Mambo 14 Ya Kuwachilia Ili Uwe Mzazi Mwenye Furaha

Mambo 14 Ya Kuwachilia Ili Uwe Mzazi Mwenye Furaha

Vidokezo hivi vina fanya safari yako ya ulezi kuwa wenye furaha.

Kuwa na jukumu la maisha ya mtu mwingine kama mzazi ni kazi isiyo rahisi. Una jukumu la kuchungu hisia, fizikia na fedha zake hata unapo jaribu kukumbana na mambo mengine nje ya nyumba. Kinacho ifanya iwe gumu zaidi ni kuwa kama mzazi unataka kuwa na udhibiti kwa kila kitu ambacho mtoto wako anafanya maisha mwake hata bila ya maana wakati mwingine. Ulezi sio lazima ukutatize, na ndiyo maana makala haya yana angazia mambo unayo paswa kuwachilia ile uwe mzazi mwenye furaha.

Mambo 14 unayo paswa kuwachilia ili kuwa mzazi mwenye furaha

Kujaribu kuwa mzazi mwenye furaha hakuna umuhimu kwa mtoto wako peke yake ila kwa familia kwa ujumla. Kulingana na utafiti umri wa mzazi, jinsia na mtindo wake wa ulezi na jinsi wanavyo tengeneza muundo wa hisia na wengine kulihusishwa na furaha yao. Baadhi ya hizi huwa ni zaidi ya uthibiti wetu, ila wengine wana nguvu za kufanya hivi. Hizi ni kama:

love and forgive

 • Epuka kukumbuka makosa ya jana

Watu wengi wazima wanaweza sema kuwa wazazi wao kwa wakati mwingi hawakuwai sahau makosa ya watoto wao. Wanangoja hadi watoto wao wafanye kitu ambacho kita leta makosa yao ya hapo awali na kuya leta pamoja hadi kwa kosa mtoto alilo fanya. Kisha wana sajili kukasirika kwao. Ili kuwa mzazi mwenye furaha, huenda ukalazimika kusoma kuwachilia makosa ya hapo awali ya mtoto wako. Makosa ni baadhi ya ukuaji. Hakuna maana kuwa mtoto wako ni mzigo.

 •  Epuka kusema "unapaswa"

Hakuna kitu kinacho ua uzazi kama kushikilia vitu fulani vilivyo fanywa hapo awali na kisha kuwa lazimisha watoto wako kuishi kwa njia hiyo. Vitu hivyo huenda vikawa vilifanywa hapo awali, ila, lazima uelewe kuwa mtoto wako alizaliwa mahali na wakati tofauti. Kujaribu kuwalazimisha kuishi na kufanya vitu unavyo taka ni kuwa nyima uhuru wa kujieleza na kukuza utu wao.

 • Wacha kuwapigia kelele

Watoto huenda wakakukera kwa tabia zao, ila hii sio sababu ya kuwapigia kelele. Kuwapigia kelele watoto wako hakusaidii katika uhusiano kati yako na wao kwani kuna wafanya wakuogope sana. Fahamu wakati na tabia zinazo kufanya uwapigie kelele na utafute njia bora ya kuzungumza nao na kuwa ambia jinsi mambo hayo hayakupendezi. Pia unaweza tumia njia za afya za kuwaadhibu.

shouting at your kids

 • Epuka kutumia nguvu

Ni vigumu kupata watu ambao hawakupitia kutumika kwa nguvu na wazazi wao walipokuwa wachanga. Nguvu hizi ni kama vile kuchapwa, kutishiwa ili mtoto afanye ifaavyo. Sikiza maoni ya mtoto wako unapo mwuliza afanye kitu anakataa. Na uwasaidie kuona na kuelewa sababu kwa nini maamuzi mengine yanafanywa kwa ajili yao. Kuwa na mjadala kunawasaidia kuongea na mtoto wako anajua kwamba uko tayari wakati wote kusikiza maoni yao.

 •  Epuka kuwa na malengo ya chakula

Wazazi ambao watoto wao hawakuli sana mara kwa mara huwawekea malengo ya chakula. Baadhi ya watu huwa na tabia ya kuwa na maoni kuhusu uzito wa wanao na jambo hili huwawekea wazazi shinikizo la kuwa lazimisha watoto wao kukula. Kuweka lengo la chakula kwa mtoto wako ambalo lazima atimize mwishowe mtavunjika moyo. Badala yake, jaribu kujua chakula ambacho mtoto wako anapenda na ufanye ufaavyo.

love

 • Epuka maamuzi unao egemea upande mmoja

Kwa sababu wewe ndiye mzazi hakumaanishi kuwa mtoto wako hapaswi kusema kitu chochote. Una usemi wa mwisho kama mzazi, ila baadhi ya wakati unapaswa kuhusisha mtoto wako katika kufanya uamuzi. Kutamsaidia kukuza kujiamini na ujasiri wake ili kuchukua majukumu ya uamuzi na vitendo vyake.

