Katika ndoa, kutakuwa na wakati ambapo lazima mzungumze kuhusu mambo magumu. Lakini mnapo zungumzia mada ngumu, unapaswa kuwa makini usiumize hisia za mchumba wako. Na kama mume hakutoshelezi kitandani, unapaswa kumweleza kwa njia inayomjali zaidi.
Wanaume huweka fahari nyingi katika nguvu zao za kiume. Na mara nyingi wanafikiria kuwa wanao ni simba kitandani wakati ambapo, ukweli ni kuwa, wao ni paka tu.
Lakini unaweza kuwasaidia, kwa kuwapatia mapendekezo ya jinsi ya kuboresha mbinu zao bila kuumiza hisia zao.
Ikiwa Mume Wako Hakutoshelezi Kitandani, Hapa Kuna Njia 5 Za Kumweleza

- Kwa njia ya kawaida na chanya
Ibua mambo ya kitandani mnapozungumzia mambo ya kawaida, mnapotazama runinga ama mnapokula. Kwa njia hii, haionekani kama jambo kubwa. Angazia mambo chanya na mambo yaliyo kufurahisha katika kipindi chenu cha mwisho. Kufanya hivi kunasisitiza unachopenda kitandani. Baada ya muda, ataelewa.
Kulingana na mtaalum wa ndoa, matatizo ya chumbani yanapaswa kuzungumziwa nje ya chumba hicho. Na kuwahimiza wanawake kusema kinachowafurahisha kitandani.
2. Himiza mema
Hata chumbani, unaweza kumhimiza mchumba wako kufanya vyema zaidi bila kusema kwa njia ya moja kwa moja. Kivipi? Angazia anachofanya vizuri mara kwa mara. Kwa mfano, ikiwa hupendi anapofanya mtindo fulani, anzisha mtindo tofauti.
Kumbuka kuwa, kama mnataka kupendezana, hakuna njia inayofaa ama isiyofaa ya kufanya ngono. Lakini kuna njia bora inayowafurahisha nyote.
"Ni rahisi sana kwa wanaume kuhisi kama wanafanya kitu vibaya, lakini hakuna njia sawa ama mbaya." Elewa mwili wa mke wako kwani miili ya wanawake huwa tofauti sana.

3. Muonyeshe wala usimhakiki
Kwa njia sawa, mtaalum wa masuala ya ngono na ndoa anapendekeza kutohakiki mchumba wako mnapokuwa kitandani. Ni kweli kwani hakuna anayetaka kuambiwa anachokosea kitandani wanapokuwa wakifanya kitendo cha mapenzi.
Badala yake, mwonyeshe unachokipendelea unapokuwa kitandani. Ikiwa anapuuza mtindo unaoufurahia, mweleze mtindo unaokupendeza.
Kumbuka kuwa mume wako anataka kukufurahisha kitandani na hata walio wazuri zaidi katika kitendo hiki wanahitaji kuelekezwa kidogo.
4. Usimzidishie
Unapomwelekeza na kuzungumza kuhusu unachokipendelea, usimzidishie maagizo. Huenda akahisi ni mengi kwa pamoja. Mweleze kitu kimoja ama mawili kwanza. Ikiwa mwanamme anatatizika na kutojiamini, uwezo wake wa kiume utaathiriwa.
5. Sikiliza maoni yake
Kumbuka kuwa kitendo cha ngono kinafanywa na watu wawili. Ikiwa mume wako ana uwezo dhaifu kitandani, unaweza msaidia kwa kumwuliza anachokipenda. Huenda ikawa mtindo wake unaweza imarika mnapofanya mitindo inayomfurahisha.
Mawasiliano ni muhimu. Kuzungumza kunawasaidia kujua vitu ambavyo mchumba wako anapendelea.
Chanzo: SELF, Bustle
Soma Pia: Kufanya Mapenzi Katika Mimba Ni Salama Kwa Mtoto? Maswali Kuhusu Ngono Katika Mimba