Mnyonyeshe Mtoto Wako Kwa Kutumia Mwongozo Huu

Mnyonyeshe Mtoto Wako Kwa Kutumia Mwongozo Huu

Wiki za kwanza za kunyonyesha huwa wakati mgumu na pia wa kusoma na huenda ukapata ukizidiwa mara kwa mara na hauko peke yako. Wakati ambapo kunyonyesha wakati wote ni kawaida na kuna kusaidia kuongeza maziwa ya mama uliyo nayo, na huenda ikachoka sana. Kwa hivyo kuwa mpole, na ujitunze, na bila shaka mambo huendelea kuwa rahisi zaidi. Mwongozo huu wa kunyonyesha utakusaidia pakubwa.

Mwongozo wa kunyonyesha: Wiki ya Kwanza

Mnyonyeshe Mtoto Wako Kwa Kutumia Mwongozo Huu

Mtoto anapaswa kunyonyeshwa mara ngapi?

Kunyonyesha mtoto mara kwa mara huhimiza usambazaji mzuri wa maziwa na kupunguza chuchu kufura. Lenga kumnyonyesha angalau mara 10-12 kwa kila masaa ishirini na manne. Hauwezi nyonyesha mara nyingi sana - unaweza nyonyesha kidogo.

Mnyonyesha unapo ona ishara za njaa kama vile kuweka vidole mdomoni - usingoje hadi mtoto aanze kulia. Mkubalishe mtoto anyonye kwa kipindi anacho taka bila kumdhibiti wakati, kisha umpe titi la pili. Kuna watoto wachanga ambao huwa na usingizi mwingi kupindukia hapo mwanzoni - amsha mtoto anyonye akipitisha masaa mawili mchana ama masaa manne wakati wa usiku bila kunyonya.

Je, mtoto anapata maziwa tosha?

mwongozo wa kunyonyesha

Ongezeko la uzito: Watoto wachanga wa kawaida huenda wakapoteza hadi asilimia 7 za uzito wa kuzaliwa katika siku za kwanza chache. Baada ya maziwa ya mama kuingia, mtoto wa wastani anaye nyonyeshwa huongeza 6 oz/ kwa wiki (gramu 170/ kwa wiki). Mpeleke mtoto apimwe uzito baada ya wiki ya kwanza ama mwanzo wa wiki ya pili. Wasiliana na daktari wa mtoto na mshauri wako wa lishe ya mtoto iwapo mtoto haongezi uzito inavyo tarajiwa.

Diapers chafu: Siku za mwanzo, mtoto huwa na diaper moja iliyo chafuka kila siku ya maisha yake (siku ya kwanza moja, siku ya pili mbili.....). Baada ya siku ya nne, kinyesi kinapaswa kuwa cha kinjano na mtoto anapaswa kuwa na angalau diaper 3-4 kila siku ambazo ni saizi ya robo ya US (2.5cm) ama kubwa. Baadhi ya watoto huwa na kinya kila mara wanapo nyonya, ama hata zaidi- hii ni kawaida, pia. Kinyesi cha kawaida cha mtoto aliye nyonya huwa laini na sio kigumu.

Diapers zenye mkojo: Katika siku za mwanzo, mtoto huwa na diaper moja kwa kila siku ya maisha yake (siku ya kwanza huwa na diaper moja, ya pili, mbili na kadhalika..). Mara maziwa ya mama yanapo ingia, tarajia diaper 5-6 zenye mkojo kila masaa 24. Kujua jinsi diaper iliyo jaa mkojo inavyo hisi, mwaga vijiko vitatu vya maji (45ml) kwenye diaper safi. Tishu ndogo kwenye diaper ya kutupa inaweza kusaidia kujua iwapo diaper ina mkojo.

