Je, Ni Vyema Kwa Mama Kumwamsha Mtoto Ili Amlishe?

Je, Ni Vyema Kwa Mama Kumwamsha Mtoto Ili Amlishe?

Ni kawaida kwa wazazi wa mara ya kwanza kushangaa ikiwa wanapaswa kuwaamsha watoto ili wawalishe. Makala haya yana kuelimisha zaidi kuhusu mitindo ya kula ya watoto yenye afya.

Wazazi wengi wa mara ya kwanza huwa na hadithi nyingi za kuwaamsha watoto wao ili wanyonye. Mzazi mmoja alikiri kuwasha sitima za chumba cha mtoto wake usiku wa maanani ili aamke amlishe. Mzazi huyu alisukumwa na uwoga wa ndani wa kuishi kwa mtoto wake. Na swali la, je, napaswa kumwamsha mtoto ale usiku?

Kama mama mmoja alivyo sema, "kila mara nilipo fikiria, je, napaswa kumwamsha mtoto wangu ale, nilikuwa na hofu sana. Singependa mtoto wangu ahisi njaa hadi afe."

Mitindo Ya Kumlisha Mtoto Mchanga: Je, Napaswa Kumwamsha Mtoto Ale Usiku?

napaswa kumwamsha mtoto ale usiku

Ikiwa una shangaa ama ni jambo la busara kumwamsha mtoto wako ili umlishe, huenda ukawa na fikira nyingi kuhusu usingizi wenye afya na mitindo ya kula ya mtoto mchanga.

Kati kati ya uchovu wote, wazazi wa mara ya kwanza huenda wakashangaa ikiwa wana fanya jambo la busara kwa kumwacha mtoto alale kwa kipindi kirefu ama kukatiza usingizi wao. Wanaelewa kuwa mtoto hupunguza uzito wa mwili siku za kwanza chache baada ya kuzaliwa na ni muhimu kumlisha mtoto mara kwa mara -  hadi mtindo wake wa kuongeza uzito uwe dhabiti.

Wataalum wengi hushauri wazazi kuwalisha wanapo dai. Ahirisha kumfunza kulala hadi mtoto anapo fikisha ama kupitisha hatua ya uzito wa kuzaliwa.

Jinsi ya kumsaidia mtoto kubadilisha

Watoto huwa na fikra ndogo ama kukosa fikra yoyote ya mchana na usiku. Katika siku za kwanza chache za kuzaliwa, watoto wengi hutumia wakati wao kula na kulala.

Walakini, wazazi wanaweza wafunza watoto wao tofauti ya usiku na mchana.

Je, Ni Vyema Kwa Mama Kumwamsha Mtoto Ili Amlishe?

"Jaribu kucheza na mtoto wako mchana. Na uanzishe utaratibu mtulivu wa wakati wa kulala kama usiku; usio kuwa na vitu vya kumfanya afungue macho," alisema Dorothy Isiguzo, ambaye ni mtaalum wa afya ya watoto. Aki ongea kuhusu swali la iwapo napaswa kumwamsha mtoto ale.

Mhimize mtoto wako kula mara kwa mara kabla ya wakati wa kulala. Watoto wanapo enda kulala wakiwa wameshiba, wana nafasi chache za kuamka mara kwa mara kula usiku.

Jinsi ya kudhibiti mwingiliano wa usiku na mtoto wako

Mtoto wako anapo fikisha hatua ya kuongeza uzito, una shauriwa kupunguza muingiliano wa wakati wa usiku na mtoto wako. Wazo ni kumsaidia mtoto kukuza uhuru.

Watoto wachanga hulala usingizi mzito wakilishwa vyema na hawana mkojo.

"Watoto ni viumbe wa uzoefu," alisema daktari Tari Fafunwa, ambaye ni mwana saikolojia wa watoto katika hospitali kuu ya Edo huko Benin. "Mpe aina yote ya starehe inayo hitajika. Lakini ufanye hivi kwa vipimo. Mlishe mtoto wako na umshike kwa muda. Lakini wakubalishe wajitulize hadi walale."

Kuwa na imani katika uwezo wa mtoto wako wa kutulia baada ya jua kucha ili akili zao zianze kujitayarisha kulala. Na wakati, utagundua kuwa mtoto wako atapunguza mwingiliano wa wakati wa usiku na hautuliza swali la iwapo ni sawa kumwamsha mtoto wako kula usiku.

Unaweza msaidia mtoto wako kulala usiku

Ikiwa mtoto wako huwa na uraibu wa kulala mchana wote na kuamka usiku, hauko peke yako. Wazazi wengi hushuhudia tatizo hili la usiku mrefu na watoto wachanga. Hapa kuna vidokezo vichache vya kumsaidia mtoto wako kulala vyema usiku.

  1. Ongeza muingiliano wa mchana kwenye ratiba yako ya mchana

Licha ya kuwa na ratiba isiyo na wakati wa mapumziko, tafuta wakati wa kuchechemua akili ya mtoto wako kwa kuongea, kucheza na kuimba. Baada ya kulala kwa masaa mawili, unapaswa kumwamsha mtoto wako ale. Mtoto wako akiamka kwa kipindi cha kutosha mchana, kuna nafasi kubwa za kulala vyema usiku. Ikiwa mtoto mdogo ana pumzika mchana wote na kulala, ataamka usiku.

2. Tumia mbinu nzuri za kufariji 

napaswa kumwamsha mtoto ale usiku

Wazazi wengi hawafahamu mbinu za kufariji zinazo fanya kazi kwa watoto wao. Zima sitima na umpe mtoto wako masi nyepesi na umwimbie nyimbo za kumtuliza. Dhibiti wakati wako uwe dakika 15. Matendo haya ya kuliwaza yana weza msaidia mtoto kulala. Lakini lazima uwe na mwongozo kabambe wa mambo haya ili mtoto wako asisitize umwimbie usiku wote.

Uthabiti ni muhimu

Wataalum wa usingizi mara nyingi huongea kuhusu umuhimu wa kuzingatia mtindo wenye afya wa kulala. "Enda kulala wakati maalum na uamke wakati maalum na mwili wako uta jenga saa yake ya undani. Na ni sawa kwa watoto pia," yuasema daktari Debbie Ake, mtaalum wa usingizi katika kituo cha afya cha Abuja.

Kuwa na uthabiti unapo msaidia mtoto wako kutengeneza mtindo wenye afya wa kulala na kula. Ikiwa lazima ufanye mabadiliko machache kwa mtindo wao wa kulala na wa kula, anza mapema ili usi ulize swali la je, napaswa kumwamsha mtoto ale usiku? Nyote, wewe na mtoto wako mnapaswa kuwa mme lala vyema usiku, kwa hivyo, kuwa na uthabiti katika kumsaidia mtoto wako kuwa na mtindo wa kulala wenye afya.

Ikiwa mtoto wako ana mahitaji spesheli, kwa mfano, mtoto wako alizaliwa kama haja komaa vyema ama mtoto wako ana matatizo ya ukuaji, masharti huenda yaka badilika. Ni vyema kwako kuwa una zungumza na daktari wake na kuuliza maswali yote muhimu. Je, napaswa kumwamsha mtoto ale usiku?  Pata ushauri wa kitaalum na utumie vidokezo tulivyo angazia kwenye makala haya. Ili kumsaidia mtoto wako kuwa na mtindo wenye afya wa kula na kulala.

Chanzo: Standfordchildrens.org

Soma Pia:Kwa Nini Watoto Hukoroma

Written by

Risper Nyakio