Jinsi Ya Kufanya Tendo La Ndoa: Mwongozo Kwa Anaye Anza

Jinsi Ya Kufanya Tendo La Ndoa: Mwongozo Kwa Anaye Anza

Kusoma mwongozo wa kufanya mapenzi ya kuvutia ni muhimu hasa kwa mara yako ya kwanza ili ufurahie kitendo chako cha kwanza. 

Kwa sasa huenda ukawa unafanya utafiti kuhusu jinsi ya kufanya ngono ya kupendeza kwa sababu uko tayari kuipata. Kama mtu anaye anza, wazo la kulifanya kwa mara ya kwanza huenda likakuzidia. Lakini usiwe na shaka, unaweza furahia ngono yako ya mara ya kwanza ukijitayarisha ipasavyo na mambo unayo hitaji kujua kabla ya kufanya ngono. Tazama mwongozo wa kufanya mapenzi.

Mwongozo wa hatua baada ya nyingine wa kufanya ngono ya kusisimua

mwongozo wa kufanya mapenzi

  1. Kuwa na uhakika kuwa hili ndilo unataka

Hatua ya kwanza katika kuwa na ngono ya kusisimua ni kuhakikisha kuwa uko tayari. Kufanya uamuzi kamili kuwa hili ndilo ungetaka na matokeo yoyote utakayo yapata. Kuhisi kuwa tayari huku kutakusaidia kufuata mwongozo ufuatao kwa urahisi.

2. Mwenzi wako anapaswa kutaka kufanya mapenzi na wewe

Kibali ni muhimu sana. Mtu unaye taka kufanya mapenzi naye anapaswa kuwa amekubali kuwa angetaka kufanya kitendo hiki na wewe. Hawapaswi kutokuwa na uhakika kuhusu jambo hili. Wanapo sema apana, unapaswa kuheshimu uamuzi wao na kutafuta mtu mwingine. Mambo hayataenda vyema uki sisitiza kufanya mapenzi na mtu asiye kutaka.

3. Tumia kinga

Kuna maradhi mengi ambayo yana ambukizwa kupitia kwa ngono. Kwa hivyo ni vyema kuhakikisha kuwa unatumia kinga unapofanya mapenzi wakati wote. Zungumza jambo hili na mchumba wako.

4. Chagua mahali ambapo mngependa kufanyia kitendo hiki

faida za tendo la ndoa

Hii ni mara yako ya kwanza, kwa hivyo ungependa kuhakikisha kuwa una angalia nyuma kwa siku hii na kutabasamu. Chagua mahali ambapo pana vutia. Unaweza tafuta chumba hotelini unayo ipenda. Hakikisha kuwa chumba hicho ni kisafi, na kuna mwangaza wa kutosha na pia ni salama.

5. Anza na busu

Busu ndiyo hatua ya kwanza katika kumtayarisha mwenzi wako kwa kitendo hiki. Mkaribie, kisha kwa ustadi na upole, ubusu midomo yake. Kuwa mwangalifu usitumie nguvu nyingi sana. Baada ya busu hilo, endelea kumpapasa na kumbusu zaidi. Usione haya.

6. Kitendo

Utajua wakati wa kitendo unapo fika. Sehemu hii ya ngono inajulikana na watu wasio chukua muda kujua jinsi wanavyo paswa kufanya ngono huenda wakafikiria kuwa hii ndiyo sehemu pekee na iliyo muhimu zaidi. Unapaswa kumtayarisha mwenzi wako vyema ili kupunguza uchungu wa kufanya mapenzi mara ya kwanza.

7. Kuendeleza kitendo

Unapo ingia ndani, epuka kufanya kitendo hiki kwa nguvu sana kwani huenda uka mwumiza mwenzi wako. Kuwa mpole na ukifanye kwa utaratibu. Nyote wawili mnapaswa kukifurahia kitendo hiki.

Hakikisha kuwa unamwongelesha kujua kama anakifurahia ama la.

8. Hitimisho

Baada ya kuhitimisha kitendo hiki, mnapaswa kukoga kisha mpumzike.

Kusoma mwongozo wa kufanya mapenzi ya kuvutia ni muhimu hasa kwa mara yako ya kwanza ili ufurahie kitendo chako cha kwanza.

Chanzo: NHS

Soma pia:Mitindo 10 Ya Kufanya Mapenzi Katika Kipindi Hiki Cha Lockdown Na Mwenzio

Written by

Risper Nyakio