Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

Mitindo 5 Ya Ngono Ya Kuepuka Baada Ya Upasuaji Wa C-Section!

wanawake walio jifungua kupitia upasuaji wa C-section wana mambo mengine ya kuwa na wasiwasi kuhusu: uchungu wakati wa ngono baada ya upasuaji wa C-section.

Wazo la kufanya mapenzi baada ya kujifungua huwatia wanawake wengi kiwewe, huku likawa wazo la mwisho vichwani mwa wengi. Haijalishi walivyo jifungua, kuna matatizo mengi ya kukumbana nayo: mwili ulivyo, uchovu wa kifizikia, chuchu zinazo toa maziwa na kukosa hamu ya kufanya ngono. Walakini, wanawake walio jifungua kupitia upasuaji wa C-section wana mambo mengine ya kuwa na wasiwasi kuhusu: uchungu wakati wa ngono baada ya upasuaji wa C-section.

Wamepitia upasuaji mkubwa na katika hatua moja maishani mwao, wata rejelea kufanya ngono na wanapo rejea, unastahili kujua mitindo ya ngono isiyo na uchungu kwa wanawake walio jifungua kupitia upasuaji wa c-section. Na mitindo unayo stahili kujitenga nayo. Tuna kuelimisha haya yote.

Unapaswa kungoja muda upi kabla ya kufanya mapenzi

ngono baada ya upasuaji wa C-section

Wakati ambapo ni vizuri wakati wote kuwasiliana na daktari wako kuhusu wakati bora wa kurejelea kufanya mapenzi baada ya upasuaji wa c-section, wiki sita kwa jumla ndiyo wakati unao kubalika.

Katika mwaka wa 2013, somo la wanawake zaidi ya 1,500 liligundua kuwa asilimia 53 yao walikuwa wamejaribu kurejelea ngono na wachumba wao baada ya wiki sita. Kwa kusema hayo, kila mwanamke ni tofauti na muda wao wa kupona  baada ya CS utakua tofauti. Walakini ukiwa tayari, epuka kufanya tendo la ndoa kwa mitindo hii.

Mitindo ya ngono baada ya upasuaji wa c-section unayo paswa kuepuka

ngono baada ya upasuaji wa C-section

Baadhi ya mitindo huenda ika sababisha kuhisi uchungu wakati wa tendo la ndoa baada  ya c-section, kwa hivyo epuka mitindo hii hadi upone.

  1. Missionary

Huu ni mtindo wa asili ambapo mwanamme ako juu ya mwanamke. Mtindo huu unaweza shinikiza tumbo yako na kidonda.

2. Cowgirl

Tofauti na mtindo wa reverse cowgirl, ambapo wanawake huwa na dhibiti zaidi, mtindo huu wa kiasili wa cowgirl huwa na sehemu yako ya pelviki ikisukuma chini na kwa nguvu zaidi. Na kushinikiza sehemu yako ya tumbo. Epuka mtindo huu hadi upone.

3. Ngono ya kusimama

Kuna shinikizo nyingi kwenye sehemu yako ya tumbo. Badala yake, geuka na ujaribu mtindo wa doggy ukiwa ume simama.

4. Doggy style

Mtindo huu una shinikiza tumbo ya chini na sehemu ya pelviki. Jitenge nayo kwa muda.

5. Kushinikiza tumbo yako

Jaribu mtindo huu baada ya kidonda chako kupona kabisa. Kufanya mtindo huu kabla ya kidonda kupona kutafanya uanze kutoa damu katika sehemu hiyo.

Chanzo: Ob-gyn Women's Centre, Women's Health

Soma Pia: Jinsi Ya Kujitayarisha Usiku Kabla Ya Upasuaji Wa C-Section

Written by

Risper Nyakio