Njia Tano Za Kuzuia Ujauzito Bila Ya Kukomesha Kufanya Mapenzi

Njia Tano Za Kuzuia Ujauzito Bila Ya Kukomesha Kufanya Mapenzi

Did you know? Withdrawal of the penis prior to ejaculation and periodic abstinence does not prevent pregnancy or the spread of sexually transmitted diseases.

Kufurahia maswala ya mapenzi sio lazima iwe biashara hatari. Haswa sasa hivi ambapo kuna njia nyingi sana za kupanga uzazi huko nje, za kutosheleza mahitaji anumwai. Uzazi wa mpango unaweza kutumika kuzuia ujauzito, na, njia zingine zitakukinga kutokana na maambukizo ya zinaa. Ikiwa unashangaa jinsi ya kuzuia ujauzito bila ya kuweka kikomo kwa mapenzi, endelea kusoma. Tumeweka pamoja orodha ya mikakati mitano ya kukusaidia.

Jinsi ya kuzuia ujauzito:  Aina za uzazi wa mpango

Njia Tano Za Kuzuia Ujauzito Bila Ya Kukomesha Kufanya Mapenzi

Waweza jipata ukijiuliza: Ni mkakati upi utakuwa bora kwangu na kwa mtindo wangu wa maisha? Ni mkakati upi utanikinga kutokana na maambukizi ya zinaa? Ni upi una urahisi wa kutumia? Kuna athari zipi? Gharama? Itafanya kazi ninavyotaka? Hapa kuna orodha ya mikakati ya kukuwezesha kufanya uchaguzi wako. Haijalishi mtindo wako wa maisha kuna mkakati utakao kufaa.

Kondomu

kuzuia kupata mimba

Kondomu ndio tu njia ya kipekee ambayo hukukinga kutokana na maambukizi ya zinaa na huzuia ujauzito. Utaipata pindi tu unapoihitaji. Haina homoni na unaweza kwenda nayo mahali popote pale utakwenda. Na huja katika aina mbili ya kiume na ya kike. Unaweka kondomu ya kiume kwa uume ulio sawa. Hivi hufanyika kama kizuizi. Huwa inazuia yale maji ya ngono yasipite kutoka kwako hadi kwa mwenzako wakati wa kujamiiana. Hapo kabla ya kufanya mapenzi, unaiweka ile kondomu ya kike ndani ya uke wako. Kulingana na matumizi, kondomu ya kike sio mwafaka ikilinganishwa na ile ya kiume na unaweza hitaji mazoezi ili kuizoea.

Uzuri:  Ndio kinga bora zaidi kutokana na maambukizi ya zinaa, yaweza kutumika wakati wowote ule unapoihitaji na haina homoni.

Ubaya: Yaweza kupasuka au kutoka wakati unafanya mapenzi kama haitatumika vizuri na watu wengine wana mzio wa kondomu za mpira.

Kidonge vya kuzuia mimba

Njia Tano Za Kuzuia Ujauzito Bila Ya Kukomesha Kufanya Mapenzi

Ni tembe ndogo ambayo humezwa mara moja kwa siku kuzuia ujauzito.  Kuna idadi ndogo ya aina za tembe kufanyia uchaguzi kwa hivyo inabidi utafute ilio sawa kwako. Tembe iliyojumuishwa huwa na estrogen na progestin lakini ile tembe  ndogo huwa na homoni moja tu progestin. Tembe ina manufaa mengi, ila kukumbuka kuimeza kwa wakati ni lazima.

Uzuri : Hufanya kazi vizuri inapotumika ipasavyo, huwezesha kufanya mapenzi wakati wowote ule na haizuii kufanya mapenzi. Tembe zingine hupunguza vipindi vizito na vichungu vya kutokwa na damu na huwa na athari chanya kwenye chunusi.

