Mama Anapaswa Kungoja Muda Upi Kufanya Ngono Baada Ya Kujifungua?

Mama Anapaswa Kungoja Muda Upi Kufanya Ngono Baada Ya Kujifungua?

Kufanya mapenzi na mwenzio ni salama baada ya kupona kwa kidonda baada ya kujifungua na unapo hisi kuwa tishu za uke wako zimepona.

Ni kawaida kwa mama na mwenzi wake kushangaa iwapo ni salama kufanya ngono baada ya kujifungua na wakiwa na mimba. Ngono mama akiwa na mimba ina athari zipi? Ina mwumiza mama na mtoto ana ni salama? Kuna mitindo hasa ambayo mnafaa kuzingatia katika kipindi hiki ama mitindo yote ya ngono ni salama? Soma makala haya kupata maarifa unayo tafuta.

Kufanya ngono katika mimba ni salama?

kufanya ngono baada ya kujifungua

Ngono ni asili na kitu cha kawaida hata katika mimba, ikiwa mimba yako haina matatizo yoyote. Kufanya ngono katika kipindi hiki hakuta muathiri mtoto. Kwani analindwa na gunia la amniotic, kuta za uterasi na tumbo yako, kwa hivyo bila shaka ako salama kabisa.

Katika miezi ya kwanza, una shauriwa kufanya ngono kama ilivyo kawaida yenu, japo mimba inavyo zidi kukua, ni vyema kutumia mitindo ambayo mama ana starehe. Wiki za mwisho kabla ya kujifungua, ni vyema kuepuka kufanya mapenzi. Wataalum wana amini kuwa manii yana homoni maarufu kama prostaglandins ambazo zinaweza  fanya mama aanze kushuhudia kubanwa.

Wakati ambapo sio salama kwa mama mjamzito kufanya ngono

matamanio ya kingono

Kuna visa ambavyo daktari ama mkunga wako anaweza kushauri kutofanya ngono. Ikiwa una mojawapo ya mimba hii ya hatari:

 • Uko katika hatari ya kupoteza mimba ama kuharibika kwa mimba kufuatia kupoteza mimba hapo awali
 • Hatari ya uchungu wa uzazi usio komaa (mara nyingi katika wiki 37)
 • Una tatizo la kuvuja damu, uchafu wa ute, kuumwa na tumbo bila sababu hasa
 • Kutoboka kwa utando ama kwa gunia la amniotic
 • Kizazi chako kufunguka mapema sana katika mimba
 • Placenta yako kuwa chini sana katika uterasi
 • Kutarajia watoto zaidi ya mmoja

Ngono katika mimba

Ushuhuda wa kila mwanamke katika mimba huwa tofauti, hata jinsi wanavyo ifurahia ngono. Kuna wanawake wasio kuwa na hamu ya kufanya ngono katika ujauzito. Huku wengine waki shuhudia hamu iliyo ongezeka ya ngono.

Unapokuwa na mimba, ni kawaida kwa hamu ya ngono kuja na kuisha jinsi mwili wako unavyo badilika. Huenda ukaanza kuwa makini na tumbo yako inayo zidi kukua, ama ukapata ujasiri zaidi na chuchu zilizo jaa. Ni vyema kuongea na mwenzi wako na kumweleza kinacho kusisimua na kukufurahisha. Katika wakati huu, mnapaswa kuwa makini na mitindo ya ngono iliyo salama na iliyo na starehe kwa mama. Kuwa makini pia na kama una shuku historia ya afya ya mwenzio, tumia kondomu kwani maambukizi katika mimba ni hatari. Yanaweza sababisha kupoteza mimba ama kumwathiri mwanao.

Kufanya ngono baada ya kujifungua

kufanya ngono baada ya kujifungua

Wiki za kwanza sita baada ya kujifungua zinajulikana kama kipindi baada ya kujifungua. Ngono katika kipindi hiki ni jambo la mwisho akilini mwako. Sababu zinazo fanya hamu yako ya kufanya mapenzi kudidimia katika kipindi hiki ni kama vile:

 • Kupona baada ya kujifungua kwa njia ya kupitia uke
 • Kupona kutokana na kushonwa baada ya kupata mtoto kupitia upasuaji wa C-section
 • Kuvuja damu baada ya kujifungua ambako ni kawaida, kwa wiki za kwanza nne hadi sita
 • Uchovu baada ya mimba na mchakato wa kujifungua
 • Mahitaji ya mtoto wako, na kumtunza hasa kwa mama wa mara ya kwanza
 • Kubadilika kwa viwango vya homoni
 • Kuumwa na chuchu kufuatia kumnyonyesha mtoto
 • Fikira nyingi baada ya kujifungua ama matatizo ya kihisia

Kufanya mapenzi na mwenzio ni salama baada ya kupona kwa kidonda baada ya kujifungua na unapo hisi kuwa tishu za uke wako zimepona. Ila usiwe na kasi kwani kupona huku kutachukua wiki nyingi. Wasiliana na daktari wako akushauri wakati salama wa kufanya ngono baada ya kujifungua.

Soma PiaIshara 7 Katika Mimba Zinazo Ashiria Kuwa Kuna Hatari

Written by

Risper Nyakio