Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Kupata Nafuu Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Yote Unayopaswa Kujua Kuhusu Kupata Nafuu Baada Ya Upasuaji Wa C-section

Approximately 3 out of 10 pregnancies in Singapore end up in c-sections. Arm yourself with knowledge to make the c-section recovery process a smooth and speedy one.

Safari ya kupata nafuu baada ya upasuji wa C-section sio jambo ambalo mtu huwa amekusudia. Mara nyingi huwa ata hujakadiria.

Unahisi uchungu na unaweza kudhani ni kubana. Unaweka mbegi yako tayari kuelekea hospitalini ukiwa na furaha na kuelekea kwenye wodi. Ratiba yako yote ya kuzaa iko tayari na huwezi kungojea kumshika mdogo wako.

Kwenye chumba cha leba, lisaa limoja linafuatia lingine na kabla ya kujua kuna mfuko wa oksijeni kwenye mapua yako na unakimbizwa kwenye chumba cha operesheni  kwa upasuaji wa dharura.

Hili halikuwa kwenye ratiba, hajui unachotarajia huko chumbani cha upasuaji, ata safari ya kupata nafuu baada ya upasuaji wa C-section. Niamini, hauko peke yako.

Kulingana na wizara ya afya, (MOH) takribani asilimia 30.5% ya waliojifungua kwote nchini Singapore huwa kupitia upasuaji.  Hizi takwimu zimeongezeka kwa miaka 15 hadi 20 iliyopita.

Aidha ni kwa vile kina mama ni ‘too posh to push’ ama kwa sababu za kimatibabu upasuaji umekuwa ukitumika sana. Kwa hilo, tunahitaji maarifa zaidi juu ya kupatanafuu baada ya upasuaji.

Kabla ya kuanza safari ya kupona baada ya upasuaji, hapa kuna maelezo juu ya unachotarajia wakati wa upasuaji.

Kujifungua ukitumia upasuaji wa C-section

Kujifungua kwa kutumia upasuaji pia inajulikana kama c-section.  Ni upasuaji wa hali ya juu unaohusisha kukata upande wa chini wa tumbo hadi kwenye uterasi. Upasuaji unafanyika kupitia kwa tabaka la tumbo na misuli ya tumbo inapanuliwa ili kufikia uterasi.

c-section recovery process

A c-section is a major surgery that cuts into the abdominal wall and pulls apart your muscles

Baada ya kumtoa mtoto na ule uzi wake, uterasi na palipo panuliwa hushonwa na sakafu za nyuzi.

Vile unavyoona, kuna mengi yanayoendelea. Kupona na kupata nafuu baada ya upasuaji bila shaka si jambo la haraka kama upasuaji wenyewe.

Walipokuwa wanakupeleka kwenye wodi, unahisi uchungu kidogo tu kwenye tumbo upande wa chini. Mikono yako iko kwenye upande na akilini mwako kumejaa maswali.  Nitaweza kukaa chini lini? Nitatembea lini? Nahisi kutapika, naweza kufanya hivyo? Je, nazo hizi nyuzi?

Msiwe na hofu kina mama. Safari ya kupata nafuu baada ya upasuaji wa C-section  ni wakati muhimu na unafaa kuwa mwangalifu. Lakini sio jambo kubwa kama linavyoonekana. Iwapo utafanya kile unafaa kufanya na uzingatie njia ulizopendekezwa, utapona kwa haraka sana. Nikiwa nimefanyiwa upasuaji kwa mara ya nne sasa, wacha nikuhakikishie sio jambo mbaya!

Daktari Ann Tan, Women Fertility and Fetal Centre, hospitali ya Mount Elizabeth ayajibu maswali ambayo huwa ya kawaida kwa kina mama juu ya kupata nafuu baada ya upasuaji wa C-section na pia anawapa vidokezo juu ya utunzi wa baadaye.

Daktari Tan alikuwa Mkuu wa Fetal Maternal Medicine katika upande wa maswala ya ukunga na kina mama katika hospitali ya Singapore General na kabla yake Rais wa Perinatal Society ya Singapore.

1. Kutembea Baada Ya Upasuaji?

Kwa vile c-section hujulikana kama upasuaji wa hali ya juu, usidhanie utaweza kutembea masaa machache baada ya upasuaji. Kupumzika ni jambo la umuhimu ili kuwezesha kidonda kupona. Wagonjwa hutakiwa kupumzika kwa kitanda kwa masaa katika ya 12 hadi 24 baada ya upasuaji.

Siku ya kwanza baada ya upasuaji ndio siku hufai kutembea sana. Ata kuna uwezekano hutafikiria kutembea ikitarajiwa utakavyokuwa unahisi baada ya upasuaji. Dawa za kutuliza maumivu zenye nguvu ziko mwilini mwako tayari. Ata kwa kutumia hizi dawa za kutuliza maumivu, kina mama uhisi kiwango tofauti cha uchungu ikilinganishwa na upana wa upasuaji.

