Nguo Za Uzazi: Mavazi Bora Unapokuwa Na Mimba

Nguo Za Uzazi: Mavazi Bora Unapokuwa Na Mimba

Kuna aina nyingi za nguo ambazo unaweza valia ila, anuwai zako hubadilika unapokuwa na mimba. Je, ni mavazi yapi unayopaswa kuvalia ukiwa na mimba?

Siku za hapo awali, wanawake wajawazito huvalia nguo kubwa, refu na pana. Wakati mwingi, wengi wao hukua wakificha mimba, hawapendi watu wajue wana mimba ama huenda wakawa wana aibika kuwa na mimba. Kwa muda, jambo hili limebadilika na wanawake wameanza kukumbatia ujauzito na safari hii ya kupendeza. Jambo hili lina shuhudiwa kufuatia jinsi wanawake wanao kuwa na mimba wana valia. Mavazi ya kupendeza na hata kutunza mili yao baada ya kujifungua. Je, mwanamke mwenye mimba anapaswa kuvalia mavazi yapi? Tuna angazia nguo za uzazi zilizo mwafaka kwa mama aliye na mimba.

nguo za uzazi

Mambo Ya Kutia Akilini Unapo Nunua Nguo Za Uzazi

Mwili wako una utabadilika

Ni vyema kwa kila mama mwenye mimba kufahamu na kukubali kuwa mwili wake unabadilika. Huenda ikawa kuwa hapo mwanzoni, ulikuwa mkonda na baada ya kupata mimba mwili wako ukabadilika na kuwa na uzito mwingi. Nguo ulizo valia hapo awali huenda ikawa hazita kutosha kama zilivyo hapo awali. Kwa hivyo ni wakati wa kufanya ununuzi wa nguo mpya ambazo zita kutosha vizuri.

Kubali umbo lako jipya, na ununue mavazi ambayo yata pendeza kwa mwili wako. Ila nguo zako mpya hazipaswi kuwa kubwa sana kiwango cha kuficha tumbo yako.

Nunua mitindo ya hivi sasa

Kuwa na mimba sio sababu ya kukufanya uvalie nguo zilizo zeeka ama zilizo pitwa na wakati. Hakikisha kuwa unanunua nguo ambazo zinapendeza na kuifanya tumbo yako ionekane. Pia hakikisha unavalia mapambo kama vile herini na mikufu ili kuongeza ladha kwa mavazi yako ya kila siku.

nguo za uzazi

Image source: BerryDakara.com

Nunua mavazi ambayo hayakazi tumbo yako

Unapo kuwa na mimba, ni vyema kuvalia mavazi ambayo hayaikazi tumbo yako. Kuna suruali ambazo zina kubalisha tumbo yako kukua vyema bila kuikaza. Kwa njia hii, unaweza fanya kazi zako kwa urahisi. Pia mavazi kama gauni ya kufunga maarufu kwa kimombo kama wrap dress ni bora katika wakati huu. Ni rahisi kuvalia na kutembelea.

Mavazi ya rangi tofauti

Una pokuwa na mimba, sio wakati wa kuvalia nguo zilizo nyeusi wakati wote. Nunua mavazi ya rangi tofauti zinazo furahisha macho kama vile machungwa, kinjano, samawati, buluu na kadhalika.

Mavazi ya kiafrika ama Ankara

Mavazi yenye nyenzo hizi za ankara zinaweza shonwa kwa njia tofauti. Unaweza tengeneza rinda ama sketi ya ankara ambayo inakutoshea vizuri. Nguo za nyenzo hii zinaweza valiwa kwa sherehe yoyote, kwenda kazini, kanisani, sherehe rasmi ama sherehe isiyo rasmi. Kwa hivyo, nunua nyenzo yako kisha uelekee kwa fundi wako wa nguo akushonee vazi litakalo kufaa.

mavazi ya uzazi

source: ankarafashion.com.ng

Zaidi ya yote, ifurahie safari yako ya ujauzito na usisahau mwili wako. Hakikisha kuwa unafanya mazoezi mepesi angalau dakika 30 kila siku hata kama ni kutembea. Pia kula mboga na matunda kwa wingi na kunywa viwango vinavyo faa vya maji kwa siku.

Kumbukumbu: Zoom Tanzania, webmd

Soma Pia: Mitindo Tofauti Ya Kiafrika Ya Mama Mwenye Mimba

Written by

Risper Nyakio