Ubaya : Kusahau kumeza tembe yako kunamaanisha haitafanya kazi inavyohitajika, ni wanawake pekee amabao waweza kutumia tembe, sio mwafaka kwa wanawake ambao hawatumia uzazi mpango ulio na estrogen na haizuii kutokana na maambukizi ya zinaa.  Tembe hupatikana tu baada ya kupata maagizo kutoka kwa mhudumu wa afya kwa hivyo tembelea mhudumu wa afya aliye karibu nawe.

 Kifaa cha ndani( IUD)

kuzuia kupata mimba

Hiki ni kifaa kidogo chenye umbo la T ambacho kimetengenezwa na vitu vilivyo na progesterone au plastiki na shaba. Mhudumu wa afya aliyehitimu hukiweka ndani ya tumbo la uzazi. Ni njia ya uzazi mpango ambayo hudumu wa afya anaweza kubadilishwa wakati wowote ule.  Kile kifaa chaweza kukaa pale ndani kwa kati ya miaka matatu, hadi kumi kulingana na aina yake.

Vifaa vingine vina homoni ambazo huachiliwa polepole kuzuia ujauzito. Hiki kifaa ni mbinu ya dharura kuzuia ujauzito. Iwapo daktari atakiweka ndani ya tumbo la uzazi katika siku tano baada kufanya mapenzi bila kinga.

Vifaa vilivyo na shaba huwa na asilimia 99% ya ufanisi na vile vina homoni huwa na asilimia 99.8% ya ufanisi. Kwa hivyo umekingwa vilivyo na uzazi mpango.

Ubaya : utakuwa na kutokwa na damu kusio kwa kawaida na kuteleza katika miezi sita ya kwanza na utahitaji mhudumu wa afya aliyefuzu kuweka na kutoa kile kifaa na hakizuii kutokana na maambukizi ya zinaa.

Contraceptive implant

Njia Tano Za Kuzuia Ujauzito Bila Ya Kukomesha Kufanya Mapenzi

Hii njia daktari huweka fimbo ndogo laini chini ya ngozi yako kwenye mkono wa juu ambayo hutoa homoni progesterone. Hii homoni huzuia ovari zako kuachilia mayai. Pia, inaneneza maji yaliyo kwenye tumbo la uzazi ikifanya ngumu kwa manii kuingia ndani. Kuwekwa hio fimbo uhitaji utaratibu kidogo ukitumia anesthetic.  Hii fimbo hubadilishwa baada ya miaka mitatu.

Uzuri: ina ufanisi mkubwa, haizuii kufanya mapenzi, hudumu kwa muda mrefu, ni uzazi mpango ambao waweza kubadilishwa na huzuia mimba.

Ubaya: inahitaji mhudumu wa afya aliyehitimu kuweka na kutoa ile fimbo, wakati mwingine kwaweza kuwa na kuvuja damu kusio kwa kawaida na haikingi dhidi ya maambukizi ya zinaa.

Mbinu zingine za kuzuia ujauzito

  • Sindano ya uzazi.

Hii sindano huwa na synthetic version ya homoni progesterone.  Daktari hudunga makalio au mkono wa juu na kwa zaidi ya wiki kumi na mbili zifuatazo homoni hutiririka katika mishipi yako ya damu.

  • Dawa za dharura za uzazi wa dharura( morning after pill)

Hizi tembe huzuia ujauzito baada ya mapenzi bila kinga, au kupasuka kwa kondomu ama ubakaji. Inafahamika kama ‘morning after’ pill mbali ina ufanisi ata baada ya siku tano za mapenzi bila kinga.

  • Pete ya uzazi wa mpango

Hii mbinu huhusisha pete ya plastiki kwenye uke wako ambayo kila wakati huwa inatoa homoni.  Hukaa pale kwa muda wa wiki tatu ambapo hutolewa alafu nyingine inawekwa pale baada ya wiki moja.

  • Diaphragm

Diaphragm ni Kipande kidogo cha silicone kinachowekwa ndani ya uke wako ili kuzuia manii au mbegu kutoingia ndani ya tumbo la uzazi. Huunda kizuizi kati ya manii na yai lako kama kondomu

 

Healthline

Also read: The Correct Method For Calculating Your Ovulation

Written by

Risper Nyakio