Utakuwa umewekwa maji kuhakikisha kuwa una maji na mshipa wa kutoa mkojo kuhakikisha bofu lako halina mkojo. Na hilo ni la kushukuru. Hebu waza kutoka kwa kitanda kila wakati kati ya hayo maumivu yote.

Daktari Tan hupendekeza wagonjwa wake kutembea  siku inayofuatia baada ya upasuaji. Kutembea ni jambo la umuhimu kwenye safari ya kupata nafuu kwa vile huzuia deep venous thrombosis (DVT). DVT ni wakati damu huganda kwenye mishipa kwenye miguu.

Ata kama hutatembea kwa masaa 24 ya mwanzo, unaweza bado kutembea baadaye . Na upesi wa utakavyotembea, ndivyo tu wepesi mwili wako utarejea hali ya kawaida. Kutembea kwa urahisi kama vile kuzungumzusha miguu, kujinyoosha mikono na miguu na pia mazoezi ya kegel ni mwafaka kabisa.

2. Kukaa? Kusimama? Kutembea?

Kupata nafuu baada ya upasuaji wa C-section ni safari ya polepole. Unaweza anza kukaa chini baada ya masaa baada ya upasuaji. Ingawaje, lazima uwe mwangalifu ili kutotumia uti wako kukaa chini. Kumbuka, wameweza kukata tumbo la chini na kusabaratisha misuli yako.  Kwa hivyo ondoshea uti wako mzigo na utumie nguvu kutoka kwa misuli ingine.

c-section recovery process

Enjoy your lovely hospital room and don’t be in a hurry to venture out

Wauguzi na wakunga huwa tayari kusaidia na kukuelekeza katika safari yako ya kupata nafuu. Wataweza kukuonyesha jinsi unafaa kupinduka kwa upande, kupumzisha miguu kutoka kwa kitanda na polepole kuinua sehemu ya juu ya mwili wako ili kukuwezesha kukaa chini.

Pia hilo linahusisha kutoka kwa kitanda ili kusimama na kutembea kikamilifu. Unapoweka miguu yako kwenye sakafu kwa mara ya kwanza, usiwe na hofu iwapo utahisi kizunguzungu. Umekuwa umelala kwa kitanda kwa masaa 24 ukitumia dawa zenye nguvu!

Jambo la umuhimu kwenye safari ya kupata nafuu baada ya upasuaji ni kuwa mpole. Jishikilie kwenye upande wa kitanda ama kwa mtu mwingine ili akusaidie kutembea. Tafadhali usiwe shupavu na utembee ovyo ovyo kwenye wodi bila msaada. Najua vile inatamausha kwenda kwa ratili iliyo karibu nawe. Lakini tafadhali kina mama, kwa usalama wenu, ni bora kutembea kwa usaidizi kwa mara ya kwanza. Ili mradi tu!

3. Chakula ama kinywaji?

Kama kuna jambo ninalokumbuka kwa masaa ikikaribia upasuaji wangu, ni kuwa nilikuwa njaa. Muwe tayari kina mama, sehemu moja ya safari ya kupata nafuu ni kukaa bila chakula kwa wakati. Kulingana na hali yako, chakula kinaweza kuchelewesha  kati ya masaa machache hadi asubuhi siku inayaofuatia. Pia unaweza kuanzishwa kwa chakula laini ama kisicho kigumu kwa tumbo lako.

Sababu kuu ya hili ni kuzuia kutapika. Safari ya kupata nafuu baada ya upasuaji ni mahututi kwa siku za kwanza baada ya upasuaji nyizi zako bado zikuwa laini. Kutapika kunaweza kufanya nyuzi zako kutokana  na hilo kumaanisha shida kubwa.

Kwa hivyo tafadhali vumilia njaa kwa hizo siku. Usiwaulize ndugu na marafiki wako kupenyeza chakula mle ndani. Ni vyema kuzingatia kanuni . Inaweza kuonekana ngumu lakini kufuata kanuni mwanzoni  kutahakikisha kupata nafuu kwako baadaye kuko shwari na kwa wepesi.

4. Kuendesha gari?

c-section recovery process

You might want to stay away from the wheel for some time.

kina mama kutoka Singapore kwa kawaida huwa wenye shughuli nyingi. Mbaya pia kama huyu sio mtoto wako wa kwanza na unahitaji kusafirisha mtoto ama watoto wako walio wakubwa kwenda shule, darasa la densi ama kuogelea, sisi wote tunajua mpango. Ata kama unajihisi mwenye nguvu kuendesha gari, ni vyema kujiepusha kwa wiki za kwanza .

