Kwa Nini Nina Ndoto Mbaya Wakati Wa Mimba

Kwa Nini Nina Ndoto Mbaya Wakati Wa Mimba

Katika mwanzo wa uajuzito, ndoto huwa kuhusu kutunga mimba. Mara nyingi huja kama sitiari, kama vile samaki kujipandikiza kwenye mto.

Kuwa na mtoto bila shaka kuta athiri mitindo yako ya kulala. Utakuwa macho wakati tofauti ukijihisi mgonjwa, kukosa starehe ama hata kuhisi njaa. Unapokuwa mjamzito, mwili wako hushuhudia mabadiliko mengi na utapata kuwa huenda ukalala sana ama hata kukosa kulala. Na mtindo huu utaendelea hata baada ya kujifungua. Mtindo wako wa kulala uta athiriwa sana. Ni muhimu kufahamu kuwa ni kawaida kuwa na ndoto mbaya wakati wa mimba.

Kwa sababu mtindo wako wa kulala hau ambatani na hapo awali. Uta kanganywa, kufilisika kimawazo na hisia zako. Tutakueleza utakayo yafanya kukusaidia kukabiliana na hili. Kwa sasa, elewa kuwa mtindo wako wa kulala sio wenye afya unapokuwa na mimba na muda mfupi baada yake.

Baadhi ya Ndoto Mbaya Maarufu Wakati Wa Mimba Na Maana Zake

ndoto mbaya wakati wa mimba

  • Ndoto kuhusu maji

Kuota kuhusu maji ni kawaida unapokuwa na mimba ama la. Lakini unapokuwa umebeba mtoto, ndoto hizi huenda zikawa wazi zaidi. Na zenye maana tofauti kulingana na umbali wa safari yako ya mimba.

Wazo la mvua, mito na bahari huwa maarufu katika mwanzo wa ujauzito, wakati ambapo mafuriko huonekana sana katika trimesta ya mwisho. Mvua ni ishara ya kusafishwa, na huashiria mwanzo mpya, maisha mapya wakati ambapo mafuriko huashiria maji yako kuvuja na kuanza kwa safari ya kujifungua.

  • Ndoto kuhusu jinsia ya mtoto

Ndoto sio mipira ya crystal ya kumweleza mwanamke jinsia ya mtoto anaye tarajia. Kuota kuhusu ngono kuna onyesha kuwa unafikiria sana kuhusu masuala ya jinsia. Watu wanataka jinsia fulani, kwa hivyo ina ashiria matakwa yako hata kama huenda ukakosa kugundua.

  • Ndoto kuhusu kutunga mimba

Katika mwanzo wa uajuzito, ndoto huwa kuhusu kutunga mimba. Mara nyingi huja kama sitiari, kama vile samaki kujipandikiza kwenye mto. Katika trimesta ya kwanza, watoto huashiriwa na wanyama wadogo wanao kua katika mimba kuwa wanyama wakubwa.

  • Ndoto kuhusu kumsahau mtoto wako

Ikiwa una ota kuhusu kumwacha mtoto wako mahali, usiwe na shaka. Hii ni kawaida katika trimesta ya kwanza. Kuhisi kuwa hauko tayari ama hauwajibiki vya kutosha kuwa mama bado. Usiwe na shaka, kila mama mpya ata hisi hivyo. Na mambo yote yatakuwa shwari mtoto anapo fika.

Ndoto mbaya kuhusu hatari za kifizikia kwako ama mtoto wako

Ndoto na maana yake. Yeyote anaye pitia kipindi cha kuto kuwa na uhakika, uwoga ama mabadiliko anaweza kuwa na ndoto mbaya. Lakini ndoto zisizo pendeza huchukua mtindo tofauti katika mimba. Wanawake huota kuhusu maisha yao ama ya watoto wao yakiwa hatarini.

Sababu za ndoto mbaya wakati wa mimba

ndoto mbaya wakati wa mimba

Kama tulivyo angazia hapo juu, mwili wako unapitia mabadiliko mengi wakati wa ujauzito. Na hali yako ya kifizikia, hisia na kiakili zinahusika. Wakati ambapo ndoto za mimba hubaki chanzo kisicho eleweka katika nyanja nyingi za kisayansi, kuna sababu nyingi kwa nini mzunguko huu wa ndoto hutendeka.

Sababu moja ni kufuatia ongezeko katika utoaji wa homoni mwilini. Utapata kuwa, wakati wa mimba, homoni zako huenda zika athiri hisia zako na wasiwasi. Pia zita athiri njia ambayo ubongo wako una chakata ujumbe na hisia na kusababisha ndoto zilizo wazi zaidi katika ujauzito.

Sababu nyingine ni ya kuathiriwa kwa mtindo wako wa kulala wa kawaida. Unapo shindwa kuweka ratiba ya kulala iliyo sawa ama unapo amka mara nyingi usiku kufuatia kutokuwa sawa ama haja ya kuenda msalani, huku kuta athiri REM sleep (rapid eye movement). Ndoto zako hutendeka katika kipindi hiki. Kwa hivyo kinapo athiriwa, huenda kikathiri jinsi unavyo ota ukiwa mjamzito.

Jinsi ya kuimarisha usingizi wako

Ikiwa una tatizika na ndoto mbaya wakati wa mimba na ungependa suluhu za mbio za kuimarisha usingizi wako, una hiari nyingi. Kwanza, hakikisha kuwa una jaribu kulala na kuamka karibu wakati sawa. Ama unaweza jaribu haya:

  • Kusikiliza soundwaves: sikiza hizi kabla ya kuenda kulala na utapata kuwa unasinzia kwa usingizi mzito, bila ndoto mbaya.
  • Mishumaa ya mwezi: Jaribu kuweka mishumaa ya digitali kwenye chumba chako. Utahisi umepumzika zaidi na uko tayari kulala, kwa njia hii, hutapata ndoto mbaya.

Soma Pia:Lishe Ya Ujauzito: Ratiba Ya Chakula Cha Ujauzito Cha Nigeria

Written by

Risper Nyakio