Njia Bora Za Kumwezesha Binti Yako Na Kuboresha Ujasiri Wake

Njia Bora Za Kumwezesha Binti Yako Na Kuboresha Ujasiri Wake

Mhamasishe binti yako na umpe moyo kuwa anaweza timiza malengo yake yote maishani.

Mabinti wachanga ni viumbe vidogo vya kupendeza. Lakini kama wazazi, tunawatakia zaidi ya hayo. Tunataka mabinti wetu wakue wawe wanawake wachanga waio na ujasiri na walio tayari kutawala. Tunataka wawe na uwezo na ushapavu wa kuwa chochote kile wanacho tamani maishani na kutimiza malengo yao. Ni vyema kumwezesha binti yako mapema maishani uwezavyo!

kumwezesha binti yako- mama kupika

Hapa kuna njia bora za kumwezesha binti yako kutimiza malengo yake maishani

1. Kuwa tayari mama

Wazazi wa kike huwa na athari kubwa zaidi kwenye maisha ya mabinti zao. Kwa hivyo mama, jikumbatie na uwe tayari kiakili. Kwa sababu binti yako anakuona na anasikiza kila neno unalo sema.

Kuwa mfano wa kuigwa na uhakikishe kuwa maneno yako yana ambatana na vitendo vyako. Kwa hivyo koma kuwa na shaka kuhusu uzito wa mwili wako na ikiwa aina fulani ya nguo inakufanya uonekana mkubwa.

Tumia lugha chanya na uwe mfano ambao ungependa binti yako afuate. Mara kwa mara, jaribu vitu mpya maishani na kwa njia hii utawahimiza binti zako kufuata nyayo zako wanapokuwa wakubwa.

 

2. Zungumza naye - kwa sana

Sote tunafahamu jinsi watoto wachanga wanavyo penda kuongea. Kwa hivyo ongea naye, na umhusishe katika mazungumzo ya kimaarifa kuhusu mada tofauti kama vile kunyanyaswa na aina tofauti ya miili.

Tengeneza nafasi ya kuzungumza kwa wazi bila kuogopa kuhukumiwa. Na uhakikishe kuwa unamsikiliza kwa makini.

3. Mhimize aseme maoni yake

Mtoto wako mchanga anahitaji kujua kuwa mawazo na maoni yake ni muhimu. Kwa hivyo mhimize aongee kuhusu vitu anavyo penda.

Badala ya kumfichia vitu vinavyo aminika kuwa vya watu wazima, na bado ataona kwenye runinga, kuwa na mazungumzo na binti yako. Mfunze mambo ya dharura na usikilize maoni yake kuhusu vitu tofauti.

Mhimize kusoma vitabu na kwenda kwenya maktaba. Kwa njia hii, atapata maarifa na busara na kumsaidia kuwa na ushupavu kuhusu mambo tofauti duniani.

kulea wasichana shupavu

4. Mfunze kuhusu mifano ya wanawake wa kuigwa

Mbali na mama zao, ni muhimu kuwapa binti zako mifano ya wanawake wanao fuzu katika nyanja tofauti ili waige mifano yao.

Kwa hivyo, ili kuhamasisha mabinti zetu, wahadithie kuhusu wanawake wa ukweli walio badilisha tasnia walizo kuwa katika na wanao heshimika.

5. Heshimu uamuzi wake

Heshimu binti yako mchanga, alivyo, utu wake, uamuzi wake, - wa mavazi, sinema na marafiki.

Epuka kumwambia anacho faa kufanya, kwa njia hii atasoma jinsi ya kuwa mtu binfasi. Ila ni vyema kumwongoza mara kwa mara afuzu katika yote ayafanyayo.

6. Kuwa mfuasi wake wa kwanza

Binti yako anahitaji kujua kuwa utakuwa naye wakati wote, haijalishi umri wake ama mambo anayo pitia maishani mwake.

Mhamasishe kujipenda zaidi kwa sababu kufanya hivi kutamsaidia kuwa na ujasiri na  mshupavu.

7. Mfunze kuwa kujitosheleza na jasiri

Wazazi wa kiume hasa wanapenda kuwaonyesha binti zao kuwa wana wajali. Kwa njia hii kuwapa kila kitu wanacho taka, wapatie nafasi mpya za kujaribu vitu mpya.

Wafunze kuwa ni sawa kufeli kwa jambo fulani na umfunze kuamka kila mara anapo anguka na kujaribu tena. Mwonyeshe kuwa ako sawa na ndugu zake wa kiume.

Mhimize kujaribu vitu ambavyo anaogopa na umkumbushe kuwa kila mara, anasoma jambo mpya.

kumwezesha binti yako - mama8. Mhimize kutangamana na watu na kuwa na marafiki

Mfunze binti yako umuhimu wa kuwa na marafiki wazuri. Hakuna jambo linalo boresha ujasiri na kujiamini kama kuwa na marafiki wazuri wanao kuinua unapokuwa ukihisi vibaya.

Mhimize kujiunga na vikundi vya michezo na utafiti, kwani utafiti unadhibitisha kuwa wasichana wanao cheza michezo huwa na ujasiri mwingi.

9. Msifu kwa juhudi zake kuliko kwa kufuzu kwake

Hakikisha kuwa anapo fanya kitu, unampongeza kwa juhudi zake na kuwa na ujasiri wa kufanya badala ya kufuzu kwake.

Ikiwa ungependa binti yako awe na ujasiri, hakikisha kuwa unamhusisha katika matendo yatakayo boresha ujasiri wake.

Kuingia kwa vikundi vya michezo, uimbaji na uigizaji vitamsaidia sana kwa sababu atafahamu jinsi ya kujieleza.

10. Mfunze kuhusu pesa 

Inapofika kwa pesa na uwekezaji wa fedha, wanawake wanaonekana kuwa nyuma ya wanaume. Njia mojawapo ya kukabiliana na tatizo hili ni kuanza kumfunza binti yako kuhusu pesa angali mchanga na jinsi ya kuzihifadhi.

11. Mfunze kuwa na malengo maishani

Mhimize mtoto wako kuwa na malengo na ndoto maishani na haijalishi zinavyo onekana kuwa ngumu, kuwa anaweza timiza yote anayo taka. Mfunze kuwa na lengo na kisha kufanya kazi ili kutimiza lengo hilo. Mzungumzie na umpe moyo kuwa anawe timiza yote anayo taka. Kumwezesha binti yako kutamsaidia kujua kuwa hakuna jambo gumu duniani ambalo hawezi timiza.

Kilicho muhimu zaidi, mkumbushe kuwa haijalishi kinacho tendeka maishani, bado utazidi kumpenda.

Soma pia: How to nurture a strong mother-daughter bond according to Science

Written by

Risper Nyakio