Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Mwezi MMoja

Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Mwezi MMoja

The first year of a newborn's life is one of the fastest in human development; it’s no wonder that when you have a baby, you often hear people say ‘they grow so quickly!’ or ‘time goes so fast!’ The best thing you can do is enjoy and marvel at your baby's month-by-month development.

Najua bado unaendelea kufurahikia jambo la kuwa mama na mwanao mchanga anayekupendeza kwa sana! Wakati ambapo unadhani kuwa halifahamu lolote lile isipokuwa kuyanywa maziwa, kulala na kulia, anakua kwa kasi sana.

Tuna angazia hatua muhimu utakazo shuhudia katika maisha ya mtoto wako wa mwezi mmoja.

Hatua Muhimu Za Mtoto Wa Mwezi Mmoja: Mwanao Anajitayarisha Kukumbana na Dunia ki vipi?

 

mtoto mchanga

Ukuaji wa Kifizikia

Mtoto anapo zaliwa, tayari ana nguvu za kuvutia iwapo angali mbali katika safari yake ya ukuaji.

Mtoto mchanga asiye na matatizo yoyote ana nguvu za kupumua, anashika vitu kwa nguvu kutumia vidole vyake, na pia anaweza nusa mamake na amtambue. Cha kushangaza zaidi, baadhi ya watoto hunyonya vidole wangali katika tumboni mwa mama zao.

Ilhali mtoto anazaliwa na nguvu hizi zote za kupendeza, mwezi wa kwanza wa maisha yake huenda yakaonekana kana kwamba anakula chakula kingi, kulala, kulia, kukojoa na kunya.

Katika umri huu, watoto hawana nguvu nyingi za kudhibiti misuli yao na wana tegemea matendo ya kiasili kama vile kunyonya, kula miayo, na kulia.

Mtoto anapozidi kukua katika mwezi wake wa kwanza maishani, anaanza kusoma jinsi ya kuudhibiti mwili wake. Kuigundua mikono yake ni wakati mkubwa kwake. Ni furaha kwake zaidi anapojua kuwa anaweza itumia mikono yake kufinya vitu ama kuvinyonya vidole anapo hisi njaa.

Kutambaa, kutembea, kukimbia na kudensi vitaanza kutendeka mbio kuliko unavyofikiria. Ila njia ya kuviana vitu hivi vinaanza anapogundua sehemu tofauti za mwili wake.

Mtoto wako wa mwezi mmoja anapaswa kuanza kurusha mateke unapomlaza kwa mgongo wakati wowote sasa. Pia ataanza kuvuta vidole vyako na kufuata vitu kwa macho yake ama kukiinua kichwa chake unapo mlaza kwa tumbo.

Huenda ikaonekana kana kwamba sio mengi yanayo tendeka katika ukuaji wake ilhali nguvu zake tofauti zina imarika.

 • Uwezo wa kuona: Mtoto mchanga anaweza yafungua macho yake na kuona punde tu baada ya kuzaliwa. Ilhali macho yake hayana uwezo wa kuona vitu vilivyo mahali zaidi ya mita moja. Anaweza kukutazama vyema usoni ama mkononi. Usishangae anapo onekana kutazama pande mbili wakati mwingine. Hii ni kawaida kwa watoto wachanga.
 • Kusikia: Mtoto mchanga huanza kusikia baada ya wiki 28 za ujauzito. Kutoka ndani mwa tumbo lako, anazisikiza sauti za mwili wako na zilizo kwenye dunia ya nje. Utafiti unadhibitisha kuwa watoto wachanga huitikia mwito wa juu wa mwanamke ikilinganishwa na sauti ya chini ya mwanamme.
 • Kunusia:  Mapua ya mtoto mdogo hayana nguvu. Mtoto wako wa mwezi mmoja anaweza kutofautisha harufu yako na ya mtu mwingine.
 • Kuonja: Mwanao anakusanya maziwa ya mamake. Uwezo wake wa kuonja umekua (wana uwezo wa kuonja zaidi ya watu wazima) na anayapenda maziwa ile.
 • Mguso: Kila mtu anauhitaji mguso wa mtu kuhisi furaha. Masi ya mtoto ni njia bora ya kujuana na mwanao. Atagundua kuwa mikono yako inafariji na kumtuliza, kama vile mtu mkubwa pia. Masi za upole inamsaidia mtoto kukua hasa misuli yake.