Sababu ni kuwa, unapoendesha gari, unaweza kutakikana kutumia breki za dharura kwa jambo ambalo halikutarajiwa. Kidonda chako kinafaa kuwa kimepona ili uweze kutumia hizi breki bila ya kujisababishia madhara.

Kina mama, iwapo ni lazima uwasafirishe watoto wako kwenda mahali, Kumbuka kuwa njia mbadala ni nyingi. Kwa kuongeza mchumba wako, kuna Grab car, Uber na bila shaka kuwapigia simu kampuni za wenye taxi. Jitoze kwenye safari ya kupata nafuu na uwe na hofu juu ya kuendesha gari baadaye!

5. Naweza kufanya shughuli za kufanya nitoe jasho?

Kweli, tunajua huwezi kungoja kuvalia hivyo viatu vya kukimbia na uweze kufanya mazoezi. Tunakusikia vizuri. Tunakuhisi. Ingawaje, kama tulivyosesma awali, safari ya kupata nafuu haifai kuharakishwa . Daktari Tan anasisitiza kuwa kanuni ya lazima ni kuanza mazoezi baada ya wiki sita. Na kuyapeleka mambo polepole na urahisi.

Kina mama wengi watarudi kwa uchunguzi baada ya wiki sita kwa daktari wa maswala ya kina mama juu ya upasuaji wake. Huu ndio wakati ataweza kuchunguzwa kidonda chake na jinsi anavyopata nafuu. Hili litaonyesha kama utaweza kuanzisha mazoezi yako.

Kwa huu wakati lakini, Daktari Tan apendekeza kufanya mazoei ya nyonga pindi tu unapojihisi unaanza kupata nafuu kutembea. Wakati mwafaka unaweza kuwa baada ya wiki moja ya upasuaji.

Ingawa kina mama huwa wanatizamia mazoezi ili kupunguza uzito, Daktari Tan anasisitiza kuwa wanafaa kuangazia kujenga nguvu ya uti  na ile ya nyonga. Hili linafaa kufanyika kabla ya kufikiria juu ya kukimbia.

 

nafuu baada ya upasuaji wa c-section

High impact exercise will have to wait for a bit.

“Uti na misuli ya nyonga iliweza kupanuka juu ya ujauzito na hizi lazima zirudi panapofaa ata kabla ya mazoezi ya hali ya juu” akasema Daktari Tan.

Tia akilini kuwa kila mtu hupona tofauti. Na pia kila mtu hupona tofauti kutoka kwa upasuaji mmoja hadi mwingine. Kadri ya mwezi mmoja baada ya upasuaji, nilikuwa nafanya mazoezi na nigeweza kutoshea kwenye nguo zangu za kabla ya ujauzito. Lakini siwezi sema hivyo juu ya upasuaji wangu wa nne.

Ata kama utakuwa huru kufanya mazoezi baada ya wiki sita, iwapo utahisi uchungu ama kuvuja damu kwa wingi baada ya kufanya mazoezi , tafadhali acha. Zingatia kupata nafuu kwanza na ufanye mazoezi tu baada ya mwili wako uko tayari.

Msiwe na hofu kina mama, iwapo una wasiwasi juu ya mwili wako baada ya kujifungua, mbinu moja huwa Spanx!

6. Kufanya mapenzi je?

Sawa, sasa vile mtoto tayari amewasili, wewe na mchumba wako mko tayari kufanya mapenzi tena. Lakini kuwa mvumilivu kwa kuwa safari yako ya kupata nafuu bado inaendelea. Wazo la Daktari Tan juu ya kufanya mapenzi ni kama lile la mazoezi.

“Mmoja anatumaini kuwa wachumba wako katika hali nzuri ya kiakili ili kufanya mapenzi baada ya wiki sita.”

Kukimbilia mapenzi baada ya wiki sita zinazohitajika ili kupata nafuu baada ya upasuaji ni wazo nzuri. Unajihatarisha na maambukizi na unaweza kusababisha ajali kwa nyuzi ambazo ziko kwenye safari ya kupona. Pia Kumbuka unaweza kuwa mjamzito hata kama mzunguko wako bado haujarudi.

Kwa wazo lingine, tafadhali zingatia mbinu ya kupanga uzazi utakayotumia inavyofanya kazi kwako. Hufai kuwa unapata mimba baada ya upasuaji.

7. Mtoto mwingine?

Swali linalofuatia bila shaka ni lini mtu anaweza kutarajia kupata mtoto mwingine? Vichwa juu, lazima utapata majibu mengi kwa hili swali.

Wakati mfupi kabisa wa kupata mimba baada ya upasuaji ni miezi sita asema daktari Tan. Lakini wakati unaopendekezwa kuwa sawa katikati ya mimba mbili imekadiriwa kuwa miezi 18 baada ya upasuaji wa kwanza hadi kupata mimba ya pili, akaongeza.

