Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto: Mtoto Wa Mwezi Mmoja

Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto: Mtoto Wa Mwezi Mmoja

Katika mwezi wa kwanza, mtoto mchanga ameanza kuzoea dunia hii kubwa iliyo na mengi. Na umeanza kuzoea kutunza mahitaji yao mengi.

Mwaka wa kwanza wa maisha ya mtoto wako ni kipindi cha kufurahisha na kusoma mengi. Katika kipindi cha miezi 12, mtoto wako atabadilika kutoka mtoto mchana kwa mtoto anaye anza kutembea, kuonea na kuonyesha ishara za kwanza za kujitegemea. Katika mwezi wa kwanza, mtoto mchanga ameanza kuzoea dunia hii kubwa iliyo na mengi. Na umeanza kuzoea kutunza mahitaji yao mengi. Hapa chini kuna mabadiliko machache unaweza tarajia kuona katika mtoto wako wa mwezi mmoja.

Ni muhimu kukumbuka kuwa watoto walio zaliwa kabla ya muda kutimia hawatafuata hatua hizi za ukuaji zilivyo. Huenda waka timiza kila hatua muhimu kulingana na tarehe badala ya siku ya kuzaliwa kwao. Watoto walio zaliwa mwezi mmoja kabla watachukua mwezi mmoja zaidi kufikia wanarika wao.

Ukuaji

mtoto wa mwezi mmoja

Usiwe na shaka ukigundua kuwa mtoto wako anapoteza baadhi ya uzito katika siku za kwanza chache za maisha yake. Watoto wanazaliwa na uowevu zaidi wa mwili na hupoteza hadi asilimia 10 ya uzito wa kuzaliwa kabla ya kusawazisha na kuanza kuongeza uzito. Wanapo fikisha wiki mbili, watoto wanapaswa kuwa wamerudia uzito wao wa kuzaliwa, na katika mwezi wa kwanza, wataongeza uzito mbio - kuongeza ounsi nusu hadi moja kwa siku. Daktari wako ataangalia uzito wa mtoto anao ongeza mtoto anapo rudishwa hospitalini, kuhakikisha kuwa wanakua ipasavyo.

Mwendo

Mfumo wa neva wa mtoto wako bado unakua, lakini watoto wanaweza timiza mengi katika mwezi wao wa kwanza. Utagundua kuwa mtoto wako alizaliwa na uwezo mwingi wa kibinafsi kama vile kunyonya. Punde tu baada ya kuzaliwa, wataweza kunyonya kutoka chuchu ya mama. Ukiweka kidole chako ndani ya kiganja cha mtoto wako, utagundua kuwa watajaribu kukumbatia.

Kulala

Maendeleo Na Ukuaji Wa Mtoto: Mtoto Wa Mwezi Mmoja

Kuzaliwa ni kazi nyingi. Kwa wiki za kwanza chache, itaonekana kuwa yote ambayo mtoto wako atafanya ni kulala. Watoto wachanga hulala kati ya masaa 15 hadi 16 kwa siku. Hajazoea tofauti kati ya mchana na usiku. Unaweza msaidia mtoto wako azoe kwa kupunguza shughuli hadi mchana na kuhakikisha kumetulia usiku. Hatimaye, wata fahamu kuwa mchana ni wa mchezo na usiku kulala.

Uwezo tofauti

Watoto huzaliwa na uwezo wa kuona usio dhahiri. Na wanaona vitu vilivyo karibu. Mtoto anaweza ona watu na vitu vilivyo inchi 8 ama 12 mbali naye. Huku kuna maana kuwa wanaweza ona uso wako unapo wanyonyesha.

Hata kama uwezo wao wa kusikia hauja komaa, watoto wanaweza gundua sauti hasa za wazazi wao, walizo zoea kusikia wakiwa tumboni. Ikiwa mtoto haitikii anapo ongeleshwa hata kwa sauti, hakikisha kumjuza daktari wa watoto.

Kula

Katika mwezi wa kwanza, tarajia mtoto uliye mnyonyesha kula mara 8 hadi 12 kwa siku(baada ya angalau kila masaa mawili ama matatu). Watoto wanao lishwa kupitia kwa chupa wanaweza kula mara sita ama nane kwa siku. Baadhi ya wazazi huwalisha watoto wanapo itisha, wakati ambapo wengine hufuata ratiba. Utajua wakati ambapo mtoto wako ana njaa (ataanza kupeleka kichwa chake nyuma na mbele akitafuta chuchu ya mama) ama kukosa kuwa mtulivu. Mtoto aliye kula vya kutosha huenda akaanza kulala.

Mazungumzo

Mtoto wa mwezi mmoja ana njia moja ya kuzungumza--kulia. Anaweza lia hadi kwa masaa matatu kwa siku(usiwe na shaka, kutapunguka anavyo zidi kukua). Kulia ni njia ya mtoto kusema kuwa ana njaa. Baadhi ya watoto ambao hulia sana huenda wakawa na colic ama tatizo la kiafya. Kwa hivyo unaweza wasiliana na daktari wako.

Vidokezo muhimu vya mtoto wa mwezi mmoja

  • Hakikisha unampa masi. Wanapenda kushikwa sana. Atahisi anapendwa na salama
  • Peleka miguu yake kana kwamba anaendesha baisikeli mara kwa mara. Hili ni zoezi rahisi la kusaidia misuli yake kuwa tayari kutembea.

Soma PiaUkuwaji na Hatua Muhimu Maishani Mwa Mtoto Wako wa Miezi Miwili

Written by

Risper Nyakio