Huenda Uke Wako Ukachomeka- Wataalam Waonya Dhidi Ya Mvuke Wa Uke

Huenda Uke Wako Ukachomeka- Wataalam Waonya Dhidi Ya Mvuke Wa Uke

Uke wako huenda ukachomeka-mtaalam wa matibabu ya wanawake ali onya dhidi ya mvuke wa uke. Baada ya mwanamke kutoka Canada kuchomeka akijaribu jambo hili.

Mvuke wa uke (v-steaming) ni mbadala ya matibabu ya ki afya yanayo fanyika katika sehemu tofauti za Africa, Asia na America ya kati. Mama huchuchuma ama kukaa juu ya maji yaliyo chemka na yaliyo na mimea kama vile mugwort, rosemary,wormwood na basil.

Imejulikana kwa sana miongoni mwa spas, na watu mashuhuri. Ina aminika kuwa njia ya kuufanya uke uwe na nguvu zaidi, kukaza kuta zake na pia kupunguza uchungu wa hedhi. Pia husaidia katika uzazi.

 

View this post on Instagram

 

face mask / heat pad / vagina steam no I don’t know if any of this works but it can’t hurt right? *vagina dissolves*

A post shared by chrissy teigen (@chrissyteigen) on

Walakini, jarida la Canadian Obstretics and Gynaecology, lilipeana kesi ya mwanamke mwenye umri wa miaka 62 aliye pata matatizo ya uke ya kuenea. Hali ambapo misuli inayo shikilia viungo vya pelvic inakosa nguvu huku kusababisha kibofu cha mkojo, urethra ama rectum kuanguka kwenye uke.

Mgonjwa yule alikuwa amechagua mvuke wa uke, na imani kuwa matibabu haya yatamsaidia kuepukana na upasuaji. Ila, hatimaye ulimfanya apate majeraha ya kuchomeka.

Vanessa Mackay, mshauri  wa Chuo Kikuu cha Royal cha Obstetricians and Gynaecologists, walipingana na matamshi kuwa uke unahitaji kuoshwa kw asana.

Mackay alishauri utumiaji wa sabuni za kunukia katika sehemu ya genitalia nje ya uke peke yake. Alitoa onyo kuwa kuchoma uke huenda kukawa na hatari. Kwani hakuna ushahidi kuwa yana manufaa ya kiafya, watu wengi wanavyo sema.

“uke una bakteria zinazo ilinda. Kuuchoma uke huenda kukaleta majeraha kwa ngozi laini inayo ufunika uke,” alisema katika matamshi yake.

Huenda pia ika athiri usawa wa kiafya wa bakteria na idadi ya pH.  Na kusababisha kusumbuka,magonjwa (kama vile bacterial vaginosis ama thrush) na mwako.

Magali Robert, mwandishi wa ripoti alisema kuwa mwanamke aliye jeruhiwa, aliuvuka uke wake kufuatia ushauri wa mojawapo wa madaktari wa Uchina wa kiasili. Kwa kuyakalia maji yaliyo kuwa yakichemka kwa muda wa dakika ishirini (20), siku mbili mfululizo.

Watunzi wa kiafya wanapaswa kufahamu mbinu zingine ili waweze kuwasaidia wanawake katika uamuzi na kuepukana na hatari,” alisema alipokuwa akipingana na mbinu hii.

Read Also:  Vaginal Tightening Using ACV: Would You Try It?

This article first appeared in The Cable and was written by STEPHEN CHARLES KENECHUKWU. Republished with permission.

 

Written by

Risper Nyakio