Je, Kufanya Mapenzi Katika Nyakati Za Mwanzo Za Ujauzito Husababisha Kupoteza Mimba?

Je, Kufanya Mapenzi Katika Nyakati Za Mwanzo Za Ujauzito Husababisha Kupoteza Mimba?

Orgasms cannot trigger a miscarriage.

Kuna imani tofauti kuhusu ngono na kupoteza mimba. Wanandoa wengi haswa wale ambao wameweza kupoteza mimba hapo mbeleni, mara nyingi, huwa na wasiwasi, iwapo, ni salama kufanya mapenzi wakati wa ujauzito.  Wana wasiwasi,  kwa mfano kama kupenya kwa uume ndani ya uke kunaweza kumuumiza  kijusi kwa bahati mbaya. Pia wanaweza jali kama kubana kwa tumbo la uzazi wakati wa msisimko wa mapenzi kunaweza kusababisha matatizo kwa ujauzito. Ni jambo la kawaida kuwa na wasiwasi. Kwa hivyo, kufanya mapenzi katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito husababisha kupoteza mimba? Hatimaye, kwa idadi kubwa ya wanawake hakuna ushahidi kuwa kufanya mapenzi wakati wa ujauzito husababisha kupoteza mimba au matatizo mengine.

Nini utafiti unaonyesha kuhusu kufanya mapenzi katika miezi mitatu ya kwanza ya ujauzito kama husababisha kupoteza mimba.

Je, ngono katika uja uzito ina athari kwa mimba?

Ingawa utafiti ni mchache  juu  ya kupoteza mimba katika miezi mitatu ya mwanzo ya ujauzito. Hakuna uhusuiano unaojulikana kati ya kufanya mapenzi na kupoteza mimba. Pia waatalamu hawaoni uhusiano wote kati ya tendo la kujamiana na uchungu wa kuzaa kabla ya wakati. Kwa hivyo kama hakuna matatizo yoyote ya kukuzuia iwapo tayari kufanya mapenzi.

Kufanya mapenzi wakati wa ujauzito huonekana tabia isio na madhara yoyote. Hii ni kwa sababu  mlango wa tumbo la uzazi wako na maji yanamzunguka mtoto tumboni humkinga mtoto kutokana na uume.

Habari njema au mbaya kulingana na vile unavyoiana ni kuwa kufanya mapenzi wakati wa ujauzito ni salama sana kwa wanawake wengi wasio na matatizo yoyote. Watu wengine huhisi kama hufurahia mapenzi zaidi wakati wa ujauzito na wengine hawana furaha.

Ngono na kupoteza mimba: Nani apaswa kutofanya mapenzi wakati wa ujauzito

ngono na kupoteza mimba

Wakati mwingine daktari wako anaweza kukushauri usifanye mapenzi wakati wa ujauzito. Hii ni ikiwa unapata dalili kama vile kuvunja damu kwa uke, unavunja maji yanayomzunguka mtoto, ama una historia ya kupatwa na uchungu wa uzazi kabla ya wakati kuwadia .

Mapenzi wakati wa ujauzito yaweza kuwa si salama kwako kama una historia ya kupoteza  mimba mara kwa mara , wewe hupatwa na uchungu wa uzazi kabla ya wakati, kuvuja damu au  una kizazi kisicho na uwezo. Hii ni hali ambayo mlango wako wa tumbo la uzazi huathirika na kupanuka bila ya kubana katika kipindi cha pili na mwanzo wa kipindi cha tatu wakati uzito wa mtoto unautilia mkazo.

Hayo sio yote, wanawake walio na placenta previa wako katika hatari ya kutokwa na damu kama watafanya mapenzi wakati wa ujauzito. Wanawake walio na kupasuka kwa utando mapema (PROM) pia wanafaa kujiepusha na mapenzi.

Ishara/onyo  zinginie za mapenzi wakati wa ujauzito hutokea baada ya kujamiana. Ikiwa una  vuja damu ama una uchafu wenye harufu mbaya baada ya kufanya mapenzi mwambie daktari wako mara moja.  Uchafu waweza kuwa ishara ya maambukizi  na yanaweza safiri hadi kwa tumbo la uzazi ilihali kuvuja damu kwa wewaza kuwa ishara ya shida kwa jumla.

Kwa sehemu kubwa,mapenzi wakati wa ujauzito sio jambo la wasiwasi kwa madaktari wengi. Lakini kama una wasiwasi kuwa kufanya mapenzi kunaweza mdhuru mtoto wako anayekua ama sababisha upoteza mimba zungumza na daktari wako. Ikiwa unaona aya kumbuka kuwa wakunga na madaktari hasa OB/GYNS huwaona wagonjwa wenye matatizo sawia na yako kila siku.  Hawatafikiri ni ujinga kuwa na maswali kuhusu mapenzi wala ata yale ya ujauzito. Ni muhimu kupata ujuzi kuhusu ngono na kupoteza mimba.

ngono na kupoteza mimba

 Msisimko wa mapenzi katika miezi ya kwanza ya ujauzito                                                

Linapowadia swala la msisimko wakati wa kufanya mapenzi, wanawake wote hupatwa na kubanwa kwa tumbo la uzazi. Prosta glandins ndio husababisha hili. Utapata prostaglandins kwenye sahawa au manii na tishu zingine za mwili. Unahisi tu kubanwa kwa zaidi hasa kwa vile tumbo la uzazi limepanuka, na, kuna mwongezeko wa damu. Lakini kwa ujauzito usio na matatizo, huku kubanwa hakutasababisha upoteza mimba. Mtoto wako ambaye hajazaliwa amekingwa vyema dhidi ya sarakasi za mapenzi.  Ule mfuko wa mimba wenye maji, na, misuli ya tumbo la uzazi iko pale kufanya kazi yake.  Na lile kamasi linalofunga mlango wa tumbo la uzazi uhakikisha amelindwa kutokana na maambukizi. Tunatambua mengi kuhusu ngono na kupoteza mimba.

Ngono na kupoteza mimba: Ni mitindo ipi bora zaidi ya  kufanya mapenzi wakati wa ujauzito

Mradi unajihisi umeliwazika, mitindo mingi ya kufanya mapenzi ni sawa.  Hata ngono ya mdomo ni sawa  mradi hauhisi kutatizika. Kuwa na uhusiano na mpenzi wako na mfanye mapenzi. Mshikamane kwa njia mpya na mtafute mitindo mipya ya kufanya mapenzi na mtakuwa wenye furaha.

Kujamiana ni tendo lenye manufaa. Na kufanya mapenzi wakati wa ujauzito kunaweza mfanya mwanamke mjamzito asiwe na wasiwasi, na awe mwenye furaha. Kufanya mapenzi hukutasababisha kupoteza mimba kwa njia yoyote ile, isipokuwa kama una hali ya kimatibabu. Pata ushauri kutoka kwa daktari wako kama una mashaka yoyote na uende mbele na kile atapendekeza. Kuwa na ujauzito wenye afya.

Also read: 5 Ways To Avoid Pregnancy Without Abstaining From Sex

Written by

Risper Nyakio