Mwezi wa tano ni wakati wa mpito kwa mtoto wako. Unaweza tarajia mtoto wako kujaribu kuongea vizuri kwa mara ya kwanza. Pia wanajitayarisha kuanza kutambaa inayomaanisha kuwa unafaa kuwa mwangalifu. Maendeleo ya mtoto wa miezi tano ni yepi?
Hatua Za Mtoto Katika Mwezi Wa Tano

Kudhibiti Misuli
Mtoto wa miezi mitano anaweza kukaa wima kwa muda mrefu. Mtoto wako bado atahitaji usaidizi wa mto lakini wana uwezo wa kukaa kwa muda bila usaidizi. Wengine wanaweza kubingilia kutoka kwa mgongo hadi kwa tumbo.
Mtoto wako anapobingilia utawaona wakichezea miguu yao. Wanajitayarisha kwa kutambaa kwa miezi inayokaribia. Lakini Kumbuka mtoto anapobingilia ni busara usimwache kwenye kitanda ama mahali anapoweza kuanguka.
Jambo lingine utagundua kuwa uwezo wa mtoto wako wa kushika vitu umeimarika. Wanaweza kuvuta vitu karibu, kuvichukua jua kwenye mikono yao na pia kubadilisha kutoka kwa mkono mmoja hadi mwingine.
Usingizi

Watoto wengi hulala usiku wote lakini sio wote. Himiza mtoto wako kuwa na mpangilio bora wa kulala( sleep rhythm). Anza kwa kumwosha na maji ya vuguvugu, ikifuatiliwa na kumsomea hadithi ili kuhimiza usingizi. Utagundua kuwa kwa uhakika ataanza kusinzia.
Kuwa na mazoea ya kumweka kwenye kitanda kama bado hajalala kabisa. Hii itamsaidia kujifunza kulala mwenyewe pasipo na usaidizi wako.
Wakati wa mchana mdogo wako bado anahitaji kulala mara mbili. Moja asubuhi na nyingine baada ya chakula cha mchana. Jaribu usicheleweshe usingizi mpaka wakati mtoto amekuwa mchovu ama anasinzia.
Hisia
Uwezo wa mtoto wako wa kuona unazidi kuimarika. Katika huu mwezi uwezo wao wa kuona bado haujatimilika lakini wanaweza kuona mbali zaidi na kuangalia kitu bila ya macho ya kupitana.
Uwezo wao wa kugundua rangi umeimarikia kiasi ya kwamba wanaweza kutambua tofauti kati ya rangi mbili zinazokaribiana. Lakini watoto katika huu umri hupendelea rangi za msingi kama vile nyekundu,majano na samawati.
Mawasiliano
Mtoto wako anafaa kuwa ana bwabwaja kwa sasa.Huku kubwabwaja kunaweza sikika kama maneno. Iwapo utaskia ma-ma ama ba-ba usifurahie bado. Kwani bado haya maneno haya maana kwao. Ni tu baada ya miezi michache wataweza kuyaelekeza haya maneno kwako.
Katika miezi mitano wanaanza kutambua sauti mbalimbali kama mbwa akibweka, ama gari linapoanza. Ata kama bado hawaelewi maneno wanaweza kugeuza kichwa wakiskia jina lao ama maneno kama vile hapana.
Vidokezo Kwa Mtoto Wako Wa Miezi Mitano
- Hupendelea muziki. Chezea mtoto wako aina zote za nyimbo kutoka kwa classical, jazz na pop. Watapiga makofi, cheka ama jaribu kuimba
- Mpatie mtoto wako vichezeo vyenye rangi. Pia unapowapatia kichezeo kipya mwambie jina lake ili kukuza msamiati wake.
- Ondoa vichezeo zinavyoning’inia kwenye kitanda chake. Mara mtoto anaweza kusongeza mikono na miguu anaweza kushikwa kwenye kamba za vichezeo
- Iwapo hujarekebisha au baby proof nyumba yako hakikisha umefanya hivyo. Funika nyaya zote za stima, weka vitu za kusafisha na vitu vingine ambazo ni hatari kwenye kabati zilizofungwa.
- Pia kuwa mwangalifu kutoacha chai ama maji moto na pasi kwenye meza ambapo mtoto anaweza kuvuta chini.
Furaha ya kila mzazi ni kuona kuwa mtoto wake anakua inavyopaswa. Iwapo mtoto wa miezi tano analemewa na hatua zingine ni bora kuzungumza na daktari wako.
Chanzo: Healthline
Soma Pia: Matatizo Ya Kiafya Mwanamke Anayo Kumbana Nayo Katika Mimba