Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 3

Ukuaji na Hatua Muhimu: Mtoto Wako Wa Miaka 6 Miezi 3

Kuna mambo mengi sana ambayo mtoto wako wa miaka 6 miezi 3 ana uwezo wa kufanya!

Wakati ambapo huenda kukawa na tofauti zilizo dhahiri ikifika ni ukuaji wa mtoto wako wa miaka 6, kuna baadhi ya vitu ambavyo ni kawaida. Jambo la kawaida kwa mtoto wa miaka 6 miezi 3, ni kuwa kucheza ni jambo la muhimu kwao. Kucheza hukuwa kugumu zaidi ambapo watoto wanaanza kusoma na kuyaelewa mambo wanapo ingiliana na watu wengine.

Kuiga kana kwamba unacheza ni jambo la kawaida kwa watoto wa miaka 6 miezi 3. Wakati huu, wanaanza kuiga majukumu tofauti - wasichana wana iga kucheza kama wamama na wavulana kama wababa. Imejazwa na ubunifu na kuigiza.

Wazazi, jua kwamba hiki si kipimo dhahiri ila ni mwongozo tu. Usi site kuwasiliana na daktari wako kutoa shaka zozote ambazo huenda ukawa nazo wakati huu kuhusu ukuaji wa mtoto wako.

Tuna angazia kwa umakini hatua muhimu ambazo mtoto wako wa miaka 6 miezi 3 anapaswa kufikisha katika hatua hii.

Ukuaji na Hatua Muhimu, Mtoto wako wa Miaka 6 Miezi 3: Je, mtoto wako anakua ipasavyo?

play is an important factor for a child's growth at 6 years 3 months old

Ukuaji wa Kifizikia

Katika miaka 6 miezi 3, mtoto wako anashughulika kifizikia kuliko hapo awali! Misuli yake midogo ama mikubwa imeikua, na kupelekea katika usawa zaidi na kuandamanisha mambo. Pia huenda ikaonekana kana kwamba hawezi tulia. Ana furahikia na kuinua mikono mara kwa mara anapo tazama televisheni ama anapo lala, unaelewa? Ila, usitie shaka, sio jambo kubwa la kukutia wasiwasi wazazi.

Mtoto wako mdogo pia anaanza kuonyesha hamu katika michezo kama vile kadanda. Hii ni nafasi kuu kwake ya kuanzisha michezo ya kifizikia itakayo msaidia mwanao kujua mambo ambayo angetaka kufanya.

Inapo fika ni mwendo wa mtoto wako, bila shaka anaonyesha kuimarika. Habari njema, kwa sababu kunamsaidia kuonyesha uhuru na kujitegemea kwake katika kazi zake za kila siku kama vile kufunga vifungo na nyororo, na pia kuichana nywele yake.

Katika hatua hii, kimo cha urefu na uzito wa mtoto wako* kinapaswa kuwa ifuatavyo:

 • Wasichana
  – Urefu: 117.3 cm (46.2 inchi)
  – Uzito: 21.4 kg (47.1 lb)
 • Wasichana
  – Urefu: 116.7 cm (46.0 inchi)
  – Uzito: 20.9 kg (46.2 lb)

Tuna angazia baadhi ya ukuaji wa kifizikia kwa mtoto wako wa miaka 6 miezi 3:

 • Kuendesha baiskeli
 • Kusimama kwa mguu mmoja kwa muda mfupi
 • Kutembea kwa visigino
 • Kushuka ngazi za nyumba bila msaada
 • Kufunga kamba za viatu zake
 • Kutumia nyororo na vifungo
 • Kuchana nywele zake
 • Kuruka na kushika mpira mkubwa
 • Kuchora michoro ya kweli (kwa mfano, uwezo wa kuchora mtu aliye na kichwa na macho, mdomo, mapua na mwili ulio na mikono na miguu)
 • Kuiga michoro rahisi kwa kutumia penseli
 • Anaandika jina lake

Wakati ambapo huenda mtoto wako akapata kazi zingine kuwa ngumu kidogo, kama vile kutumia kisu kula chakula chake, bado anafurahikia nafasi ya kufanya hivi.

