Njia Tofauti Za Kupima Mimba

Njia Tofauti Za Kupima Mimba

Vipimo vya mimba, njia unazo weza kudhibitisha iwapo una mimba ama la.

Iwapo una shuku kuwa una mimba ama ungependa kutunga mimba. Makala haya yana angazia baadhi ya namna ya kupima mimba.

Namna za kupima mimba

Namna ya kupima mimba: Vipimo vya mimba

Unaweza jua iwapo una mimba kwa kugundua mojawapo ya ishara maarufu za mimba. Iwapo una shuhudia ishara yoyote ya mimba, unapaswa kuchukua kipimo cha nyumbani ama kumtembelea daktari ili adhibitishe iwapo una mimba ama la.

namna ya kupima mimba

Vipimo vya nyumbani

Kipimo cha nyumbani kinaweza tumika na kuwa na matokeo sawa siku moja baada ya kukosa kipindi chako cha hedhi. Ila ni vyema zaidi kungoja wiki moja kabla ya kupima mimba. Kipimo hiki hugundua kuwepo kwa homoni ya HCG kwenye mkojo. Homoni hii inapatikana pale tu unapokuwa na mimba. Kemikali inayo kuwa kwa kijiti cha kupima mimba hubadilika rangi ikiwa mkojo wako una homoni ile. Wakati wa kungoja huwa karibu dakika kumi. Ili kuhakikisha kuwa kipimo ni cha kweli, ni vyema zaidi kuchukua kipimo kile mara mbili.

Kipimo cha mkojo cha kliniki/zahanati

Iwapo hutaki kufanya kipimo kile peke yako, unaweza mtembelea daktari wako atakaye chukua kipimo kile. Faida za kufanya hivi ni kuwa daktari wako ataweza kudhibitisha iwapo kuna madoa kwa kipimo kile na matokeo yatakuwa sawa zaidi. Matokeo pia yatakuwa tofauti kwa kila kliniki na muda wa kungoja huenda ukawa hadi siku saba baada ya kuchukua kipimo kile.

namna ya kupima mimba

Kipimo cha damu

Kipimo hiki kinafanyika hospitalini. Kipimo cha maabara cha damu yako kinafanyika ili kugundua kuwepo kwa HCG. Kipimo hiki kina dhibitisha iwapo mwili wako unatoa homoni ya HCG na pia kiwango cha HCG kinacho tolewa mwilini iwapo una mimba.

Kipimo cha pili kina onyesha muda ambao umekuwa na mimba iwapo hauna uhakika kuhusu wakati ambao ulitunga mimba.

Ishara za mapema za mimba

Pia kuna baadhi ya ishara za kuangazia kujua iwapo una mimba. Ishara hizi ni kama vile:

  • Kukosa kipindi chako cha hedhi
  • Kuhisi kutapika
  • Kutapika
  • Chuchu zilizo fura
  • Kuenda msalani mara kwa mara
  • Kuhisi kuchoka

Written by

Risper Nyakio