Kendrick Oyando, mwigizaji maarufu anayefahamika kwa jina lake la utani Mulamwah. Alienda kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii kusema kuwa Keilah Oyando sio mtoto wake. Mulamwah na Carol Sonnie wamekuwa katika uhusiano kwa muda mrefu, ila katika miezi michache iliyopita, uhusiano wao umekuwa na tashwishi.
Mulamwah na Carol Sonnie
Picha: Mulamwah Instagram
Mwaka uliopita, wawili hawa walitengana kwa muda kisha wakarudiana na miezi michache baadaye, kuwajulisha wafuasi wao kuwa wanatarajia mtoto. Carol Sonnie alipojifungua, mchumba wake alikuwa na furaha nyingi, na akaonekana akimpongeza na pesa taslimu laki moja. Kila mwanadada alimwonea wivu na kuwapongeza kwa kujifungua mtoto wa kike.
Mnamo Aprili tarehe 8, Mulamwah kupitia kwa mitandao yake ya kijamii ya Instagram na Facebook, aliwajuza watu kuwa Keilah Oyando, tuliyemdhania kuwa binti yake na Carol Sonnie kuwa sio mtoto wake. Kwani Carol Sonnie alikuwa mwenzi nje ya uhusiano wao. “Keilah sio Mwanangu,” aliandika.
Utata katika uhusiano wao
Picha: Mulamwah Instagram
Siku chache kabla ya kufanya kauli hii, alisema kuwa mzazi mwenziye alikuwa na mwenzi wa kando, kwa zaidi ya mwaka mmoja walipokuwa wangali pamoja. Kulingana na Mulamwah, alipokuwa akisombwa na mawazo wakati wa janga la Corona, mzazi mwenza wake alikuwa nyumbani mwa mwanamme mwingine. Carol Sonnie hajapeana kauli yake kudhibitisha iwapo kilichosemwa kumhusu ni kweli ama la.
Mulamwah alizidi kusema kuwa, alijua kuwa Carol alikuwa na mpenzi mwingine kwa muda ila hakutaka vita vyovyote, na akaamua kunyamaza. Katika mojawapo ya machapisho yake, alisema kuwa jirani mmoja alimtumia picha za mzazi mwenza wake na mchumba wake. Na kuwa alikuwa na picha hizo kwa muda mrefu. Aliendelea kuweka nambari ya mwanamme huyo mwingine.
Wafuasi wake hawakulichukulia jambo hili vizuri. Wengi walimkashifu kwa alichofanya. Huku wengine wakitaka kujua marafiki zake ni kina nani na kuwa wangependa akae mbali na mitandao ya kijamii hadi apone na akubali kilichofanyika.
Soma Pia: Kisiwa Cha Zanzibar Kuzungumziwa Kwenye Mitandao Baada Ya Msafiri Wa Kipekee Wa Kike Kukisi Kuwa Alidhulumiwa Kingono Katika Mojawapo Ya Hoteli Huko