Katika hatua hii, kimo cha mwanao cha urefu na uzito wake* unapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wavulana
  – Urefu: 54.8 cm (21.6 inchi)
  – Uzito: 4.4 kg (9.8 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 53.8 cm (21.2 inchi)
  – Uzito: 4.3kg (9.6lb)

Na kipenyo cha kichwa chake* kinapaswa kuwa:

 • Wavulana: 37.3 cm (14.7 inchi)
 • Wasichana: 36.6 cm (14.4 inchi)

Jambo lingine muhimu katika ukaji wa mtoto wako wa mwezi mmoja ni reflexes zake.

watoto wachanga huzaliwa na relexes kadhaa ambazo ni muhimu sana maishani mwao. Kama vile reflex ya rooting inayo mwezesha mtoto wako kulipata titi lako mashavu yake yanapo wekelewa karibu. Reflex ya kunyonya na kumeza inayo msaidia mwanao kunywa na kumzuia kuyanywa maziwa mengi zaidi.

Pia kuna reflex za kushika zinazo vutia. Zinamsaidia mwanao kushika vitu kwa nguvu kwa kutumia vidole vyake. Na pia reflex ya moro inayomsaidia kushtuka akisikia kelele nyingi.

Vidokezo:
 • Msaidie mwanao kukuza uwezo wake wa kujua mambo. Mhusishe katika kuongea na kuimba ili uwezo wake wa kusikia uimarike. Mkumbatie kila mara kuimarisha uwezo wake wa mguso. Mnyonyesha anapotaka kukuza uwezo wake wa kuonja na ahisi upendo.
 • Usinunue vijidoli vya rangi nyingi. Mwanao anapokuwa mchanga kiasi hiki, wanapenda kuangalia mimchoro, vidoli na simu zenye rangi za kupingana. Kama vile, nyeupe, nyeusi na nyekundu kuimarisha uwezo wake wa kuona.
 • Mpe mwanao masi ya upole kwenye mikono, miguu, na tumbo yake kuipa misuli yake nguvu. Masi ya upole kwenye tumbo lake ukifuata upande wa saa unasaidia mwanao kutoa hewa, na kuto starehe kokote.
 • Mwanao anapolazwa kwenye tumbo, bila kukawia, atasongesha kichwa chake ili aweze kupumua. Hata kiweka kichwa chake chini. Inajulikana kama reflex ya labyrinthine. Kwa hivyo wasaa wa tumbo ni muhimu sana. Dakika chache kama vile tatu ama mbili kwa siku zimetosha. Fanya hivi unapokuwa karibu na usimwache mwanao amelala kwa tumbo usipokuwa karibu.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwanao:

 • Hana starehe unapo mpindua shingo kutoka upande mmoja hadi mwingine.
 •  Haonyeshi hisia zozote kwa kelele nyingi.
 • Ana shida nyingi kuyatembeza macho yake na anabaki kutazama pande mbili.
 • Anaugumu kusongesha mwili wake.
UKuaji wa Kiakili

Ukuaji wa kiakili ni kuunda njia yake ya kufikiria, kukumbuka, kutatua mambo na kuamua. Mengi sana kwa mtoto wa mwezi mmoja? Si sana!

Kuanza tu, watoto hujua habari kuhusu dunia hii mpya na watu walioko ndani. Mwanao anakutazama kila mara, kusikia unachosema na kuyaangalia mazingara yake. Haya yote yana imarisha ukuaji wake wa akili.

