Ukuaji na Hatu Muhimu Kwa Mtoto: Mtoto wako wa Miezi Tisa

Ukuaji na Hatu Muhimu Kwa Mtoto: Mtoto wako wa Miezi Tisa

Find out if your little one is on track with his or her development.

Hii ni robo ya tatu kutoka ulipo jifungua na ni miezi mitatu kutoka sasa hadi mtoto wako anapofikisha mwaka mmoja! Mtoto wako wa miezi tisa anayatamka maneno yenye maana zaidi kwa sasa, na anajishughulisha kwa shughuli zaidi.

Huu ni baadhi ya ukuaji unao azimia kwa mtoto wako wa miezi tisa:

 

mtoto wa miezi tisaUkuaji na Hatua Muhimu Katika Mtoto Wako Wa Miezi Tisa: Je, Mwanao Anakua Ipasavyo?

Ukuaji wa Kifizikia

Kusimama na kutembea kwa kujishikilia kwa kitu ni baadhi ya mambo ambayo mtoto wako huenda akaanza kufanya katika umri huu wa miezi tisa.

Mtoto wako wa miezi tisa huenda akaweza kukaa kwa muda mrefu na kujivuta hadi anaposimama imara. Kwa sababu mifupa na misuli yake imekua kwa zaidi, huenda akawa ni mtambaaji mashuhuri na huenda akaanza kutambaa kwa kutumia mkono mmoja na magoti yote mawili anapo shikilia kitu kwa mkono mwingine.

Uwezo wa kutembea wa mwanako umeimarika kwa sana katika wakati huu. Kwa sasa, huenda akawa mtaalum wa kutambaa - wakati mwingine, kutambaa hadi chini ya ngazi za nyumba, Huenda akawa na kasi ya kubadilika kutoka kukaa hadi kutambaa. Kuwa makini kwani mtoto wako huenda akaweza kusimama na kutembea kutoka pahala pamoja hadi pengine anapo jishikilia kwenye kiti. ( hakikisha kuwa nyumba yako inazingatia usalama wa mtoto!)

Uwezo wa kutembea umeimarika vyema katika mwezi wa tisa. Mtoto wako mchanga ataweza kuvichukua vifaa vidogo kama vile vidoli vidogo na kuambatanisha mwendo wake wa mikono.

Kama mtoto wako wa miezi tisa anahamu zaidi ya kutembea, mhimize kwa kumpa nafasi tosha ya kutembea. Na kwa kuwa mtoto wako anatembea, ongezeko la uzito wake litadhihirika kwa upole ikilinganishwa na miezi iliyo pita na hili ni kawaida.

Vidokezo kwa wazazi

ukuaji wa mtoto

 

Mpe mwanao wakati mwingi nje ya nyumba, na kuhakikisha kuwa wakati huu umetumika vyema ipasavyo. Haya ni baadhi ya mambo ya kufanya kuimarisha ukuaji wa kifizikia.

  • Cheza mchezo wa kukimbishana. Anapotambaa, unaweza mkimbiza ukitambaa pia, watoto wanalipenda jambo hili!
  • Usivitumie vikofia vya kujilinda (helmets) kwa mtoto wako kama huja shauriwa na daktari. Kutambaa kunasaidia kuongeza nguvu yake ya mikono na miguu.
Wakati wa kuwa na wasiwasi

Watoto wanapo anza kutambaa, baadhi ya magonjwa ya kukosa vitamini mwilini kama vile ukosefu wa vitamini D mwilini utaonekana kwenye mikono yake. Daktari atampima mwanao kuhakikisha hana ukosefu wowote mwilini. Ila, iwapo ungetaka kujadili zaidi na daktari wako, hasa kama mtoto wako amenyonyeshwa na hajapata virutubisho vifaavyo.

Ukuaji wa kiakili

Mtoto wako wa miezi tisa anatazama mambo kwa umakini na ana maswali mengi- kuelewa kwao kwa lugha hii pia kuna imarika. Mtoto wako pia anasikiza kwa umakini na anaielewa lugha ya ishara.

Huu ni wakati ambapo mtoto wako huenda akaanza kuelewa maana ya "apana" kupitia kwa matendo yako.

Mwezi huu wa tisa ni wakati ambapo mtoto wako ataanza kuyaiga matendo yako, kuiga sauti yako na kuwa mchekeshaji wa nyumba atakaye fanya jambo lolote kuwachekesha watu wazima walioko kwenye nyumba hiyo.

Vidokezo kwa wazazi

Huu ni umri ambao wanaanza kufurahia michezo ya kujificha. Haya ni baadhi ya mambo unatakayo yafanya

  • Ficha kitu mbele yake, kama vile kwa kutumia shuka, kisha umwache akitafute!
  • Watoto katika umri huu wanapenda kufuata vitu vinapo rushwa ama vinapo anguka. Kwa hivyo hili ni jambo moja litakalo hakikisha unacheka kwa sana.
Wakati wa kuwa na wasiwasi

Mtoto wako anapaswa kupitisha vitu kutoka mkono mmoja hadi mwingine. Iwapo mtoto wako hajihusishi katika michezo, unapaswa kumwona daktari.

Ukuaji wa Hisia na Muingiliano

Hii ni hatua ambapo uwoga kwa watu wageni linakua tatizo na pia uwoga wa kuwachwa. Mtoto wako kwa sasa anaelewa unapo karibia kuenda na anakuwa na wasiwasi mwingi wageni wanapokuwa karibu.