Mabadiliko kwenye matiti

mwongozo wa kunyonyeshamtoto mchanga

 

Maziwa yako yanapaswa kuanza kuingia (kuongezeka kwa idadi na kubadilika kutoka kwa colustrum hadi kwa maziwa yaliyo komaa) kati ya siku 2 hadi 5. Ili kupunguza kufura kwa titi: nyonyesha mara kwa mara, usikose kumnyonyesha mtoto (hata usiku), hakikisha ameshika chuchu inavyo faa, mshike vizuri na umkubalishe amalize titi la kwanza kabla ya kumpa hilo lingine. Kupunguza kutokuwa na starehe kufuatia kufura, unaweza kamua maziwa hadi chuchu iwe laini, kisha ujaribu kumnyonyesha tena.

Ita daktari wako ama mshauri wa lishe iwapo:
  • Mtoto hana diaper zenye mkojo ama zilizo chafuka
  • Mtoto ana mkojo wa rangi nyeusi baada ya siku ya 3 (inapaswa kuwa ya kinjano chepesi ama isiyo na rangi)
  • Mtoto ana kinyesi cha rangi nyeusi baada ya siku ya 4(kinapaswa kuwa cha kinjano)
  • Mtoto ana diaper chache zilizo chafuka kuliko tulizo shauri
  • Mama ana ishara za ugonjwa wa mastitis(chuchu zinazo uma, homa ama kuhisi baridis)

Vitu vifuatavyo ni kawaida:

 

  • Kunyonya mara kwa mara na kwa kipindi kirefu
  • Kunyonya mara tofauti kwa siku
  • Kunyonya kwa vipindi vinavyo karibiana (mara kwa mara hadi kunyonya wakati dhabiti) kwa masaa mengi - mara nyingi -  jioni -  kila siku. Huenda kipindi hiki kika ingiliana na wakati anapo kuwa msumbufu ambao watoto wengi huwa nao miezi ya kwanza michache.

Je, mtoto anapata maziwa tosha?

Kuongeza uzito: Mtoto wa wastani aliye nyonyeshwa huongeza ounsi 6/kwa wiki (gramu 170 kila wiki). Ongea na daktari wa mtoto wako na mshauri wa kunyonyesha unaye fanya kazi naye, ikiwa mtoto wako haongezi uzito inavyo faa.

Diapers chafu: Tarajia kinya mara 3-4+ kwa siku saizi ya 2.5 cm ama zaidi. Baadhi ya watoto huwa na kinyesi kila mara wanapo nyonya ama mara nyingi zaidi, na hii ni kawaida. Kinyesi cha kawaida cha mtoto aliye nyonya ni cha kinjano ana laini na huenda kikaonekana kana kwamba kina mbegu. Baada ya wiki 4-6, baadhi ya watoto hunya mara zaidi. Na ni sawa bora mtoto anaongeza uzito inavyo faa.

Diapers zenye mkojo: Tarajia diaper 5-6+ zenye mkojo kila masaa ishirini na manne. Kuhisi diaper yenye maji ilivyo, unashauriwa kumwaga vijiko vitatu vikubwa kwenye diaper safi. Kutumia kipande kidogo cha tishu kutakusaidia kujua iwapo diaper ina mkojo. Baada ya wiki 6, diaper zenye mkojo huenda zikapunguka na kuwa 4-5 ila kiwango cha mkojo kwenye diaper kita ongezeka kwani sehemu ya kuhifadhi mkojo ya mtoto inaendelea kukua.

Mwongozo wa kunyonyesha: Kiwango cha maziwa

Baadhi ya wamama huwa na shaka kuhusu kuwepo kwa maziwa. Bora mtoto ana kua inavyo faa kwa kunywa maziwa ya mama pekee, kiwango cha maziwa kilichoko kina tosha. Kupata idadi ya diaper zilizo chafuka na zenye mkojo ni ishara kuwa mtoto anapata maziwa tosha.

Chanzo: Parents

Soma pia: Wataalum Wanashauri Kufanya Hivi Ili Kumfanya Mtoto Alale

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio