Dalili 3 Kuu Zinazo Ashiria Kuwa Mwanamke Ana Mimba!

Dalili 3 Kuu Zinazo Ashiria Kuwa Mwanamke Ana Mimba!

Mabadiliko kwenye matiti na chuchu huzidi katika wiki ya 11 ya ujauzito. Na rangi nyeusi ya chuchu kuongezeka na kuwa kubwa zaidi.

Wakati ambapo kufanya kipimo cha mimba ama kuenda ultra sound ndizo njia dhabiti za kudhihirisha kwa kweli iwapo mama ana mimba. Kuna njia zingine ambazo zinaweza msaidia mwanamke kufahamu hali yake. Kama vile kuangalia ishara za mimba. Je, nini dalili za mimba?

Ishara za mimba

nini dalili za mimba

Kutoka wiki ya kwanza hadi ya nne, mabadiliko mengi hufanyika kwenye seli. Yai lililo utubishwa hugawanyika na kutengeneza kikundi cha seli ambacho kitakua kuwa fetusi.

Siku 10-14 baada ya kupevushwa kwa yai, yai hujipandikiza kwenye uterasi. Na mwanamke hutokwa na matone ya damu. Wakati sawa na mwanamke anapo tarajia kipindi chake cha hedhi. Na huenda hali hii ikaonekana kama kipindi cha hedhi chepesi.

Rangi ya matone baada ya kupandikiza kwa yai huwa pinki. Damu hii hutoka kwa siku chache ikilinganishwa na na kipindi cha hedhi. Uchungu wake sio mwingi kama wa hedhi.

  • Kukosa kipindi cha hedhi

Baada ya kupevushwa kwa yai, mwili huanza kutoa kichocheo cha human chorionic gonadotropin kwa kifupi hCG. Homoni inayo komesha ovari kutoa mayai zaidi kila mwezi. Na mwanamke kukosa kupata vipindi vyake vya hedhi vya kila mwezi.

Unapo kosa kupata kipindi chako cha hedhi, ni vyema kufanya kipimo cha mimba. Ili kuwa na uhakika. Vipimo vingi vya kinyumbani vinaweza baini kuwepo kwa hCG kwenye mkojo na kuonyesha kama una ujauzito.

  • Uchovu katika siku za mwanzo za ujauzito

nini dalili za mimba

Uchovu una weza anza wakati wowote ukiwa na mimba. Ongezeko la idadi ya homoni ya progesterone mwilini humfanya mama ahisi kuchoka wakati wote.

Wiki za kwanza za ujauzito utahisi uchovu mwingi. Hakikisha kuwa unapumzika vya kutosha. Kuweka chumba chako cha kulala kikiwa na temprecha zisizo juu kutasaidia. Temprecha ya mwili huwa juu wiki za kwanza za ujauzito.

  • Mabadiliko kwenye matiti

Katika wiki ya 4 hadi ya 6. Utaanza kuhisi kana kwamba chuchu zako zimefura kufuatia mabadiliko ya homoni mwilini. Wiki chache baada ya mwili wako kuzoea mabadiliko haya, hali hii itahisi ya kawaida.

Mabadiliko kwenye matiti na chuchu huzidi katika wiki ya 11 ya ujauzito. Na rangi nyeusi ya chuchu kuongezeka na kuwa kubwa zaidi. Nunua sindiria nzuri ya pamba, ili uwe na starehe tosha.

Mbali na mabadiliko haya, mwanamke hushuhudia mhemko wa hisia, kichefuchefu na ugonjwa wa asubuhi. Ikiwa swali lako kuu lilikuwa, nini dalili za mimba? Ni matumaini yetu kuwa sasa hivi, una maarifa zaidi.

Soma Pia: Kwa Nini Una Hisi Kujikuna Miguu Katika Ujauzito?

Written by

Risper Nyakio