Kwa Nini Ni Vigumu Kwa Wanaume Kusamehe Mwanamke Anapo Toka Nje

Kwa Nini Ni Vigumu Kwa Wanaume Kusamehe Mwanamke Anapo Toka Nje

Kwa mwanamme, mwanamke kutoka nje kuna tia alama ya swali katika nguvu zake za kiume na utendaji kazi wake kitandani.

Kwa nini ni vigumu kwa wanaume kusamehe mwanamke anapo toka nje? Mojawapo ya sababu ni kuwa, ni nadra kwa wanaume kuwa wame jitayarisha kudanganywa.

Wanaume wana julikana kuto samehea wanapo gundua kuwa wanawake wao wametoka nje. Na hii ni kejeli kwani wanaume ndiyo wanao aminika kutoka nje zaidi kati ya jinsia hizi mbili.

Kwa njia fulani, wanawake wana onekana kuwa

Kwa Nini Ni Vigumu Kwa Wanaume Kusamehe Mwanamke Anapo Toka Nje

Inapaswa kusemwa kuwa wanawake hutoka nje pia. Na kuna onekana kuwa na ongezeko katika nambari ya wanawake wanao toka nje siku hizi. Lakini jambo kuu linalo tofautisha wake kwa waume wanao toka nje ni kuwa wanawake wana uwezo zaidi wa kuficha matendo yao. Wanawake wana sifika kwa kuficha walicho kifanya.

Kauli iliyoko mitaani ni kuwa, mwanamke anapo amua kutoka nje, hautawahi jua.

Haijalishi ikiwa wewe ni mwanamke ama mwanamme, ikiwa uko makini ama haujali unapo toka nje ya ndoa ama uhusiano wako, jambo hili huwa na hatari ya kupatikana. Hatari inapunguzwa tu, hai ishi.

  • Kwa hivyo, kwa nini wanaume hawa samehei wanawake wanapo toka nje?Wanaume wengi huona hili kama jambo la kudhalilishwa na kuonekana kama wanyonge. Haijalishi ikiwa tabia zao zilimsukuma mwanamke kutafuta mtu mwingine ama ilikuwa dakika ya unyonge.
  • Kwa mwanamme, mwanamke kutoka nje kuna tia alama ya swali katika nguvu zake za kiume na utendaji kazi wake kitandani. Na kuathiri kitambulisho chake kama mwanamme.
  • Wanaume huwa na hisia hasi mwanamke anapo toka nje kwa sababu sehemu ya kufanya mapenzi ni muhimu sana. Kufikiria jinsi mwanamme mwingine anavyo mfanyie bibi yake mapenzi kwa mtindo wa ngono anao upenda zaidi humfanya ahisi hasira zaidi.
  • Sababu nyingine kwa nini hawasamehei jambo hili ni kuwa hakuna wakati mmoja ambapo mwanamme anakuwaga tayari kudanganywa na mwanamke anaye mpenda. Na hupigwa na butwaa anapo gundua kuwa mpenzi ama bibi yake ana mpango wa kando.

Hii ni tofauti na wanawake wengi wanao amini kuwa kuna uwezekano wa bwana ama mpenzi wake wa kiume kuwa na mpango wa kando. Kwa hivyo, wachache sana hushtuka wanapo gundua. Kwao, kugundua ni kudhihirisha hofu waliyo kuwa nayo.

Soma Pia:Umuhimu Wa Vidoli Vya Ngono Vya Wanandoa Na Umuhimu Wake Katika Ndoa

Written by

Risper Nyakio