Koma Kuwaambia Wasichana Kuwa Ndoa Ni Tuzo Kwa Kuwa Na Tabia Nzuri

Koma Kuwaambia Wasichana Kuwa Ndoa Ni Tuzo Kwa Kuwa Na Tabia Nzuri

Wakati ambapo tabia nzuri zinaweza wavutia wanaume kwako, hazikuletei bwana hivyo tu. Wazazi wengi wa ki Afrika wana weka ndoa kwenye kitengo cha kitu unacho fanyia kazi, unacho stahili, kama umekuwa mtoto mzuri, binti mwenye tabia nzuri. Huenda ikawa ni kwa sababu hawajui vyema ama kwa sababu jambo hilo liko kwa mwongozo wa kuwalea watoto ambao wao pekee wanafahamu. Wavyele hawa huwapatia mabinti ushauri na mitindo ya kitabia ya kuiga ili wapendeze kuolewa, na kusahau kuwa ndoa si tuzo la tabia nzuri.

Sababu Kwa Nini Ndoa Si Tuzo La Tabia Nzuri

ndoa si tuzo la tabia nzuri

Ikiwa umekuwa katika familia ya kiafrika, nafasi kubwa ni kuwa umesikia mojawapo ama wazazi wote wawili wakimwambia ndugu yako wa kike kuwa tabia fulani hazitakubalika katika nyumba ya bwanako. Kauli hii na zingine huwa na lengo la kurekebisha tabia za binti huyo na kumweka katika njia ya kuwa na tabia nzuri, kujitenga na tabia fulani na kuwa mwanamke anayefaa kuolewa. Lazima uwe na tabia nzuri kama binti ili upate mtu wa kukuoa, walisema.

Watu wamekua na kuamini kauli hizi maishani mwao mote, kwa hivyo inapaswa kusemwa kuwa ndoa sio tuzo la tabia nzuri zinazo sisitizwa kwa wasichana katika umri mchanga.

Wakati ambapo sio mbaya kwa njia yoyote kuwa wazazi wetu waliwafunza watoto kuwa na tabia nzuri, kumwogopa Mungu na mambo mengine ambayo wazazi wa kiafrika huwasisitizia watoto wao, rekodi inapaswa kutengenezwa kwa jambo hili na hivi ndivyo watu maalum kwenye mtandao kama Jola Sotubo wanavyo sisitiza.

Jola ni mwandishi wa kitabu 'Barua kwa mpenzi wangu wa kale,' kitabu kuhusu kupata mapenzi, mwangaza na kuangazia aina zote za uchungu baada ya kuwachwa na mpenzi wako na fikira nyingi mnapo achana.

Ali andika kwenye kurasa yake ya mtandao wa Instagram na kusema:

"Nasikia watu wakiulia "Kwa nini wasichana wabaya wanaolewa kwa urahisi na kwa mbio kuliko wasichana wazuri? Kuna haja ya kubaki bikira?" Swali langu ni "Je, ulikuwa mzuri kwa nani?"

Je, ubikira ni jambo la kuwa na mjadala kuonyesha mwanamme kuwa una thamani? Pole, lakini wanaume hawa wachagui mabikira kwenye foleni ya wana vijiji. Chochote unacho kifanya, kifanye kwa sababu una amini kuwa ni wazo bora. Sio kwa sababu mtu alikwambia uta faulu katika ndoa. Watu hupendana na kuingia katika ndoa hata wakiwa na madoa na dhidi ya imani za watu. Tabia nzuri zina tarajiwa kutoka kwa kila mtu.

Soma Pia :Mambo Ya Kufanya Mapenzi Yanapo Isha Katika Ndoa

 

Written by

Risper Nyakio