Vidokezo vya ulezi:

 • Himiza mwendo katika mtoto wako. Hakikisha anajihusisha katika michezo tofauti na shughuli za mapumziko, pamoja ama na wengine.
 • Fikiria kuhusu darasa za kuogelea na kumfunza mtoto wako kuhusu usalama wa moto.
 • Watoto wa umri huu huenda wakateta kuhusu uchungu wa nje kama vile kuumwa na tumbo, miguu. Wazazi hawapaswi kupuuza maneno haya, hakikisha kuwa hakuna maradhi ama kuumia.
Wakati wa kumwona daktari:

Iwapo unafikiria kuwa mtoto wako wa miaka 6 na miezi 3 anabaki nyuma, tulia ila, uwe makini kwa yafuatayo:

 • Mtoto wako ataanza kushuhudia kupoteza uwezo ambao alikuwa nao hapo awali. Mlete mtoto wako atembelee mtaalum iwapo jambo hili lita tendeka.
 • Kukujoa kitandani: Wakati ambapo mtoto wako hakuwa anafanya hivi hapo awali ila kwa sasa anaanza kukojoa kitandani. Kibofu chake na boweli ina dhibitiwa na umri wake na kuishi kwa kipekee.
 • Iwapo mtoto wako anatatizika kulala ama kupata usingizi usiku.

mtoto wa miaka 6 miezi 3

Ukuaji wa Kiakili

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 3, anaendelea kukua umakini zaidi, na uwezo wa kufanya mambo magumu na kazi ngumu anapokuwa shuleni ama nyumbani.

Sio hilo tu, ana uwezo wa kuelewa vitu rahisi kama vile wakati (leo, kesho na jana), anagundua maneno mepesi kwa kuyaona na kujaribu kuyasoma maneno. Huenda akaweza kujisomea kwa kipekee.

Ni katika hatua hii ambapo mtoto wako anakuwa na uwezo wa kuona vitu vizuri kulingana na maoni ya mwingine. Hiki ndicho kinamsaidia kupata marafiki kwa urahisi.

Kuwa makini kwa hatua hizi katika mtoto wako:

 • Anaelewa kuhusu nambari
 • Kutambua mchana na usiku, kushoto na kulia
 • Hamu iliyo ongezeka ya kujua kuhusu dunia inayo mzingira
 • Uwezo wa kuwa na mawazo magumu
 • Anajua kati ya mbaya na nzuri
 • Uwezo wa kusema wakati
 • Kurudia nambari tatu kinyume nyume
 • Kuwa makini na shughuli za shule kwa dakika 15

Vidokezo vya ulezi:

Huenda ikawa kawaida kwa mtoto wako kushuhudia kuto elewana na marafiki wake wa ndani. Katika visa kama hivi, inasaidia iwapo wazazi (na walimu) wanaweza onyesha mwongozo wa kimapenzi kusaidia kuongoza mtoto kwa mawazo yake.

Wakati wa kumwona daktari:
 • Wakati ambapo mtoto wako anaonyesha tabia nyingi changamoto
 • Anaonyesha tabia nyingi za kujitenga na watu, kuhuzunika, shaka ama kukwaza kifikira
 • Ana tatizika kujitenga nawe
 • Kutatizika kufuata maagizo pande mbili kama vile, " Weka mkoba wako na kisha uniletee sare za kadanda."

mtoto wa miaka 6 miezi 3

Ukuaji wa Hisia na Muingiliano

Mtoto wako wa miaka 6 miezi 3 kwa sasa ana uwezo wa kueleza hisia zake. Walakini, unapo kumbana na hisia zake kama vile za wivu ama kuhuzunika, huenda akahitaji usaidizi na wakati kuongea kuhusu mambo haya.

Hayo kusemwa, kwa sasa mtoto wako anadhibiti hisia zake vyema zaidi na huenda ukatarajia kuwa na hisia nyingi mara kwa mara kama vile kukasirika ama kuhuzunika. Huenda pia akajaribu kuonyesha jinsi alivyo "mkubwa" ama "huru" kwa kujaribu kufanya mambo ambayo huenda yakawa hatari.

Watoto katika umri huu bado wanajaribu kugundua wanapo toshea na kinacho kubalikwa. Kwa hivyo huenda wakajaribu kupima mambo haya kwa kuhusika katika kudanganya, ama kuiba.