 • Wachana na jumbe hasi

Wazazi wengi huenda wakajipata kwa mtego wa kurudia jumbe hasi sana hadi kuna badili jinsi mtoto anavyo jioni na kuwafanya wawe na maoni hayo kujihusu. Kama mzazi, jaribu kuchukua vitu vyema kwenye mtazamo wa mwanao ulio hasi na uzitilie maanani. Badala ya kusema "unaongea sana" sema "kwa kweli unapata marafiki kwa urahisi."

 • Wachilia hadithi yako ya utotoni

Watu wengi walisikia wazazi wao wakiwa hadithia jinsi walivyo tembea kilomita nyingi bila viatu na jinsi walikosa chakula cha kukula kufuatia hali duni ya maisha na umaskini. Kurudia hadithi hizi huenda zikafanya watoto wapate uwoga wa siku za kale.

different generation parent

 • Epuka kujaribu kuwa bila doa ama sawa

Wazazi hujaribu kujiona na kufanya kila kitu kuhakikisha kuwa wako sawa bila doa ili kupatia watoto wao mfano bora zaidi wa kuiga. Ni kwa sababu hii utawasikia wazazi wengi wakiringa kuwa waoto wao kwa mara zote huongoza darasa lao. Hakuna kitu kama mzazi bila doa. Kuwa tayari kusoma, na kuimarisha ulezi wako. Kutamfanya mwanao kuwa huru kutokana na shinikizo lisilo faa. Na mtoto wako pia atasoma kutoka kwa makosa hayo na unaweza soma mengi pia.

 • Usitie shaka sana

Dunia ni pahala pagumu na hakuna njia ya kujua iwapo watoto wako wako salama wanapokuwa mbali nawe. Baadhi ya wazazi huwa na shaka sana kwa wakati kama huu, ila, kumbuka wakati wote kutokuwa na shaka sana kwani hakufanyi wawe salama, unajinyima furaha unapo fanya hivi.

 • Epuka kuamini kuwa watoto wote ni sawa

Epuka kuamini kuwa watoto wote ni sawa kwani kila mtoto huwa na utu tofauti. Hata kama kuna maagizo yanayo aminika kuwa jumla, kama vile kumheshimu kila mtu na kuwa mwema. Jaribu kutengeneza maagizo kulingana na unavyo fikiria ni sawa kwa mtoto wako.

 • Usijaribu kuangalia ulicho fanya katika kila dakika

Unapaswa kuhisika sana katika maisha ya watoto wako ya kila siku, ila, jaribu kuhesabu ama kuangalia ulicho fanya kila dakika kwa sababu huenda ukavunjika moyo. Watoto huwa wabunifu wanapo boeka, kwa hivyo wanachukua jukumu wa wakati wao. Hakikisha umewapatia vitu wanavyo hitaji, kisha ujaribu kuwapatia nafasi wafanye vitu vyao.

mzazi mwenye furaha

 • Epuka kujitolea kufanya mambo yasiyo yenye afya

Kujitolea kufanya mambo yasiyo na afya huenda yakakufanya uchukie vitu kwa sababu utahisi kana kwamba kuwa mzazi kumekufanya ujinyime kuji eleza kadri ungependa. Kupuuza mahitaji yako kutawafunza wanao kufanya hivyo pia watakapo kuwa wazazi.

 • Epuka kuhisi kana kwamba una hatia

Kuwacha hisia za hatia zikuje akilini huenda kukakufanya uhisi kana kwamba hauna gharama kama mzazi. Wazazi kwa wakati mwingi huchukua majukumu yote mikononi mwao na kujilaumu pale ambapo wana jambo halija kamilika. Hisia chache za hatia unapo tazama kufanya mabadiliko, na kuendelea kujionea huruma kwa jambo hili sio jambo lenye afya. Hata ukifikiria kuwa ulimharibu mwanao kwa njia fulani, kuna wakati wa kufanya mabadiliko.

Kuna sehemu tofauti zinazo badilika katika ulezi, ila kuwachilia vitu tulivyo orodhesha hapo juu kutasaidia sana katika kukufanya mzazi mwenye furaha.

Soma Pia: My Idea Of What Nigerian Parenting Should Be

Chanzo: Fatherly

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio