Utaratibu Aina 6 Wa Kufuata Kupata Ngozi Ya Afya Na Inayo Ng'aa

Utaratibu Aina 6 Wa Kufuata Kupata Ngozi Ya Afya Na Inayo Ng'aa

Healthy skin doesn't come in a day, but by following this guidelines you can be certain that you are on the right path.

Ngozi ni kiungo cha mwili kilicho kikubwa zaidi cha mwili wa binadamu kinacho ufanya kuonekana zaidi. Kwa sababu hii, kwa asili tuna hamu ya kung’aa na kuwa na ngozi yenye afya. Walakini, hamu hiyo inaridhishwa tunapo ona matokeo bila kukawia. Haijalishi ama unapambana na hali ya acne, madoa, ngozi nyeusi ama iliyo kauka, hali hiyo hairekebishwi kwa siku moja. Kwa ujumla, ngozi yenye afya inahitaji muda, upole na kutuzwa kila mara kwa kufuatia utunzaji wa ngozi. Fahamu jinsi ya kupata ngozi ya afya inayo ng’aa utakayo ipendelea.

Jinsi ya kupata ngozi ya afya inayo ng’aa kwa urahisi

Wengi wanataka ngozi ya afya na inayo ng’aa, ila ngozi hii inakaa vipi kwani ngozi ni tofauti. Kulingana na Dr. Tina Funt, “Ngozi inayo ng’aa ni ngozi iliyo na unyevu na laini- sio nyepesi, haijakauka wala kuwa na doa. Ngozi inayo ng’aa ina shimo ndogo ama hata inavyo kaa ni laini bila madoa”. Hapa chini kuna njia ambazo unaweza tumia kukuza ngozi yenye afya na inayo ng’aa:

  •  Chagua viungo vya kuing’arisha ngozi yako

bright skin

Unapo nunua bidhaa za moisturizer na serum, chukua muda kuangalia kontena yake. Tafuta majina kama “kufanya ing’ae kwa kimombo brightening” na skin tone-evening,” na viungo kama vile vitamini C, vitamini B3, Resorcinol na alpha-arbutin. Wataalum wanasema kuwa vitamini C ni enzyme inayo ifanya ngozi yako kung’aa kwa kubana enzyme inayotoa pigments na vitamini B3 inapunguza utoaji wa pigment ili kufanya sehemu nyepesi zing’ae. Na Resorcinol na Alpha-arbutin huvunja pigments na kufanya rangi ya ngozi kuwa sawa, asema Cynthia Price, M.D mtaalum wa afya ya ngozi wa Phoenix.

  • Hakikisha una maji tosha mwilini wakati wote

African woman drinking water in a field

Kulingana na Jeanine Downie, M.D., mtaalum wa afya ya ngozi katika New Jersey, “Kukosa maji tosha mwilini huifanya sura yako ikakaa nyepesi na hata kupata mikunjo. Hakikisha unapaka bidhaa za kuipa unyevu almaarufu kama moisturizer kila asubuhi na jioni kuipa unyevu ufaao”. Unapo tafuta bidhaa za kuipa ngozi yako unyevu nyevu, endea mafuta na krimu badala ya serums. Lotions na krimu huipa ngozi unyevu zaidi kwa sababu ni mchanganyiko wa mafuta na maji, ambazo zina ipa ngozi yako unyevu ufaao.

  • Zingatia utaratibu wa kuusafisha kila mara

Kuhakikisha unaiweka ngozi yako iking’aa wakati wote, lazima uwe ukiisafisha wakati wote. Huku kunasaidia kutoa uchafu na mabaki yanayo ziba shimo za ngozi. Fanya hivi usiku na mchana wa kutumia idadi ndogo ya cleanser kwenye vidole vyako. Kisha uendelee na kusafisha uso wako kwa kufuata mwendo kana kwamba wa saa. Kisha kutoka kwa upande wa ndani hadi wa nje wa uso wako kuhakikisha umesafisha kila mahali.

African woman aplying lotion

  • Kula vyakula vilivyo na antioxidants

Ikiwa umekuwa ukishangaa ama chakula unacho kula kina iathiri ngozi yako, ndio, kina athari kubwa. Hakikisha una strawberries, blackberries, walnuts, pomegranate, raspberries, cranberries na guavas. Jaribu kuchanganya lishe yako ya kila siku ama kuzila peke yake. Kulingana na Jaclyn London, M.S., R.D, “Utafiti wa mwanzo uli husisha aina hii ya antioxidants zinazo toa sumu kulinda seli za ngozi kutokana na hatari za miale ya jua kama vile hyperpigmentation.

  • Tumia mafuta ya uso ili kufanya uso wako ung’ae 

Kuna habari njema kwa wale wanao taka ngozi yao ing’ae baada ya haya yote. Bidhaa mpya za utunzaji wa ngozi zinazo husisha umuhimu wa kuwa na maji tosha na kutumia moisturizer iliyo na athari za kuongeza uwezo wa uso wako kung’aa zinapatikana. Ili kuzipaka ifaavyo, paka kana kwamba unapaka mafuta usoni kabla ya kujipodoa ama kwa upole kwenye uso, mashavu na chini ya nyusi zako.

  • Exfoliate ngozi yako
ngozi ya afya inayo ng'aa

Picha: Shutterstock

Unatumia exfoliants za kifizikia mbili ama tatu kwa wiki ama kemikali za exfolianta mara moja kila wiki iwapo ngozi yako ni nyeti. Kulingana na mkemia mkubwa Sabina Wizemann, “Mojawapo ya njia bora zaidi za kuifanya ngozi yako ing’ae zaidi kwa kipindi hiki na muda mrefu ujao ni kwa ku exfoliate. Mchakato huu unatoa ngozi ya nje ya seli zilizo kufa na kuifanya ngozi iwe laini zaidi.”

Kuna matatizo ya ngozi ambayo huwa vigumu kutibu kwa sababu ya kuharibiwa na miale ya jua ama sababu zingine ambazo huenda zikahitaji kuangaliwa na mtaalum wa afya ya ngozi. Iwapo utajipata na matatizo ya ngozi, usisite kumtembelea mtaalum ambaye atakushauri kuhusu suluhu bora kwako.

Soma pia:

Best Foods For Oily Skin: Maintain Your Skin By Including These Foods In Your Diet

Recipe For The Best Homemade Cream For Chocolate Skin

Vyanzo: Good House Keeping, Skin Science, Image Dermatology

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Lydia Ume na kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio

Written by

Risper Nyakio