya kuanguka.
 • Kuhimiza wakati wa tumbo wakati wa mchana ni muhimu kwa ukuaji wa mikono, miguu, shingo na misuli ya mgongo kuwa na nguvu zaidi.
 • Vidoli ni muhimu katika ukuaji wa kuambatana kwa mikono na macho yake. Hata kukiweka kidoli cha mtoto wako mbali kidogo naye ili kumhimiza kukifikia.
 • Tazama iwapo ni salama mwanao kutembea. Ni muhimu kuhakikisha kuwa hakuna vifaa vinavyo weza kumhatarisha mtoto.

Wakati wa kuongea na daktari

Iwapo mwanao:

 • Hajibiringishi kwa upande wowote
 • Hana juhudi za kuvifikia vitu vilivyo mbali
 • Anaonekana kuwa na misuli iliyo shikana
 • Ana matatizo kuvipeleka vitu mdomoni mwake

 

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

Ukuaji wa Kiakili

Katika hatua hii, mwanao atakuwa amegundua mfumo maalum wa nyimbo ama nyimbo za watoto na kuanza kuazimia wakati utarudia.

Utagundua ongezeko la uwezo wa kuvifahamu vitu katika mtoto wako wa miezi sita. Wanapenda kugusa gusa vitu vilivyo laini ama vigumu. Vichukue vitabu ili muwe na wakati wa kujuana! Ataanza kuvipitisha vitu kutoka mkono mmoja hadi mwingine. Hii ni hatua kubwa!

Uwezo wa kuona utazidi kuimarika, na utaona kuwa mwanao anapendezwa na vitu vinavyo meta meta vyenye rangi nyingi na anapenda kuvinyakua.

Vidokezo

 • Wakati wa mchana, jaribu kumweka mahali palipo pasafi, penye mwangaza tosha. Mzingire na vidole vichache na umwache ajaribu kuvifikia.
 • Mpeleke matembezi na ukumbuke kuiweka rununu kwenye kijigari chake cha kutembelea kuhimiza uwezo zaidi.
 • Weka vitu vilivyo visafi karibu naye ambavyo ni salama kwake ili kumhimiza kuvipeleka karibu na mdomo wake. Pia hakikisha kuwa vitu hatari kama vile funguo na mashilingi vimewekwa mbali naye.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao

 • Haonyeshi athari za kusikia sauti za juu ama kujaribu kukufuata chumbani.

 

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

Ukuaji wa Muingiliano na Hisia

Mtoto wako wa miezi sita atakuwa na furaha zaidi kuingiliana na watu aliowazoea. Hasa mama na baba yake. Huenda akaonyesha hisia za woga watu wapya wanapo mkaribia.

Miongoni mwa mambo ambayo mwanao anayapenda zaidi ni kucheza usoni mwaka na kwa ujumla kujaribu kukufanya umwangalie. Kuwa tayari kuyashuhudia mengi, yote na kusudi la kupata mwitikio wako.

Vidokezo kwa wazazi
 • Huu ni wakati mwemwa wa michezo ya kumfuata kiongozi.
 • Mchezo wa kusisimua ni kuiga sauti ambazo mwanao mchanga anazitoa, kisha kuanzisha miigo ya sauti za wanyama aziige.
 • Unaweza utumia wakati huu kumsaidia kuikuza lugha yake kwa kumwonyesha picha za wanyama na kisha kusema jina la mnyama huyo na kuiiga sauti yake kwa pamoja.
Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Hana shughuli na mazingara yake ama haonyeshi ishara zozote kwa mtunzaji wake

Ukuaji wa mtoto na hatua muhimu: mtoto wako wa miezi sita

 

Ukuaji wa Mazungumzo na Lugha

Ichukue kamera! Mtoto wako wa miezi sita anapenda kuyarudia maneno anayo yasikia na huenda ukasikia "ma-ma" na "da-da" katika wakati mmoja. Watoto wengine huenda wakaiga sauti za wanyama kama vile "woof woof" ama "baa baa".

Anahisi kuwa anaongea vyema sana anapo yatamka maneno kwa sauti ya kitoto na kucheka. Hakikisha kuwa unamhimiza kwa kuitikia!