Kwa ujumla, mtoto wako mdogo atahitimisha hatua hizi katika umri huu:

 • Anakuwa weka umuhimu zaidi katika kukualika na wanarika wake. Wanasoma njia za kushirikiana na kugawa vitu vyao.
 • Anaanza kupata uwezo na umakini uliongezeka
 • Anaelewa umuhimu wa michezo ya vikundi.
 • Anakuwa mwema zaidi katika kueleza matukio yaliyo tendeka: Wanacho hisi ama kufikiria, wanapo ingiliana na wanarika wao kinaongezeka.
 • Viwango vilivyo ongezeka vya utulivu na kuwa huru zaidi kuya fikiria mambo nawe.
Vidokezo vya ulezi:
 • Usiaibike kuongea kuhusu mada ngumu na watoto wako kama vile shinikizo la wanarika, vurugu, uraibu wa madawa ama jinsia.
 • Tafuta njia ya kuyajibu maswali yake kwa lugha ya umri wake bila ya kumwongeza uwoga.
 • Mkubalishe mtoto wako kufanya uamuzi wake kuhusu michezo ama vidoli.
 • Tegemeza kujiamini na kumhimiza kufurahikia ama kujieleza.
 • Mhusishe mtoto wako katika kufanya kazi za kinyumbani: Kuiandaa meza ama kukusaidia kupanga nguo safi.
 • Panga siku za kucheza zinazo msaidia mtoto wako kupata wakati na watoto wengine.
 • Ongea kuhusu hisia za mtoto wako naye na umsaidie kueleza hisia zake kwa maneno.
Wakati wa kumwona daktari:
 • Iwapo mtoto wako ni mtulivu zaidi ama ananyamaza kwa sana baada ya kutoka shuleni, huenda ikawa ishara ya kunyanyaswa.
 • Anapo onyesha dalili nyingi za ukatili.

mtoto wa miaka 6 miezi 3

Ukuaji wa Lugha na Mazungumzo

Katika miaka 6 miezi 6, mtoto wako atakuwa na mengi ya kusema, hata pasipo na mtu chumbani. Mbali na hayo, ubongo wake hufikiria kwa kasi kuliko asemacho.

Wakati ambapo mtoto wako huenda akaanza kuongea kwa sentensi kamili  na kuanza kuhusika katika mazungumzo ya watu wazima. Huenda akatatizika kusema mawazo magumu.

Shuleni, mtoto wako anafurahikia nafasi ya 'kufanya na kuonyesha shuleni'. Pia, si vigumu kwake kuelewa ucheshi ama vitendawili.

Hatua zingine za lugha na matamshi kwa mtoto wako wa miaka 6 na miezi 3 ambazo mtoto wako huenda akawa amefikisha katika hatua hii:

 • Anasoma kiwango cha majina 5-10 mapya kila sikua
 • Anaongea kwa sentensi fupi zilizo kamilika za majina 5-7
 • Anafuata maagizo matatu kwa kufuatanisha
 • Anaanza kugundua kuwa baadhi ya majina yana maana zaidi ya moja
 • Anaanza kusoma vitabu vilivyo sawa kwa umri wake
 • Anayatamka majina ambayo hajazoea
Vidokezo vya ulezi:
 • Jaribu ujue wasimamizi wa shule ya mtoto wako na walimu wake.
 • Endelea kumsomea mtoto wako, na pia umhimize akusomee.
 • Husika katika mtoto wako kufanya kazi yake ya ziada, lakini kama mtu wa kumwonyesha pale tu unapo hitajika.
 • Jifunze tabia ya darasani. Mpatie mtoto wako kazi ndogo ndogo kumfanya awe makini kufuata maagizo mepesi.
 • Kuwa na mazungumzo kuhusu mambo ambayo mtoto wako anapenda ama pia mnyama ama mchezo aupendaye, ambayo yatamhimiza kusikiza, kuitikia na kukuuliza maswali.

Wakati bora kumwona daktari:

Kuwa mwangalifu kwa mambo yafuatayo iwapo unafikiria mtoto wako wa miaka 6 miezi 3 anabaki nyuma kwa mambo yafuatayo:

  • Kutatizika kusoma ama mtoto kuonyesha ishara za kuwa na ulemavu
  • Kitu ambacho kinamsumbua mtoto wako kama vile kunyanyaswa.
  • Dalili kuwa mtoto wako anaonyesha kukwaza kifikira ama tatizo la afya ya kiakili

Kumbuka kuwa mtulivu iwapo kisa chochote kati ya hizi kinatokea.

mtoto wa miaka 6 miezi 3

Afya na Lishe: Mtoto wako wa miaka 6 na miezi 3

Ni muhimu kusaidi mtoto wako wa miaka 6 na miezi 7 kufanya shughuli za kifizikia. Cha muhimu kwa uzito wa afya? Angalau dakika 60 za michezo ya kifizikia kwa watoto na wazazi.

Kwa kuyasema hayo, itasaidia kwa wingi kufurahia matunda, mboga na michezo ya kifizikia kwa afya ya mtoto wako, badala ya kuzingatia uzito wa afya.

Baada ya yote, kitu chema zaidi cha kumfanyia mtoto wako ni kuiga tabia njema za kula na kufanya mazoezi.

Vidokezo:

 • Hakikisha kuwa wakati wote unatumia "nafaka zilizo 100%" badala ya" vyakula vilivyo tengenezwa na nafaka," vifaa vilivyo na nafaka zilizo tengenezwa ndani yake.
 • Unapo pika vyakula kama vile nyama nyekundo ama vilivyo na iron kama vile maharagwe ama mbogo, unashauriwa kutumia vyakula viwili vilivyo na viwango vya juu vya vitamini C, kama vile viazi vitamu ama nyanya - inasaidia mwili wa mtoto wako kutumia iron nyingi.
 • Weka kiwango kidogo cha chakula kwa watoto wako na kumwongeza anapo taka.
Watoto wa umri huu kwa kawaida hukula vitu vifuatavyo kila siku:

Mwongozo unao shauriwa wa lishe ya kila siku kwa mtoto wa miaka 6 ni angalau kalori 1,200, ukihusisha vyakula kutoka kwa familia tofauti za virutubisho kama vile maziwa, protini, matunda na mboga.

Kwa ujumla, kiwango cha kalori cha wavulana na wasichana katika umri huu kinapaswa kuwa hivi:

 • Wavulana: 1,773 Kcal/kwa siku
 • Wasichana: 1,664 Kcal/kwa siku
Familia ya maziwa

Mojawapo ya virutubisho muhimu zaidi kwa mtoto anayekua ni maziwa. Mtoto anahitaji vikombe 2.5 za maziwa ama yoghurt kwenye lishe yake- hakikisha unachagua vyakula vyenye ufuta mdogo.

Habari njema ni kuwa maziwa huenda yakafichwa kwenye chakula ambacho mtoto wako anakipenda zaidi kama vile oatmeal, matunda ama smoothies za kutengenezwa. Pia weka kwa mayai ya mtoto wako.

Familia ya protini

Kwa watoto wenye miaka 6, shirika la CDC linawasiliana angalau gramu 19 za protini kila siku. Kwa wazazi wanao pambana na watoto wanao chagua vyakula, usitie shaka!

Vyanzo muhimu za protini ambazo watoto wadogo hufurahikia ni kama vile mayai, waffles na karanga.

Pia, unaweza jaribu yoghurt ili ya ufuta wa chini na matunda juu yake. Pia, kuku ama nyama ya nguruwe na maharagwe nyeusi.

Familia ya matunda na mboga

Huu ni wakati mwafaka wa kuwa m-bunifu na vyakula. Kuna aina nyingi sana za matunda, na marangi za kujaribu. Mtoto atahitaji angalau kikombe 1 cha matunda na vikombe 1.5 za mboga kusawasisha lishe yao ya siku.

Nafaka

Unapaswa kumwanzishia mtoto wako nafaka vyema. Unaweza mpatia ounsi 4 za nafaka kila siku. Huenda ikawa ni kikombe kimoja cha cereal zilizo tayari kuliwa, kipande kimoja cha mkate ama nusu kikombe cha pasta ama cereal zilizo pikwa. Hizi zote mara nne kwa siku.

Unaweza chagua nafaka, kama vile oatmeal, quinoa, mkate wa wimbi mzima, popcorn, mchele wa hudhurungi. Ila, hakikisha kuwa unapunguza nafaka zilizo tengenezwa kama vile wali, pasta ama mkate mweupe.

Kwa kifupi, hapa ni mahitaji ya mwanao ya kila siku (tazama hapo juu kuona viwango vinavyo hitajika):

 • Matunda: vikombe vitatu kwa wavulana; na vitatu kwa wasichana
 • Mboga: vikombe viwili kwa wavulana; na kikombe viwili kwa wasichana
 • Nafaka: ounsi nne kwa wavulana; ounsi nne kwa wasichana
 • Protini: gramu 32.4 kwa wavulana; gramu 32.4 kwa wasichana
 • Maziwa: 17-20 ounsi kwa wavulana; 17-20 ounsi kwa wasichana
 • Maji: 1500 ml kwa wavulana; 1500 ml kwa wasichana (karibu vikombe sita)

Vidokezo: 

 • Mwanzishie matunda na mboga kama vyakula vidogo. Weka matundwa yakiwa yameoshwa, kukatwa na kuonekana kwa urahisi kwenye friji.
 • Tengeneza saladi nyingi mara kwa mara.
 • Fikiria kujaribu kupika vyakula vya mboga bila nyama: tumia mboga badala ya nyama unapo kipika chakula chako.
Wakati wa kumwona daktari:
 • Ana uzito mdogo zaidi ama mwingi zaidi
 • Ana upele na vidondo visivyo vya kawaida
 • Joto zaidi ya 39 degrees C

Chanjo na Maradhi ya Kawaida: Mtoto wako wa miaka 6 miezi 3

Nyingi kati ya chanjo za mwanao zinapaswa kuwa zimeisha katika umri huu. Wasiliana na daktari wako kwa chanjo za kawaida ambazo mtoto wako anahitaji kwa sana, kama vile flu shot.

Kadri mtoto wako anavyo kuwa shuleni kwa wakati mwingi, huenda akaugua ama akakosa maradhi ya kawaida kama homa na mafua. Pia, kuwa makini kuona upele unao ibuka kwenye mwili wa mwanao. Na cha muhimu zaidi, mtie moyo akwambie iwapo anahisi kujikuna mwili ama anahisi hayuko sawa.

Ni muhimu kwa wazazi kukumbuka kuwa watoto wote hushuhudia ukuaji tofauti. Kila mtoto ni wa kipekee. Inapofika kwa hatua muhimu, hii ni miongozo tu ila haipaswi kufuatwa kwa umakini.

Kutibu magonjwa ya kawaida

Kutibu matatizo ya kiafya yaliyo kawaida sana kwenye watoto- joto jingi, kukohoa na homa - fuata maagizo haya:

 • Kutibu joto jingi: Iwapo mtoto wako ana joto jingi hadi 38°C (100.4°F), unaweza jaribu matibabu machache ya kinyumbani. Tumia maji ya vuguvugu kumpaka mtoto wako, hasa iwapo ana joto jingi hadi 39 degree celsius. Mvalishe mtoto wako nguo nyepesi ili asibaki na joto jingi mwilini. Unapaswa kuhakikisha kuwa mtoto wako anakula vyema na ana maji tosha mwilini. Iwapo matibabu ya kinyumbani hatitafanya kazi, wasiliana na daktari wako kuhusu madawa ya kununua. Ila, kumbuka kuto tumia aspirin kwa watoto. Huenda ikasababisha Reye's syndrome - maradhi ya kutishi maisha ambayo yana athiri ubongo na maini.
 • Kutibu kikohozi: Mpe kijiko nusu cha asali nyeusi kama vile buckwheat, inayofanya kazi vyema kwa sababu ina idadi ya juu ya viungo vinakumbana na uongezeko wa kilo. Jaribu kumlisha mtoto wako supu ya kuku kwani ina uwezo wa kuosha mfumo wa mapua. Pia, unaweza mpatia mtoto wako maji moto ya sharubati ama chai iliyo pikwa na asali.
 • Kutibu homa: Kwa kawaida, homa inapaswa kuisha baada ya siku chache. Ila, iwapo haiishi, unaweza jaribu kutumia matibabu ya kinyumbani kama vile kuweka kifaa cha kupepeta hewa kwenye chumba cha mtoto wako. Karibu na yeye kusaidia kulegeza kifua chake. Inua kichwa cha mwanao kwa kutumia mto ama taulo iliyo kunjwa kumsaidia kupumua kwa urahisi.

Ni muhimu kujua kuwa wakati ambapo baadhi ya madawa huenda yakanunuliwa bila kushauriwa na daktari, unapaswa kujaribu matibabu ya kinyumbani. Hasa kwa matatizo ya kiafya mepesi. Kwa mfano, mtoto ambaye ana homa ama kikohozi anapaswa kupatiwa maji yaliyo na joto jingi.

Pia ni wazo la busara kumhimiza kuzingatia usafi kama vile kunawa mikono ili kuepuka kueneza magonjwa.

Wakati wa kumwona daktari

Iwapo mtoto wako,

 • Ana joto jingi zaidi ya 39 degrees Celsius
 • Ana upele, vidonda ama kugwaruzwa kusiko kwa kawaida
 • Kulia mara kwa mara kuhusu kuumwa na mwili ama kichwa
 • Amekuwa akitapika ama kuendesha zaidi ya siku mbili

Kumbukumbu: WebMD

Mwezi uliopita: 6 years 2 months

Mwezi ujao: 6 years 4 months

Vyanzo: Webmd, Kidshealth, MSF

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio