Mitindo Tofauti Ya Kiafrika Ya Nguo Za Mama Mwenye Mimba

Mitindo Tofauti Ya Kiafrika Ya Nguo Za Mama Mwenye Mimba

Haijalishi ladha yako ya mavazi kwani tuna mtindo wa kila mmoja.

Miaka mingi ya hapo awali, huenda ikawa kuwa hujashuhudia  matatizo ya kupata nguo za kuenda sherehe kama vile  za mikutano ya kikazi, harusi, kula nje na zinginezo. Wakati huu unao mtarajia mtoto, huenda ukawa na wakati mgumu kupata mavazi ya kupendeza ya mama mwenye mimba yatakayo kupendeza. Kuna aina nyingi za nguo za mama mwenye mimba hasa zenye nyenzo za ankara.

Baadhi ya wakati, inakutaabisha kujua kuwa huweza valia mitindo fulani ya mavazi, kwa sababu haina starehe na sio ya afya kwako na kwa mtoto wako.

Hauko peke yako. Wanawake wajawazito mara kwa mara huteta hawawezi pata mavazi ya kuvalia.

“Hata kama mtaalum wa mavazi, nilikuwa na wakati mgumu nikinunua mavazi ya uzazi. Kuvalia ninapo enda sherehe, kupanga, kuchagua na kuzitengeneza,” alisema Shuga, mtaalum wa mavazi huko Uyo, Nigeria. “Unapo kuwa na mimba, inasaidia kuwa na mitindo tofauti ya mavazi.”

Mtu yeyote anawependeza anapokuwa katika safari yake ya mimba. Ili kupunguza kazi nyingi ya kutafuta kwenye mitandao mavazi ya mama mwenye mimba, tume orodhesha mitindo tofauti itakayo kufaa.

Kabla tuendelee, hapa kuna mambo muhimu ya kujua kuhusu mavazi ya mama mwenye mimba:

• Wataalum wa afya ya uzazi ama kike hawashauri viatu vyenye visigino virefu

• Sio lazima uyahatarishe maisha ya mtoto wako; unaweza pendeza na viatu visivyo na visigino virefu

• Mbali na viatu, unaweza patia mavazi yako ladha kwa kuvalia mishipi, shanga, begi, herini na kusongwa mitindo ya kupendeza.

Hapa Ni Orodha Yetu Ya Nguo Za Mama Mwenye Mimba Za Nyenzo Za kiafrika ama Ankara

1. Vazi lisilo na mabega la mama mwenye mimba
beautiful dresses for pregnant women

Chanzo cha picha hii: BerryDakara.com

Huu ni mtindo usio na wakati na ni wa tabaka lake, na wa kupendeza hasa kwa wanawake wenye mimba. Haijalishi iwapo unachagua urefu wa goti la mguu ama blausi ama hata rinda bila mabega kwani utalifurahia.

“Rinda la mama mjamzito bila ya mabega hupendeza zaidi na linaweza valiwa wakati wowote katika safari yako ya mimba,” alisema Shuga.

Unaweza livalia na lapulapu ama viatu vyovyote vyenye starehe.

2. Rinda la Ankara ama Vlisco la kiuno kilicho dhibitika
ankara pregnancy dresses

Chanzo cha picha: Nigerianfinder.com

“Napenda rinda linalo kuwa na kiuno hiki kwa sababu linapendeza wakati wote. Kwa hivyo, mara kwa mara, nashauri mwanamke mwenye mimba aliye choka kutafuta mavazi ya mama mwenye mimba kwa mtandao kununua rinda la mtindo huu. Nawaambia kwa urahisi wajaribu mtindo huu na kiuno kilicho dhibitika,” alisema Shuga.

Rinda hili linapendeza zaidi unapo livalia na mshipi mwembaba. Kisha uchague rangi ya mshipi inayo andamana na rangi ya nyenzo za rinda unalo livalia.

3. Rinda la kiafrika la trapezium la mama mwenye mimba
ankara pregnancy dresses

Chanzo cha picha: tuko.co.ke

Iwapo unatafuta mtindo wa hivi sasa ambao unaweza valia trimesta ya tatu ya mimba, usitafute tena. Nguo za trapezium huwa mojawapo ya mavazi ya ankara yanayo pendwa zaidi na watu.

“Na mavazi haya, unawetengeneza nguo lisilo na bega moja, shingo ndefu ama mtendo wowote unao kupendeza.”

Ina hakikisha una starehe, na hii inapaswa kuwa sababu kuu ya kununua nguo yoyote wakati wa safari yako ya mimba.

4. Rinda la kiafrika la ghorofa

nguo za mama mwenye mimba

Chanzo cha picha gistvic.com

Rinda lililo na ghorofa ni bora kwa wanawake wanao taka kuficha mimba yao.

“Mavazi ya ankara ama vlisco ya ghorofa bila shaka ni maarufu zaidi kwa mavazi ya uzazi ya Nigeria, alisema Shuga. Unaweza onyesha urembo wa mwili wako na wakati huo huo kuficha tumbo yako inayo anza kuonekana.”

Mavazi haya yanamfanya mwanamke mjamzimto kukaa wa tabaka la juu. Ila, zaidi ya yote, yanaukubalisha mwili wako kupumua na kukuwezesha kutembea kwa urahisi.

5. Rinda refu la kiafrika la msimu wa kiangazi

nguo za mama mwenye mimba

Chanzo cha picha: amillionstyles.com

Ifurahie mimba yako kwa kuvalia rinda hili lirefu na la kupendeza. Sawa na yale mavazi marefu ya msimu wa jua yaliyo mapana na huru.

“Vazi hili linalo pendeza ni mojawapo ya mavazi ninayo yapenda zaidi. Nalipenda kwa sababu ni mojawapo ya mavazi ambayo unaweza valia hata baada ya kujifungua. Bila shaka unaweza punguza urefu wake na saizi baada ya kupunguza uzito wako wa mwili,” alisema Shuga.

Iwapo ungetaka mavazi ya uzazi ya mitindo ya hivi sasa ambayo inaweza tengenezwa kwa urahisi ya kuenda matembezi, unapaswa kuweka akilini tungeneza rinda refu la msimu wa jua.

Kuna aina nyingi tofauti za mavazi ya ankara ya mimba, mitindo na starehe ambayo unaweza tumia mapambo tofauti na upendeze sana. Haupaswi kuvalia nguo zisizo pendeza kwa sababu unakaribia kujifungua.

Iwapo unapendelea rangi zinazo ng’aa, unapaswa kuchagua nyenzo za ankara zinazo ng’aa, Vlisco ama Kente. Wataalum wengi wa mitindo hushauri nyenzo zinazo kuwa na rangi za kung’aa.

Usiwe na shaka kuwa safari yako ya mimba itakuwa mbali na mitindo ya mavazi. Orodha yetu ya nguo za mama mwenye mimba itakusaidia kuhakikisha kuwa una ng’ara hata ukiwa na kiumbe kina cho kua tumboni mwako.

 

Pulse NG

Soma pia: Pregnancy photo shoot poses

Makala haya yaliandikwa kwa mara ya kwanza na Julie Adeboye kisha yaka tafsiriwa na Risper Nyakio.

Any views or opinions expressed in this article are personal and belong solely to the author; and do not represent those of theAsianparent or its clients.

Written by

Risper Nyakio