Vidokezo:

 • Ukuaji wa kiakili kwenye watoto hulingana na mambo mengi ya utunzi wakati wa uja uzito na baada ya kujifungua kama vile afya ya mama wakati wa ujauzito.  Wakati mtoto alipo jifungua (kwa mfano, mtoto aliyezaliwa katika umri wa wiki 38, hufika hatua muhimu maishani polepole kuliko aliyezaliwa wiki 40). Matatizo wakati wa kujifungua, maradhi miaka ya kwanza ya maisha yake na mengineyo.
 • Katika umri huu, ni vigumu kupima ukuaji wake wa kiakili, ila kuna mambo mengi unayopaswa kufanya kuipa akili ya mwanao chanzo chema.
 • Mwonyeshe mtoto wako wa mwezi mmoja vitabu vya michoro vyenye rangi zinazopingana. Ata furahikia kuzitazama picha zile, kuisikia sauti yako itakayo imarisha akili yake.
 • Ongea na uimbe na mwanao mchanga mara kwa mara. Kuisikia sauti yako kunamtuliza na kumwashiria kuwa uko hapo.
 • Mpe vijidoli vinavyotoa sauti ndogo kuikuza akili yake na uwezo wake wa kusikia.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwanao:

 • Anapokea kichapo kichwani, hasa kwa sehemu iliyo laini fontanelle

Ukuaji wa Hisia Kuingiliana

Watoto wachanga hawalii kwa sababu wameboka, ila kwa sababu wana mahitaji (njaa, wana mkojo, wamechoka, wana baridi ama joto). Ni muhimu kutopuuza mwanao anapolia ama kumwacha ahangaike muda mrefu.

Kulia ni njia ambayo mwanao anatumia kuzungumza, anastahili msaada wako. Kumpuuza huenda kuka athiri ukuaji wa hisia zake. Mama na baba, unapaswa kujua kuwa anahisia kwako. Iwapo una furaha, atajua na unapokuwa na fikira nyingi ama umekasirika, atajua pia.

Vidokezo:

 • Zungumza na mtoto wako wa mwezi mmoja kwa njia ya upole. Itasaidia kumtuliza na kumpa faraja ya uwepo na upendo wako.
 • Usimwache mwanao alie kwa sana hadi ajitulize. Anastahili mguso wako ili atulie. Kutompa mguso huu huenda ukaharibu ukuaji wake wa mhemko na kuzidhibiti baadaye.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwano:

 • Hatulii unapom-beba, mwongelesha ama kumshika.

mtoto mchanga wa mwezi mmoja

Ukuaji wa Lugha na Kuongea

Jambo la kustaabisha katika ukuaji wa mwanao ni kuwa msingi wa kuongea na lugha huanza mtoto anapo anza kusikia. Huenda ikawa mapema anapokuwa bado yumo tumboni mwako.

Iwapo mtoto wako wa mwezi mmoja hata anza kuongea maneno machache kwa miezi michache baada ya kuzaliwa. Maneno ya mtoto yake huwa bila ya kuongea na hutendeka punde baada ya kuzaliwa kwake. Mtoto wako hulia na kuonyesha ishara za kulia ama hisia nyingi za furaha na kutaka kitu. Huenda akakuchekesha unapomwongelesha kwa utulivu.

Vidokezo

 • Hata ingawa mwanao hajaanza kuongea bado, mwongeleshe. Itamsaidia kwa sana. Baada ya miezi michache, huenda akaanza kuitikia ila msingi wake unaanza mapema.
 • Nyimbo ni njia murua ya mazungumzo na kujuana na mwanawe, kuimba ama kusikiza nyimbo za kipole.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwanao:

 • Haonyeshi ishara za kuiitikia sauti yako, huenda kuna haja ya kupima uwezo wake wa kusikia.

mwanao mchanga

Afya na Lishe

Katika umri huu, mtoto wako anachohitaji cha kukua ni maziwa ya mama – hakuna kingine. Maziwa yako ya mama ina virutubisho na vitamini zinazo saidia kumkuza kifizikia na kiakili. Pia maziwa haya yana viini vya kupigana na magonjwa na kumlinda kutoka na magonjwa. Kutapika kidogo baada ya kukula ni kawaida katika hatua hii.

Kutoka wakati ambao mwanao anazaliwa hadi anapofikisha wiki mbili, kupoteza uzito ni kawaida. Ila baada ya hapo, mwanao anapaswa kuanza kuongeza uzito. Katika umri wa mwezi mmoja, mwanao huenda akawa na uzito wa kilo kati ya 3.2 hadi 5.7 kg na urefu wa inchi 19 hadi 23.

