Mbinu 4 Za Kupima Mimba Zilizo Tumika Na Nyanya Zetu

Mbinu 4 Za Kupima Mimba Zilizo Tumika Na Nyanya Zetu

Ikiwa swali lako kuu ni jinsi wavyele wa kale walivyo pima mimba, usiwe na shaka. Kwani makala haya yana kujuza zaidi kuhusu mbinu zilizo tumika kupima mimba.

Teknolojia imebadilisha mambo yakawa rahisi zaidi katika nyanja mbalimbali za maisha. Kutoka kwa mazungumzo, leo hii, unaweza zungumza na mtu aliye bara tofauti nawe na hata kumwona mnapo zungumza. Kujua kinacho tendeka mahali pengine kunawezekana. Pia watu wanapata masomo wakiwa manyumbani mwao. Bila shaka teknolojia imesaidia kurahisisha maisha sana. Ikiwa wewe ni miongoni mwa watu wanao penda kujiuliza maswali na kutaka kujua jinsi watu wa jadi walivyo ishi. Huenda mojawapo ya maswali uliyo nayo ni jinsi walivyo pima mimba nyakati hizo. Makala haya yana angazia njia asili za kupima mimba zilizo tumika hapo awali.

Njia Asili Za Kupima Mimba

njia asili za kupima mimba

Sote tuna fahamu kuwa mbinu zinazo tumika hivi leo kupima mimba hazikuwa karne chache zilizo pita. Walio ishi enzi hizo hawakuwa na teknolojia tulizo nazo sasa na zinazo tuwezesha kuishi maisha bora zaidi ikilinganishwa na walio ishi hapo awali.

Je, wanadada walijua vipi kuwa wana mimba hapo awali?

Kuna njia mbalimbali ambazo wanadada hapo awali walitumia kujua kuwa wana mimba.

1.Kipimo cha ngano na shayiri

Mojawapo ya vipimo vya kinyumbani vya mapema zaidi vilitoka nchi ya Egypt. Katika enzi za kale, wanawake walishauriwa kukojolea mbegu za ngano na shayiri kwa kipindi cha siku kadhaa. Ikiwa mbegu za ngano zili chipuka, mama alitarajia mtoto wa kike. Na ikiwa mbegu za shayiri zili chipuka, mama alikuwa ana tarajia mtoto wa kiume. Ikiwa mbegu hizi hazi kuchipuka, mwanadada hakuwa na mimba.

Cha kufurahisha zaidi kuhusu kipimo hiki ni kuwa kilifanya kazi na matokeo yake yalikuwa sahihi. Katika majaribio ya maabara mwaka wa 1963, yali dhihirisha kuwa asilimia 70 ya wakati, mkojo wa mwanamke mjamzito ulifanya mbegu kuchipuka na mkojo wa wanawake wasio na mimba, mbegu hazi kuchipuka.

2. Kipimo cha sungura ama panya

Katika miaka ya 1920, wana sayansi wawili kutoka Ujerumani Selmar Aschheim na Bernhard Zondek waligundua kuwa kuna homoni hasa iliyoko kwenye mkojo wa wanawake walio na mimba iliyo husishwa na ukuaji wa ovari. Inayo julikana leo kama HCG. Waligundua haya kwa kundunga mkojo wa mama mwenye mimba kwenye sungura ambaye hakua amekomaa kingono, na kuanzisha mchakato wa kukua kwa ovari. Ili kugundua matokeo ya kipimo hiki, madaktari wali chinja wanyama wale na kuangalia hali ya ovari.

3. Kipimo cha chura

Sawa na kipimo cha sungura, kipimo hiki angalau kilikuwa kizuri kidogo kwani mnyama hakuuliwa. Wana sayansi katika miaka ya 1940 waligundua kuwa mkojo wa mwanamke mwenye mimba unapo dungwa kwenye chura aliye hai, mnyama huyo ata taga mayai katika muda wa masaa 24. Na mnyama huyo hakufa.

4. Kipimo cha kitunguu

onion juice for hair growth

Katika kipimo hiki, mwanamke mwenye mimba ali agizwa kusafisha kitunguu vyema. Kisha kukata na kuingiza kipande cha kitunguu hicho kwenye uke. Matokeo yange gunduliwa asubuhi ya siku iliyo fuata. Ikiwa harufu ya mdomo wake ilinuka kitunguu, hakuwa na mimba kwani uterasi yake ilikuwa wazi na kuwezesha harufu ya kitunguu hicho kufika kwenye mdomo wake. Ikiwa harufu ya mdomo wake ilikuwa kawaida asubuhi iliyo fuata, bila shaka mwanamke huyo alikuwa na mimba.

Baadhi ya vipimo hivi vilichangia pakuu katika vipimo vya damu vinavyo fanyika leo hii.

Chanzo: Mentalfloss

Soma Pia:Je, Mwanamke Ana Uwezo Wa Kuamua Wakati Ambao Atapata Mimba?

Written by

Risper Nyakio