Je, Kuna Nambari Ya C-sections Ambazo Mama Hawezi Pitisha?

Je, ushai jiuliza nambari ya C-sections ambazo mama anaweza pata?
Siku hizi, visa vya upasuaji wa C-section kama njia ya kujifungua vinaongezeka huku baadhi ya wamama waki amua kuenda njia ya upasuaji wa C-section badala ya kujifungua kwa njia asili. Kwa hivyo, ni nambari gani ya upasuaji wa c-sections ambayo mama anaweza pata iliyo salama?
Na kwa mama ambaye mtoto wake wa kwanza alizaliwa kupitia kwa upasuaji wa C-section, kuna nafasi za asilimia 90 kuwa mtoto wa pili atazaliwa kupitia C-section.
Nambari ya Upasuaji wa C-sections iliyo salama kwa mama?
Kwa sehemu kubwa, hakuna jibu shwari ikifika ni mara ngapi zilizo salama kwa mama kushuhudia upasuaji wa C-section.
Walakini, madaktari wanakubaliana kuwa kadri mama anavyo shuhudia mara nyingi za upasuaji wa C-section ndivyo anavyokuwa katika hatari kubwa.
Daktari Marra Francis anasema, “Upasuaji wa C-section mara moja ama mbili hauna hatari kubwa kwa mama na mtoto.” Kwa kuongeza, Mayo Health Clinic ilisema kuwa hatari zinaongezeka baada ya upasuaji wa mara ya tatu wa C-section, ila hakuna nambari salama za upasuaji wa C-section.
Hatari ni zipi?
Hapa ni hatari zinazo husika na C-section nyingi:
- Kupata alama – kila mara unapo pitia upasuaji wa C-section, kutakuwa na alama nje ya mwili na ndani. Kuwa na alama hizi nyingi huenda kukafanya upasuaji wa C-section ujao kuwa na matatizo.
- Matatizo na placenta yako – baada ya C-setion nyingi, placenta yako huenda baadhi ya wakati ikaji shikilia kwenye uterasi yako ama baadhi hata kufunika mlango wa kizazi chako.
- Majeraha ya kibofu na tumbo – Wakati ambapo sio jambo linalo shuhudiwa mara kwa mara, haya hutokea na C-sections nyingi.
- Kuvunja damu nyingi – kutoa damu nyingi ni hatari inayo kuja na C-sections na nambari inavyo zidi kuongezeka, ndivyo hatari ya kuvunja damu nyingi inavyo ibuka. Katika baadhi ya visa, uterasi huenda ikatolewa, utaratibu unao julikana kama hysterectomy.

Midsection of pregnant Black woman holding belly
Katika mwisho wa siku, ni muhimu kuongea na daktari wako na kutumia ushauri wao, utafanya uamuzi iwapo ungetaka kuwa na C-section ama kujifungua kwa njia asili. Kwa njia hiyo, unaweza pima hiari zako na uamue ni ipi bora kwako na kwa mtoto wako.
*Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza katika kurasa la theAsianparent Philippines na kuchapishwa tena katika kurasa ya the Africanparent na kisha kutafsiriwa na Risper Nyakio.
Chanzo: familyshare.com
Soma: Finally, A Way To Heal Your C-Section Cut Without A Scar!.