Kwa sasa, kisiki cha kitovu chake kinapaswa kuwa kimekauka na kutoka. Kumwacha na tumbo ya kupendeza unayoweza kuibusu. Je, ulijua kuwa baadhi ya wazazi huvieka visiki vya watoto wao vilivyo kauka.

Wakati ambapo fontanelle (sehemu iliyo laini ya kichwa chake) bado iwazi, kuna hatari kubwa. Hakikisha kuwa utunzi unaofaa unazingatiwa anapo safishwa. Shingo yake bado haina nguvu za kutosha, kumbuka kuisitiri kwa kuuweka mkono wako chini ya shingo yake unapo msafisha.

Mama, huenda unahisi haujakuwa ukipata usingizi wa kutosha, kwani mtoto wako hana muundo maalum wa kulala. Usijali- mambo huendelea kuwa mazuri. Jaribu kulala mwanao anapolala angalau dakika 30.

Mwanao anapaswa kupewa dosi ya pili ya chanjo cha Hepatitis B mwezi huu. Ya kwanza anapewa anapozaliwa. Hakikisha kuwa umeongea na daktari wako kuihusu na chanjo zinazo fuata.

 Vidokezo:

 • Katika umri wa mwezi mmoja, uwezo wake wa kupigana na maradhi bado unakua. Si vyema kuwakubalisha watu kum-busu mwanao kwenye uso ama mikono. Iwapo wanam-beba, wahakikishe kuwa wamenawa mikono vyema.
 • Ni vyema kumnyonyesha mwanao anapo taka. Kumbuka kuhakikisha amemaliza maziwa katika kila titi kila unapomnyonyesha. Unaweza tumia bangili ya kunyonyesha kukumbusha titi ulilo malizia nalo kila mara.
 • Mwanao bado ni mchanga sana wa kutofautisha kati ya mchana na usiku. Ila unaweza iiga kwa kutumia chumba chenye mwangaza mchana na kuzima stima jioni anapolala. Itamsaidia kuelewa wakati wa kulala na wa kuamka.
 • Hakikisha analala vyema kuepuka Kifo Cha Ghafla Cha Watoto. Mgeuze mwanao na umlaze kwa mgongo anapolala, epuka kumlaza kwa tumbo. Kijitanda chake hakipaswi kuwa na mito, blanketi mzito ama vijidoli. Unaweza kudhibiti joto mwilini mwake kwa kumlaza na nguo zinazofaa.

Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo mwanao:

 • Anapoteza uzito kwa kasi
 • Anatabika baada ya kula kila mara
 • Ana fontanelle iliyo rudi ndani
 • Haja tulia
 • Ana jaundice
 • Ana joto jingi
 • Anatoa uchafu kutoka kwa sehemu zake za siri

Ni muhimu kukumbuka kuwa mwanao anapo kua, anabadilika sana, anahisia nyingi za kihemko na za kifizikia unazo zihisi pia.

Wamama wapya huenda wakahisi mkazo wa kukaa ama kuhisi njia fulani, na kutamani uzazi uje kwa kiasili. Kwa watu wengi, kubadilika kuwa mzazi na mabadiliko yanayo tokea mwilini, hisia na mengineyo, huchukua muda.

Iwapo una hisia za kukasirika ama unamatatizo kujuana na mwanao ama mwenzio, huenda ukawa na fikira nyingi baada ya kujifungua {post-natal depression (PND)}.

Wasiliana na daktari wako akushauri.

Mwishowe, kumbuka kuwa ukuaji wa watoto ni tofauti kwa kila mtoto. Kila mtoto ni tofauti na kuzifikia hatua muhimu kwa kasi ama polepole si kipimo cha atakavyo kua maishani.

mwanao wa mwezi mmoja

 

Source: WebMD

Previous: Baby development and milestones: your 3 week old
Also Read : Baby development and milestones: your 2 month old

*Disclaimer: This is the median length and weight, and head circumference according to WHO standards)

Republished with permission from theAsianparent

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio