Je, Ni Wakati Upi Ulio Bora Kufanya Kipimo Cha Mimba?

Je, Ni Wakati Upi Ulio Bora Kufanya Kipimo Cha Mimba?

Muda wa kupima mimba ulio bora kupata matokeo dhabiti ni upi? Mwanamke ana shauriwa kufanya kipimo cha mimba wiki mbili baada ya kukosa kipindi cha hedhi.

Mama anaye tamani kupata mtoto huwa na shaka kuhusu muda wa kupima mimba. Wakati bora wa kufanya kipimo cha mimba utakao onyesha matokeo dhabiti ni upi? Tuna angazia zaidi kuhusu vipimo vya mimba.

Nitapata wapi kipimo cha mimba?

Vipimo vya mimba vinapatikana kwenye maduka ya madawa ama kwenye hospitali. Ikiwa unashuku kuwa una mimba, unaweza nunua kipimo hiki bila kuidhinishwa na daktari. Huku utumiaji wa teknolojia ukizidi kunoga, unaweza kupata vipimo hivi mtandaoni na kuletewa kwako nyumbani baada ya kununua.

Muda wa kupima mimba ulio bora ni upi?

muda wa kupima mimba

Je, mama anapaswa pima mimba baada ya muda upi? Kupima mimba mapema sana huenda kukaleta matokeo yasiyo halisi. Huenda mwanamke akawa na shaka kuhusu hali yake na kumfanya akose subira tosha.

Mimba hutokea baada ya yai na manii ya mwanamme kupatana. Yai linapo rutubishwa na manii, lina jipandikiza kwenye kuta ya uterasi. Seli mpya hugawanyika na kutengeneza kiinitete. Placenta ya mtoto hutoa homoni ya hCG mwilini ambayo inatumika kudhibitisha iwapo mwanamke ana mimba ama la.

Mwanamke anapaswa kufanya kipimo cha mimba wiki mbili baada ya kukosa kipindi chake cha hedhi. Kwani katika kipindi hicho, hCG mwilini imeongezeka na matokeo ya kipimo huwa dhabiti.

Mzunguko wa kipindi chako cha hedhi utaku dhibiti kufahamu muda bora wa kuchukua kipimo hiki. Unapo fanya kipimo kabla ya kukosa kipindi chako cha hedhi, huenda ikawa kuwa viwango vya homoni ya hCG bado ni vidogo. Na wakati huo mwanamke hatapata matokeo dhabiti.

Wakati bora wa kufanya kipimo cha mimba

muda wa kupima mimba

Mwanamke anaye taka kujua hali yake ya mimba huenda akawa na shaka kuhusu wakati bora wa kufanya kipimo. Ni vyema kuwa makini na wakati wa kufanya kipimo hiki kwani kunaweza kuathiri matokeo ya mimba. Kwa kutumia vipimo vya mimba vya dukani, binti anashauri kupimo mapema anapo amka. Kwa kutumia mkojo wa kwanza wa siku kabla ya kuchukua kiamsha kinywa. Mkojo wa asubuhi huwa na viwango vikubwa vya homoni ya hCG inayo dhibitisha kuwepo kwa mimba.

Unapokunywa maji, viwango vya homoni hii hupungua. Na kuongeza nafasi za kupata matokeo hasi.

Nitakitumia kipimo cha mimba?

Kutumia kipimo cha mimba ni rahisi sana. Maelezo yote yame dokezwa kwenye kijikaratasi cha nje.

Kipimo cha nyumbani kina matokeo dhabiti?

Kipimo cha nyumbani kimedhibitishwa kuwa na matokeo dhabiti muda wa kupima mimba unaofaa unapo timia. Ikiwa una shaka kuhusu matokeo uliyo yapata, enda kwa kituo cha afya karibu nawe ili ufanyiwe kipimo cha damu.

Soma PiaFibroids Zina Athiri Uwezo Wako Wa Kupata Mimba?

Written by

Risper Nyakio