Kuweni wapole kina mama. Upe mwili wako wakati ili kupona. Siwezi tilia mkazo umuhimu wa nafasi ya kupata nafuu baada ya upasuaji bila ya kuharikishwa.

8. Masi baada ya kujifungua?

Kukandwa mwili baada ya kujifungua kunapata umaarufu. Kina mama wengi Singapore hujiapisha na hili ili kusaidia kupata nafuu kwa haraka na kuwasaidia kupunguza uzito.

Daktari Tan anasema kuwa mmoja anaweza furahia kukandwa baada ya upasuaji.

Ilihali tahadhari inafaa kuzingatiwa kina mama kwani kukandwa baada ya kujifungua huhusisha kukandwa tumbo la uzazi. Ni vyema kungoja hadi baada ya wiki sita baada ya uchunguzi. Iwapo daktari wako wa maswala ya kina mama atapendekeza basi unaweza kuendelea. Wengi wa wataalam wa andika huko Singapore hupendekeza ata baada ya wiki tatu baada ya upasuaji.

Yanayo Husika: Postnatal massage in Singapore: The comprehensive guide 

Vidokezo vya kupata nafuu

1.Lishe

Daktari Tan anapendekeza kula lishe lenye protini na mafuta ili kupona vizuri. Anaelezea kuwa madini Zinc na Vitamini C ni virutubisho vinavyosaidia na kurekebisha tishu mwilini.

Daktari wengine wanaweza amurisha Vitamini E kusaidia baada ya upasuaji.  Virutubisho vyovyote utakavyoamrishwa tafadhali vitumie!  Pia, ni bora kujiepusha na chakula cha ziwa kwa huu wakati.

2. Utunzi wa nyuzi zilizoshonwa

Wakati uko kwenye hospitali, wauguzi wataosha kile kidonda na dawa kwa kila siku. Utaweza kuelekezwa nyumbani na kitambaa ambacho hupaweka mahali pale pakavu.  Mara nyingi hii huwa plasta spesheli ambayo huzuia maji isiguze kile kidonda. Hufai kuwa unapaka sabuni kwa kile kidonda kwa huu wakati.

Kati ya siku saba hadi kumi baada ya upasuaji zile nyuzi zitatolewa. Daktari wako ataamurisha collagen cream ama geli nyingine ya kupaka pale ili kuzuia keloids kuumbika. Hii pia husaidia kupona kwa upande wa nje wa kidonda.

Baada ya kutolewa kwa nyuzi, unaweza kuoga na kupitisha maji ama sabuni juu ya mahali pale. Ingawaje, kuwa makini usisukume kile kidonda. Nyakati za mwanzoni  za kupata nafuu ni vyema kutotumia maji iliyo moto sana.

3.  Mjalidi wa upasuaji

Siku baada ya upasuaji, daktari wako atakuamrisha kuweka mjalidi. Hii ni ya kusaidia kwenye safari yako ya kupata nafuu. Kwanza, hutoa msaada mzuri na huzuia mwendo sana. Iwapo utahitaji kukohoa, hii husaidia sana.

Kubana kwa ule mjalidi kunakupa uhakika kuwa kile kidonda hakitafunguka ama kulipuka. Kwa kuongeza, ule mjalidi husaidia kufanya ngumu ngozi na kuzuia tumbo kwa kuniginia. Ule mkazo wa mjalidi,  hutulia kwa kile kidonda  na hupunguza kufanyika kwa alama kwenye tishu.

Kwa kumalizia juu ya kupona baada ya upasuaji, haya ndio daktari Tan anayo kwa kina mama.

Kuwa mtulivu.  Mtoto alichukua miezi tisa kukua na kuumbika ndani yako. Misuli yako imenyooka. Ingawaje, upasuaji huonekana kama mtoto wako alitoka ndani ya mfuko, haina uhakika kuwa misuli yako itarejea kwa upesi. Hapana, halifanyiki hivyo.

Huchukua wakati kupona. Safari ya kupata nafuu huwa ya polepole. Kwa hivyo kuwa makini. Chukua muda kupona na kufanya mazoezi hadi kurejea ulipokuwa kabla ya ujauzito.

 

Soma piaEverything you need to know about postnatal care

Hakikisha una iangalia tovuti ya  Africa Parent’s Community kwa hadithi zingine nyingi za kujuza, maswali na majibu kutoka kwa wazazi na wataalum. Iwapo una maswali, maarifa ama ujumbe mfupi, tafadhali tujulishe kwa kuwacha maoni yako kwenye visanduku vya maoni hapa chini.

Makala haya yamechapishwa tena na idhini ya Asianparentkisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Written by

Risper Nyakio