Baada ya kuwa pamoja kwa muda mrefu, mara nyingi mioto ya kufanya mapenzi hudidimia katika wanandoa. Huenda wakafanya tendo la ndoa mara tatu ama chache kwa wiki. Hata wanapofanya kitendo hiki, hakina ladha kama ilivyokuwa hapo awali. Vidokezo hivi vitawasaidia wanandoa kurejesha na kuwa na ngono ya kutikisa akili zaidi.
Ngono ya Kutikisa Akili
- Zungumza

Mlipokuwa mkianza kuchumbiana, mara kwa mara mlikuwa na mazungumzo ya kingono. Mazungumzo haya husaidia kuiweka akili katika hali ya kujitayarisha kwa kitendo kile. Baada ya kuwa pamoja kwa muda, mazungumzo haya kati ya wanandoa hufifia.
Rejesha mazungumzo haya na mchumba wako. Mnapokuwa hadharani, nong'ona maskio mwa mchumba wako jinsi ambavyo utamtesa kitandani usiku. Fanya hivi mara kwa mara. Mtumie jumbe kwenye rununu anapokuwa kazini. Mweleze unavyomtamani na mambo ambayo ungependa kujaribu naye.
2. Mapenzi ya asubuhi
Badala ya kuamka kukoga kwa haraka kisha kuenda kazini. Kuwa na kipindi cha mapenzi ya asubuhi na mchumba wako. Kufanya mapenzi ni aina ya mazoezi na kutakupa faida sawa na kukimbia asubuhi.
Kuanzia siku yako kwa njia hii kutakupatia nishati tosha za kusukuma siku yako. Pia, utahisi vyema zaidi.
3. Rejesha Kutopanga

Mojawapo ya vitu vinavyofanya mapenzi kukosa ladha ni kuwa na utaratibu fulani wa kufuata. Mmezoea jambo mmoja na ni rahisi kwenu kufahamu kinachofuata. Badilisha mambo, fanya kitu ambacho mchumba wako hatarajii.
4. Toka Chumbani cha kulala
Nani aliyesema kuwa kufanya mapenzi kunastahili kuwa chumbani cha kulala tu? Kuna vyumba vingine ambavyo mnaweza kujaribu kitendo hiki.
Ukianza kucheza na mchumba wako, usimvute hadi chumbani cha kulala ili kukamilisha mlichoanza. Sebuleni, jikoni ama hata bafuni ni baadhi ya vyumba ambavyo mnaweza kujaribu kitendo hiki. Hata hivyo tahadhari mnapokuwa bafuni.
5. Kusafiri pamoja

Kusafiri pamoja na kufanya mapenzi katika miji tofauti huongeza mapenzi na utangamano kati ya wanandoa. Panga safari ya siri kisha umjulishe mpenzi wako siku ya safari. Atafurahia wazo lako na mtakuwa na wakati mwema mbali na majukumu yenu ya kila siku.
Soma pia: Kufanya Mapenzi Kupata Mimba: Mambo 9 Wanandoa Wanapaswa Kujua