Mwongozo Wa Mimba Wiki Baada Ya Nyingine

Mwongozo Wa Mimba Wiki Baada Ya Nyingine

Safari ya mimba huwa katika vikundi vitatu vinavyo julikana kama trimesta. Kila trimesta huwa na hatua muhimu kwa mama na mtoto wake. Kuna mabadiliko muhimu yanayo shuhudiwa katika kila trimesta. Tazama makala yetu kuhusu mwongozo wa mimba.

Mwongozo Wa Mimba Kwa Mama

mwongozo wa mimba

Trimesta ya kwanza

Trimesta ya kwanza huwa kipindi kati ya wiki moja hadi wiki 12 ya ujauzito. Katika trimesta hii, fetusi huanza kukua akili, uti wa mgongo na viungo vya mwili. Mtima wake pia huanza kupiga.

Mama huwa katika hatari ya mimba kuharibika ama kupoteza mimba katika trimesta hii. Kulingana na madaktari wa afya ya uke, moja kati ya mimba kumi huharibika. Na visa hivi mara nyingi hushuhudiwa katika trimesta ya kwanza. Unapo shuku kuwa una poteza mimba yako ama kuvuja damu nyingi katika trimesta hii, wasiliana na daktari wako bila kusita.

Trimesta ya pili

Hii huwa kati ya wiki 13 hadi 27 za ujauzito. Katika kipindi hiki, daktari humfanyia mama ultrasound kudhibitisha ikiwa kuna matatizo yoyote katika ujauzito wa mama na ili kubaini jinsia ya mtoto anaye tarajia.

Utaanza kuhisi mtoto wako akirusha mateke ama kusonga kwenye uterasi katika trimesta hii. Ni jambo lenye hisia za kufurahisha. Una shauriwa kuanza kuzungumza na mtoto wako mara kwa mara hata kama angali tumboni mwako. Kwani mtoto hufahamu sauti ya mamake, na kufanya hivi kuna zidisha utangamano kati ya mama na mwanawe.

Trimesta ya tatu

mwongozo wa mimba

Kipindi kutoka wiki ya 28 hadi 40. Mama hushuhudia ongezeko la uzito katika wiki hii na utahisi kuchoka zaidi. Huenda ukashindwa kufanya kazi nyingi. Ni vyema kujitenga na kazi ngumu zinazo shinikiza mgongo ama tumbo yako.

Katika trimesta hii, mtoto ana weza kufungua na kufunga macho yake na mifupa mwilini ina endelea kukua. Ni kawaida kwa mama kushuhudia kufura kwa miguu katika trimesta yake ya tatu ya ujauzito. Kufuatia ongezeko la uzani wa mwilini na kushinikiza miguu.

Hitimisho

Safari ya ujauzito huwa ya kusisimua hata kama ina nyakati zenye hisia tofauti kwa mama. Una soma mengi na pia kupata fursa ya kupatana na wanawake wengi wanao tarajia kujifungua pia. Kumbuka kuwa hata kama mambo yanayo tendeka katika kila trimesta huenda yakawa sawa kwa wanawake wengi, kila mwanamke ni tofauti na safari yake haifanani na ya mwingine.

Soma Pia: Kipimo Bora Cha Kupima Mimba Kwa Upesi

Written by

Risper Nyakio