Mwongozo Wa Sindano Unazo Hitaji Ukiwa Na Mimba

Mwongozo Wa Sindano Unazo Hitaji Ukiwa Na Mimba

Chanjo zinazo husishwa na ujauzito ni kama kutengeneza kitu kipya. Hii ndiyo sababu kwa nini chati ya sindano za ujauzito ni muhimu.

Ujauzito huambatana na utaratibu mwingi na chanjo ni muhimu katika kipindi hiki. Chanjo zinazo husishwa na ujauzito ni kama kutengeneza kitu kipya na hakuna kinacho paswa kuachiliwa. Hii ndiyo sababu kwa nini chati ya sindano za ujauzito ni muhimu. Ina ongoza wanawake wajawazito kufahamu sindano yanazo paswa kupata na wasizo hitaji. Na wakati wanao paswa kupata sindano hizi. Na bado wanawake wengi hukosa kufahamu wanapo chelewa ama kukosa kupata sindano hizi. Na kuwatia katika hatari ya kuugua magonjwa pamoja na watoto wao.

Chanjo ni nini?

Chanjo ni dawa yoyote inayo saidia kulinda mwili dhidi ya magonjwa fulani. Kwa wanawake wenye mimba, chanjo ni muhimu sana kwa sababu zina saidia kulinda mama na mtoto kutokana na magonjwa. Lakini ni vyema kuwa siliana na daktari wako kwani sio chanjo zote ni salama unapokuwa mjamzito.

Je, chati ya sindano za ujauzito ni nini?

Mwongozo Wa Sindano Unazo Hitaji Ukiwa Na Mimba

Huu ni mwongozo unao onekana. Una onyesha chanjo ambazo mwanamke mjamzito anapaswa kuchukua kabla na baada ya ujauzito.

Chanjo unazo weza kuchukua kabla ya mimba

Ni muhimu kufanya vipimo kudhibitisha ikiwa uko salama kupata mimba. Katika kipimo hiki, daktari ana angalia kuhakikisha kuwa uko sawa kutunga mimba. Pia ni vyema kwenda na historia yako ya chanjo unapo enda kufanyiwa kipimo hiki. Lakini kama hauna habari, daktari wako anaweza fanya kipimo cha damu kujua chanjo unazo hitaji. Daktari wako huenda aka shauri upate chanjo zifuatazo.

  • Influenza

Pia ina fahamika kama homa ama flu. Mara nyingi huenda ika sababisha koo kuuma, kuumwa na mwili, kutapika na kuendesha kwa watu wa kawaida. Lakini kwa mwanamke mwenye mimba, hatari za kupata influenza ni nyingi zaidi. Huenda aka shuhudia uchungu wa mama usio komaa. Na matatizo mengi ya afya huenda yaka fuata mtoto aliye zaliwa kabla ya wakati.

  • HPV (Human Papillomavirus)

HPV ni ugonjwa ambao unaoweza kupata kutokana na kufanya ngono bila kuji kinga ama maambukizi ya kingono. Na unaweza pata chanjo muda tu kabla ya kupata mimba. Kwani HPV huenda ika sababisha saratani ya cervical ama genital warts.

  • Measles, mumps na rubella

Katika nchi nyingi, watu hupata chanjo hii wakiwa wadogo. Lakini unapoendelea kukua, huenda ukahitaji chanjo nyingine kusaidia ya kwanza. Ugonjwa wa surua husababisha upele unao sambaa kwa kasi. Lakini kwa wanawake walio na mimba, huenda ukasababisha kupoteza mimba. Na rubella inaweza sababisha mtoto kufa kabla ya kuzaliwa ama kujifungua kabla ya wakati kufika.

  • Chickenpox

Sio salama kupata chanjo hii ukiwa na mimba. Ikiwa unaihitaji, inapaswa kuwa kabla. Ugonjwa huu husababisha matatizo ya ngozi kama vile kujikuna ngozi na upele. Lakini kwa wanawake wenye mimba, huenda ikasababisha matatizo ya kujifungua. Na kuathiri viungo fulani vya mtoto.

Chanjo zaidi

sindano za ujauzito, mimba

Chanjo zingine ambazo unaweza pata kabla ya kutunga mimba ni kama vile pneumonia, meningitis, hepatitis A na B, influenza B na tetanus.

Ni chanjo zipi ambazo unaweza chukua ukiwa na mimba? Sindano za ujauzito

Unaweza patiwa chanjo zifuatazo ukiwa na mimba.

  • Chanjo ya Tdap

Jaribu kuchukua chanjo hii katika kila ujauzito. Ina linda mtoto wako kutokana na pertussis katika miezi ya kwanza michache ya kuzaliwa kabla ya kupatiwa chanjo.

  • Polio

Polio inaweza sababisha ulemavu utakao dumu. Ugonjwa huu una hatarisha mfumo wa neva wa kati na ku athiri uti wa mgongo.

  • Rabies

Huu ni ugonjwa una ua usipo tibiwa bila kukawia. Unaweza pata rabies kutoka kwa mnyama aliye na ugonjwa huu. Mara nyingi hupitishwa kupitia kuumwa. Kama vile unapo umwa na mbwa aliye na ugonjwa huu.

  • Smallpox

Ugonjwa huu una sababishwa na virusi na unaweza sambaa kwa urahisi kutoka kwa mtu mmoja hadi kwa mwingine. Na matokeo ni upele ambao unaweza sababisha kifo.

  • Yellow fever

Mbu walio ambukizwa ndiyo wanao beba virusi hivi hatari. Ishara ni viungo vya mwili kukosa kufanya kazi, kutoa damu na joto jingi mwilini. Ni maradhi hatari.

  • Chanjo ya homa ya matumbo (Typhoid fever)

Ni ugonjwa maarufu duniani kote. Una pitishwa kwa chakula na maji na ugonjwa huu unajulikana kwa ishara ya joto jingi zaidi. Kwa kesi sugu, una weza sababisha kuvunja damu ndani ya mwili wako.

Unapo mtembelea daktari wako kwa kipimo kabla ya kutunga mimba, ongea na daktari wako kuhusu mizio yoyote ambayo huenda ikaku athiri kabla ya kuchukua chanjo.

Soma Pia:Ratiba Ya Chanjo Kenya : Mwongozo Kwa Wazazi

 

Written by

Risper Nyakio