Vidokezo 
 • Unaweza kubaliana naye anapo ongea ama kuviashiria vyombo anavyo vitazama na uvitaje. Kutahimiza ukuaji wa uwezo wake wa lugha.
 • Njia nyingine ya kukuza uwezo wa lugha wa mwanao ni kupitia kuongea unapofanya jambo machoni mwake. Huenda ikaonekana jambo lisilo la maana unapo ongea kwa nguvu unapo fanya kazi za kinyumbani. Ila, maneno yote haya yanawekwa akilini mwake yatumike hapo mbeleni.
 • Ongea kwa njia ya kawaida, epuka kutumia lugha ya kitoto.
 • Tumia lugha ya kawaida badala ya kutumia maneno ya mtungo kwa vitu vya kawaida kama vile maziwa ama kidoli.

Wakati wa kuongea na daktari

Iwapo mwanao:

 • Anashindwa kutamka voweli kama 'aa', 'oh' 'eh'

 

mtoto wa miezi sita

Afya na Lishe

Katika hatua hii, mtoto wako wa miezi sita atakuwa tayari kuanza kula. Anza kwa kuchanganya vyakula vigumu na maziwa yako ya mama kisha uanze kumlisha matunda na mboga.

Katika umri huu, mtoto wako anapaswa kuwa na uzito kati ya kilo 7.1 hadi 8.8 na urefu wa kati ya 61 hadi 69.8 cm. Walakini, iwapo mtoto wako amekua akiwa mdogo lakini anaendelea vema, usiwe na shaka!

Mwezi huu, mtoto wako anapaswa kupata dosi la tatu la chanjo ya 6 ndani ya 1 na dosi la pili la PCV. Kuwa makini kuyakumbuka haya na uongee na mtaalum wa watoto anaye kuchunga kuhusu jambo hili.

Vidokezo

 • Mwanzishie vyakula vipya moja baada ya nyingine na siku kadhaa kati ya vyakula hivi ili kuangalia iwapo mtoto wako ana mzio kama vile upele, kuharisha ama kutapika.
 • Ila, usifikirie kuwa mwanao ana mzio asipo kipenda chakula fulani. Watoto huchagua! Kujaribu chakula kipya mara kadhaa kutasaidi kumzoesha ladha mpya.
 • Vyakula vyema vya kuanza ni kama vile parachichi, mandizi, papaya na viazi vitamu. Iwapo inahitajika, ongeza maziwa ya mama.
 • Iwapo unataka kuepuka vyakula vya kukamuliwa(purees), jaribu baby led weaning.
 • Kumbuka kuwa maziwa yatabakia kuwa chanzo cha kipekee cha virutubisho vya mwanao kwa miezi michache ijayo. Usitie shaka kuhusu kumlisha mwanao lishe tatu za vyakula vigumu kutoka mwanzo. Kijiko kimoja cha vyakula vigumu kimetosha.
 • Usi mwanzishie mwanao vyakula vigumu anapo hisi usingizi ama akiwa njaa. Wakati bora zaidi ni kati ya lishe ama baada ya kuamka.
 • Endelea kumnyonyesha na iwapo utagundua kuwa kinyesi cha mwanao kimekuwa kigumu sana baada ya kumpa vyakula vigumu, ni sawa kumwanzishia maji baada ya kumlisha. Tena, vijiko vichache vimetosha. Ama, mnyonyeshe baada ya kumlisha.
 • Shule ya Kibinafsi ya Wataalum wa Watoto huko Umerikani, imedhibitisha kuwa hakuna uhusiano kati ya kuwalisha watoto mayai ama samaki na mzio baada ya miezi sita. Ila vyakula fulani kama vile asali ama maziwa ya ng'ombe vinapaswa kuepukwa kwa miezi ifuatayo sita.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mwanao:

 • Anashuhudia kupoteza kwa kilo kwa ghafla
 • Hafuati asilimia ya hapo awali ya urefu na uzito
 • Anapata upele baada ya kula vyakula vipya

Vyanzo: WebMD

*Tahadhari: Hiki ni kipimo cha urefo na uzito na kipenyo cha kichwa kulingana na WHO.

Mwezi uliopita: Baby development and milestones: your 5 month old

Mwezi ujao:

Republished with permission from theAsianparent

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio