Swali la, ngono kwa kawaida hudumu muda upi huwa kawaida hasa kwa watu walio hai katika kufanya mapenzi. Kufanya mapenzi ni zaidi ya kuingiza kibofu kwenye uke wa mwanamke. Kitendo cha mapenzi huwa zaidi, muda kabla ya kitendo hiki na baada. Lakini kwa leo, tuna angazia kitendo hiki pekee. Kupima muda hasa wa kitendo hiki sio rahisi. Na je, kuwauliza watu muda wanaochukua? Hakuna uhakika kuwa majibu watakayo sema ni kweli kwani huenda wakapunguza ama kuongeza wakati wanaochukua.
Utafiti una yapi ya kusema?

Utafiti tulio nao kuhusu wakati wa wastani unaochukuliwa kufanya mapenzi kwa watu kwa kawaida unaohusisha wanandoa 500 kutoka duniani kote wakipima muda wanaochukua kufanya mapenzi kwa kipindi cha wiki nne kutumia saa.
Wanandoa hawa walianzisha saa kitendo cha ngono kilipoanza sio kabla. Ni vyema kufahamu kuwa, huenda kitendo hiki kikaathiriwa na vitu tofauti. Watafiti walipata kuwa kuna tofauti kubwa ya wakati kati ya wanandoa. Kutoka sekunde 33 hadi dakika 44.
Kwa hivyo ni shwari kuwa hakuna wakati wa "kawaida" ambao kufanya mapenzi hudumu. Wakati wa wastani kati ya wanandoa wote ni dakika 5.4. Huku kuna maana kuwa unapopanga wanandoa wote 500 kutoka kwa kipindi kifupi zaidi na kirefu zaidi cha ngono, wanandoa wa wastani hudumu kwa dakika 5.4 kila mara wanapofanya kitendo hiki.
Kwanini tunafanya ngono kwa kipindi kirefu hivyo?

Kuna mazungumzo mengi kuhusu kipindi ambacho ngono hudumu kwa kawaida. Ukweli ni kuwa, kila mtu ni tofauti. Huku wengine wakichukua muda mrefu katika kitendo hicho, wengine wanachukua muda kidogo. Kufanya mapenzi kunapaswa kuwa kitendo chenye furaha haijalishi iwapo kitachukua muda mfupi ama mrefu. Kisha baada ya kitendo wanandoa wapumzike. Kwa wanandoa wanaolenga kupata watoto, kitendo hiki kina lengo la kutia manii ya manii kwenye uke wa mwanamke ili kurutubisha yai lake kisha kutunga mimba.
Kuna baadhi ya wanaume wanaotumia tembe kuwasaidia kudumu muda mrefu kitandani. Tembe hizi zina athari hasi kwa afya ya wanaume na kuna baadhi waliopoteza maisha yao baada ya kutumia tembe hizi. Kitendo cha kufanya mapenzi kinapaswa kuja kwa njia asili. Furahia kitendo hiki bila kuwa na fikira nyingi kuhusu ngono hudumu muda upi kwa kawaida.
Chanzo: WebMD
Soma Pia:Malengo 7 Ya Uhusiano Ya Kufanya Mapenzi Yenu Yawe Bora Zaidi