Je, umejihami kabisa, tayari kumkaribisha mtoto wako? Kabla ya kuwa na shaka, hapa kuna mwongozo wa ujauzito wa vitu vya kuangalia dakika ya mwisho kabla ya maisha yako kubadilika kabisa. Twa kutakia mema katika safari yako mpya!
Siku chache zimebaki kabla ya mtoto wako kuwasili na huenda ukawa na uwoga mwingi zaidi. Kwa wakati huu, huenda ukawa usha anza mapumziko ya mama mjamzito na huendi kazini tena ili uwe na wakati tosha wa kujitayarisha.
Ikiwa u-miongoni mwa wamama wengi ambao hawajifungui kabla ama hata siku wanayo tarajia mtoto wao kuwasili, mchezo wa kungoja huenda ukawa na mawazo mengi. Kwa hivyo badala ya kujitia mawazo mengi, angalia vitu hivi kuhakikisha kuwa uko tayari asilimia 100 kumkaribisha mtoto wako.

Mwongozo wa ujauzito; vitu unavyo paswa kuangalia dakika ya mwisho
Safisha mavazi yote ya mtoto wako
Haijalishi ikiwa ulinunua nguo za mtoto wako kwenye duka na bado ni mpya. Nguo zote zinapaswa kufuliwa kabla ya mtoto kuzivalia. Watu wengi wamezigusa nguo hizi kabla uzinunue, ni vyema kuziosha ziwe safi na kumlinda mtoto wako kwani bado mchanga na hana mfumo dhabiti wa kukumbana na maradhi.

Suuza ama utumie vitakasio kusafisha chupa za mtoto
Huenda watu wengi waka puuza jambo hili kwani mara nyingi tunafikiria kusafisha chupa baada ya kuona uchafu ama baada ya kuzitumia. Walakini, nguo hizi, na chupa zimeguswa na mikono mingi, kwa hivyo ni vyema kuwa salama.

Nunua pedi za chuchu
Huenda wamama wa mara ya kwanza waka puuza hili wakidhania kuwa sio muhimu - ila zina manufaa sana. Zina saidia maziwa ya mama yanayo mwagika kuto onekana kwenye nguo. Na kuepusha nguo zako kupata madoa.
Angalia kiti cha gari ulicho kinunua
Ikiwa wewe ni mmoja wa wazazi walio barikiwa na gari, ni vizuri ununue kiti cha gari cha mtoto, kita saidia kumwegemeza inavyo faa. Kwa njia hii, safari zenu zitakuwa rahisi, angalia kuhakikisha kuwa kiti chake kiko sawa na kinafungika inavyo faa na kiko salama. Jaribu kukitoa na kukirudisha bila usaidizi ili uwe stadi wa kufanya hivyo.

Begi ya hospitali
Angalia mkoba wako wa hospitali kuhakikisha kuwa umeweka kila kitu unacho hitaji unapo enda hospitalini. Baadhi ya vitu unavyo paswa kuwa navyo ni kama vile; nguo za mtoto, pamba, nguo zako za kubadilisha, simu, pesa za kutosha. Pia ni vyema kuhakikisha kuwa umempigia rafiki, ama jamaa ambaye ungependa akupeleka hospitalini siku ikiwadia.
Pumzika
Jaribu kutulia, punguza mawazo yako kwa kufikiria kuhusu kitu kingine mbali na kujifungua kwa mtoto wako ambako kuna wadia. Hata kama halitakuwa jambo rahisi kufanya. Furahia wakati wako na marafiki ama hata na mchumba wenu kabla familia yenu ikuwe kubwa na maisha yenu yabadilike.

Unaweza fanya mambo ambayo mnapenda kufanya kwa pamoja, kama kwenda mahali pa kuvutia na kuburudika, ikiwa unapenda kukaa nyumbani, unaweza jaribu kusoma kitabu ama hata kupigwa masi ya tumbo. Baadhi ya wamama pia hupenda kupika, ama kuoka keki na mikate. Furahia kipindi hiki kabla ya maisha yako kubadilika.
Soma pia: Jinsi Ya Kujitayarisha Usiku Kabla Ya Upasuaji Wa C-Section
Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Prianka na kuchapishwa tena na idhini ya theAsianparent kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio