Hongera kwa kufika umbali huu! Kwa sasa ukatika wiki 37 ya ujauzito wako. Jiunge nasi tung’amue zaidi kuhusu mtoto wako katika wiki hii.

Mtoto Wako Ni Mkubwa Kiasi Gani Katika Wiki 37?
Mama, saizi ya mtoto wako imeongezeka kiasi cha kutoshana na rockmelon. Utahisi kuwa tumbo yako imekuwa kubwa sana. Pia, katika wiki 37 ya ujauzito, mtoto wako kwa sasa anachukuliwa kama mtoto aliyekomaa. Ana urefu wa sentimita 48.5 na uzito wa kilo 2.85.
Ukuaji wa Mtoto Wako
Katika mwongozo huu wa ujauzito wa wiki baada ya wiki, utagundua kuwa:
- Katika wiki 37, mtoto wako anajulikana kama mtoto aliyekomaa.
- Kichwa cha mtoto wako kwa sasa kimezingirwa na kulindwa na mifupa ya pelviki; kichwa kinapumzika kwenye nafasi ya pelviki.
- Kwa sasa, mtoto wako ana nywele zenye urefu wa hadi sentimita 3.5 na hana nywele zilizo ufunika mwili wake.
- Ana bingirika, kunyoosha na kutabasamu zaidi na anapenda kunyonya kidole chake cha gumba. Anapenda kuenda upande hadi mwingine huku akifunga funga macho.
- Mtoto wako anafanya mazoezi ya kupumua kwa kupumua nje na ndani amniotic fluid.
Dalili za ujauzito
- Huenda ukashuhudia usiku bila usingizi, shukrani kwa woga unaohisi kuhusu uchungu wa uzazi na kuwa mzazi. Kujumuisha kwa kuto starehe kwa sababu ya uzito ulioko kwenye tumbo lako.
- Wakati ambapo kuongezeka kwa uchafu wa uke ni kawaida, kuwa makini unapo ona makamasi ama viwango vidogo vya damu kwani kuna maana kuwa uchungu wa uzazi unakaribia. Iwapo uchafu wa uke wako ni mzito, wasiliana na daktari wako bila kusita.
Utunzaji wa Ujauzito
- Hakikisha una maji tosha mwilini. Haijalishi unavyo hisi kufura tumbo, ni muhimu kunywa glasi nane za maji kwa siku kupunguza kutokuwa na maji mwilini.
- Jipe masi ya kujitayarisha kwa siku yako kuu. Huku kutakusaidia kunyoosha perineum yako (sehemu ya ngozi kati ya uke wako na rectum yako) kwa juhudi za kuepuka kupasuka kwa episiotomy. Hapa ni jinsi ya kujipa masi ya perineal: Kwa kutumia mikono safi na kucha zilizo katwa, paka vidole vyako vya gumba mafuta na kisha uziingize kwenye uke wako. Sukuma chini kana kwamba kwenye rectum yako kisha katikati ya sehemu ya chini na upande wa perineum, na kuvuta polepole nje na mbele sehemu ya chini ya uke wako na vidole vyako vya gumba vikiwa ndani. Huku kunasaidia kunyoosha ngozi kwa njia sawa na vile ambavyo kichwa cha mtoto wako kitafanya wakati wa kujifungua.
Orodha muhimu ya kuzingatia
- Jiratibishe kabla ya wakati katika hospitali yako ili uwe na wakati rahisi siku ikifika.
Wiki yako ifuatayo: 38 Weeks
Wiki yako iliyopita: 36 weeks
Una maswali kuhusu mwongozo huu wa ujauzito wiki baada ya wiki? Shaka zako kwa wakati huu ni zipi mama? Tujulishe kwa kutuwachia ujumbe hapa chini!
Makala haya yamechapishwa tena kwa idhini ya theAsianparent