Wiki 38 Ya Ujauzito: Mwongozo Wako Wa Ujauzito Wa Wiki Baada Ya Wiki

Wiki 38 Ya Ujauzito: Mwongozo Wako Wa Ujauzito Wa Wiki Baada Ya Wiki

Hata katika hatua hii, mapafu ya mtoto wako bado haya kamilika kukua. Cha kufurahisha zaidi ni kuwa hata baada ya kuzaliwa kwake, atachukuwa muda kabla ya kutunga mfumo wa kupumua. Kwako mama, punguza woga wako kwa kununua vitu utakavyo hitaji ama kununua pampu ya matiti. Tuna orodha itakayo kusaidia kwa sana.

Mama, unakaribia siku yako kuu! Lazima uwe unafurahikia wazo la kupatana na mtoto wako mdogo. Kwa wiki 38 ya ujauzito wako, tarajia kuhisi mtoto wako akitembea tumboni mwako anapo endelea kukua tumboni mwako. Soma zaidi kujua mambo ya kutarajia katika mwezi huu.

week 38

Mtoto Wako Ni Mkubwa Kiasi Gani Katika Wiki 38?

Kwa sasa, mtoto wako anatoshana saizi ya leek na mwenye uzito wa kilo 3.1 na sentimita 46.8. Ana ufuta mwingi chini ya ngozi yake na anakaa mnene kuliko wiki za hapo awali.

pregnancy week 38

Picha shukrani kwa: Pixabay

Ukuaji wa Mtoto Wako

Katika mwongozo huu wa wiki baada ya wiki, utagundua kuwa:

  • Wakati ambapo viungo vingi vya mfumo wa mtoto wako huenda vikawa vimekuwa na viko mahala panapo faa, mapafu yake ingali kufika ukomavu wake. Hata anapo zaliwa, itachukua muda kutunga muundo wa kupumua.
  • Kucha za mtoto wako zimekuwa zikimea na kwa sasa zimefika mwisho wa vidole vyake vidogo.

pregnancy weekly guide

Dalili za Ujauzito
  • Kwa wakati huu, huenda miguu na vifundo vya mguu wako vikawa vimefura. Walakini, iwapo utashuhudia kufura kwenye mikono na uso, ama kushuhudia kuvimba kwa macho, wasiliana na daktari wako bila kusita.
  • Unastahili kuwa makini na dalili za preeclampsia zilizo kama vile kuumwa na kichwa, kuto ona vizuri, kichefu chefu, kutapika na kuumwa sana na sehemu ya chini ya mwili. Iwapo utashuhudia dalili zozote kati ya hisi, mpigie daktari wako kwa kasi ama ukimbie hospitalini.
  • Katika wiki 38 ya ujauzito, huenda matiti yako yakaanza kutoa maziwa ya kwanza ya mama, yaliyo ya kinjano chembamba ambayo yanatangulia maziwa ya mama. Yamejazwa na antibodies ambazo zinamlinda mtoto wako kutokana na maambukizo. Ina protini nyingi, ufuta mdogo na kiwango kidogo cha sukari kuliko maziwa ya mama yanayo kuja baadaye.
  • Miguu yako na sehemu yako ya uke itaanza kuhisi kuto starehesha japo mtoto wako anapofanya njia yake hadi sehemu ya chini ya pelviki na kusukuma dhidi ya neva zingine.
Utunzaji wa ujauzito
  • Iwapo matiti yako yanatoa colostrum (maziwa ya kwanza), wekelea pedi maarufu kama pads za kunyonyesha ili kuepuka kuchafua nguo zako. Kwa upande mwingine, usipo shuhudia kutoa maziwa, colustrum bado inatolewa kwani ni lishe ambayo mtoto wako anahitaji unapo mnyonyesha.
Orodha ya kuzingatia
  • Angalia kwa kina orodha yako kuhusu vitu ambavyo chumba cha mwanao kinahitaji. Hakikisha kuwa una vitu vyote unavyo hitaji kabla ya mtoto wako kufika.
  • Nunua pampu ya matiti yako iwapo unataka kuwa unayakamua maziwa yako. Hapa kuna mwongozo uliokamilika wa jinsi ya kununua pampu iliyo bora zaidi. Pia nunua pedi za matiti na sindiria za kunyonyesha.

Wiki yako ijayo: 39 weeks pregnant

Wiki yako iliyo pita: 37 weeks pregnant

Una maswali kuhusu mwongozo huu wa wiki baada ya wiki wa ujauzito? Mama, shaka zako ni zipi katika wakati huu? Tujulishe kwa kutuwachia ujumbe mfupi hapa chini!

Makala haya yamechapishwa tena kwa idhini ya theAsianparent

Written by

Risper Nyakio