Mengi yanaendelea akilini mwake kwa sasa. Anatizama, na kuyaweka akilini na kuyaangazia ayaonayo. Ukuaji wa hisia ni mwingi katika umri huu, hata kama hauja dhihirika bado.

Vidokezo kwa wazazi

Iwapo unamchunga mtoto wako katika hatua hii, jaribu kuongea na yeye kuhusu kila kitu. Anavisikiza vyote. Iwapo anaenda kwa utunzi wa mchana, fuatilia ukuaji wake kwa kuongea na watunzaji wake.

Unaweza

  • Mtembeze aione dunia. Magari, mabasi, watu na vyote vilivyo muhimu kwa ukuaji wake wa muingiliano kuliko hapo awali.
  • Kuingiliana na wanyama wa nyumbani huenda kukakuza ukuaji wake wa hisia na muingiliano katika hatua hii. Matembezi kwa vyumba vya wanyama kunapaswa kuwa kwa mambo unayo kusudia kuyafanya.
Wakati wa kuwa na wasiwasi

Iwapo kuwa na uwoga kwa wageni hakujaanza kudhihirika bado, ama iwapo mtoto wako na shughuli na chochote kinacho endelea kwenye mazingara yake, unapaswa kumtembelea daktari.

Ukuaji wa Kuzungumza na Lugha

Katikati ya majina ya kitoto, mwanao huenda akasema maneno ya kweli na wakati mwingine hata kutunga sentensi.

Fahamu kuwa mtoto wako anafikiria anakwambia kitu unacho elewa, hakikisha kuwa unaitikia chochote akwambiacho.

Huenda kwa sasa, maneno ya kitoto ya mtoto wako yanasikika ya kweli sasa - maana kwamba huenda ukaanza kusikia "mama" ama "baba."

Wakati ambapo mtoto wako anaongea kwa sana, haimaanishi kuwa hatambui anacho kisema. Katika hatua hii, mtoto wako mchanga huenda akaanza kutambua mengi kuhusu sauti unayo itumia (ukali ama utulivu) kulinganishwa na maneno. Ina maana kwamba uendeleavyo kuongea na mtoto wako, atajua jinsi ya kuzungumza zaidi.

Kwa umakini lakini, kwani hii ina maana kwamba chochote usemacho, huenda akakirudia.

Mtoto wako wa miezi tisa ana uwezo wa kuelewa unacho mwambia vyema kwa kupitia matendo yako ikilinganishwa na maneno.

Hatua hii ni muhimu sana kwa kumsaidia mtoto wako kuelewa tofauti kati ya hisia na vitu vizuri na vibaya.

Kupitia kwa sauti ya maneno yako, mtoto wako ataweza kujua iwapo una furaha ama la. Kwa sasa huenda akaanza kuelewa jina "hapana," ila, huenda hatatii amri yako ama si wakati wote. Kulitumia jina hili kwa uchache kutamsaidia mtoto wako kulielewa vizuri. Kusema "hapana" na kufuatiliwa na kumtoa mahali aliko ama kutoa kifaa anacho kitumia ama kumnyonyesha unapo mwonyesha kitu kipya, kutamsaidia kuelewa unacho maanisha.

ukuaji wa mtoto

Afya na Lishe

Kwa wakati huu, mtoto wako anapaswa kuwa na uzito wa kilo 8 hadi 9.9 na urefu wa 65.7 hadi 74.2 cm.

Mtoto wako mchanga huanza kuchagua vyakula anavyo kula, kwa hivyo ni muhimu sana uanze kumlisha vyakula bora asikose virutubisho vyovyote mwilini. Ni vyema pia uanze kumpa vyakula vyenye ladha tofauti kwenye lishe yake.

Muundo wa mwanao wa kulala huenda pia ukabadilika wakati huu kwani anaanza kufurahikia wakati wa kucheza zaidi, huenda ikawa ni mchana ama usiku.

Vidokezo kwa wazazi

Panga lishe ya mtoto wako kulingana na HPB's sahani yangu ya afya. Mtoto katika umri huu anapaswa kunywa maziwa idadi ya 750 ml kwa siku. Anapaswa kuwa na kiasi cha wali ama 1/2 ya nafaka, matunda, mboga na nyama kuongeza kwa lishe yake.

Iwapo mtoto wako anapoteza asilimia za ukuaji wa urefu ama uzito, ni jambo la kutia wasiwasi. Iwapo hakuli vizuri, hakikisha umepata ushauri wa daktari kuhusu jambo hili.

Maono ya mwisho

Mtoto wako anavyo ongea, soma, cheza na vitu afanyavyo ni muhimu kukueleza kuhusu ukuaji wake.

Iwapo hizi ni hatua muhimu za ukuaji wa mtoto wa miezi tisa, ni vyema kukumbuka kuwa kila mtoto ni wa kipekee inapofika wakati wa hatua muhimu maishani. Mwongozo huu utakusaidia kujua vitu ambavyo mtoto wako atatimiza katika hatua hii.

Iwapo una maswali kuhusu ukuaji wa mtoto wako, ni vyema kupata ushauri kutoka kwa daktari maalum wa watoto kuhakikisha kuwa unashauriwa ipasavyo.

Source: WebMD

*Disclaimer: This is the median length and weight, and head circumference according to WHO standards.

Previous month: Baby development and milestones: your 8 month old

Next month: Baby development and milestones: your 10 month old

Republished with permission from theAsianparent

 

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio