Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Njia Tofauti Za Uzazi Wa Mpango Ambazo Wanandoa Wanaweza Kutumia

2 min read
Njia Tofauti Za Uzazi Wa Mpango Ambazo Wanandoa Wanaweza KutumiaNjia Tofauti Za Uzazi Wa Mpango Ambazo Wanandoa Wanaweza Kutumia

Kwa wanaotafuta njia nzuri ya uzazi wa mpango, ni vyema kuwasiliana na daktari ili akushauri njia itakayo kuwa bora kwako zaidi.

Kupanga uzazi kunamsaidia mzazi kufanya uamuzi wa wakati bora ambao angependa kumleta mtoto duniani. Wakati ambapo ako tayari na anahisi kuwa ana misuli ya kifedha ya kumtunza mtoto. Pia anapo malizana na mambo kama masomo ama kipindi chenye fikira nyingi kwani ujauzito humhitaji mama kutokuwa na fikira nyingi. Kwani zinamweka katika hatari ya kupoteza mimba. Na kuibua swali la njia nzuri ya uzazi wa mpango ni ipi?

Kuna njia mbali mbali ambazo wanandoa wanaweza kutumia kupanga uzazi. Kuna njia mbili maarufu, za homoni na za barrier.

Njia hizi mbili hufanya kazi vitofauti. Mbinu za barrier huzuia manii kuingia na kukutana na yai la mwanamke. Hakuna dawa ama kichocheo kinacho tumika. Maarufu ni utumizi ya kondomu, za kike ama za kiume. Ni salama kwa wote wanaume na wanawake na hazina athari hasi kwa afya yao.

Njia ya pili ni ya homoni ama vichocheo. Mbinu hizi hutumia vichocheo viwili, cha progesterone na estrogen. Vichocheo hivi huzuia mimba kujipandikiza kwenye kuta za uterasi na kuzuia yai kupevuka.

Njia tofauti za uzazi wa mpango

  • Kutumia kondomu

njia nzuri ya uzazi wa mpango

Njia maarufu ya uzazi wa mpango. Ina walinda wanandoa dhidi ya kutunga mimba, kupata magonjwa ya zinaa kama vile gonorrhoea.

Hakikisha kuwa imevaliwa inavyo paswa na haipasuki. Ina asilimia 99 ya kuepuka kutunga mimba.

  • Vidonge vya kupanga uzazi

njia nzuri ya uzazi wa mpango

Vina asilimia 95 ya kulinda dhidi ya kupata mimba. Ila, hakikisha kuwa unavimeza inavyo paswa kama ulivyo shauriwa na daktari wako.
Hata hivyo, vidonge hivi huenda vika athiri mzunguko wa hedhi ya mwanamke. Kwa kufanya iwe ya kawaida, kupunguza uwezekano wa kupata saratani ya ovari na kupunguza uchungu wa hedhi.

  • Sindano ya uzazi

njia nzuri ya uzazi wa mpango

Ina asilimia 99 ya ufanisi wa kuepuka kuto tunga mimba. Ina punguza uwezekano wa kuugua saratani ya kizazi.

Athari hasi za sindano kama njia ya kupanga uzazi ni mwanamke huhisi kichefu chefu, kuongeza uzani wa mwili ama kupunguza kwa kasi.

Njia zaidi za kupanga uzazi

  • Kutumia tembe za dharura za emergency contraception
  • Kufunga kizazi
  • Kutumia IUD ama kitanzi
  • Kijiti cha kupandikiza

Ikiwa unatafuta njia nzuri ya uzazi wa mpango, ni vyema kuwasiliana na daktari ili akushauri njia itakayo kuwa bora kwako zaidi.

Soma Pia: Utumiaji, Manufaa Na Athari Za Limau Katika Kuzuia Mimba

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Pregnancy
  • /
  • Njia Tofauti Za Uzazi Wa Mpango Ambazo Wanandoa Wanaweza Kutumia
Share:
  • Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!

    Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!

  • Njia Za Kisasa Za Kupanga Uzazi Na Athari Zake Kwa Mwanamke

    Njia Za Kisasa Za Kupanga Uzazi Na Athari Zake Kwa Mwanamke

  • Je, Madhara Ya Sindano Za Uzazi Wa Mpango Ni Gani Kwa Mwanamke?

    Je, Madhara Ya Sindano Za Uzazi Wa Mpango Ni Gani Kwa Mwanamke?

  • Aina Tofauti Za Kupanga Uzazi Na Umuhimu Wake Kwa Jamii Na Wanandoa

    Aina Tofauti Za Kupanga Uzazi Na Umuhimu Wake Kwa Jamii Na Wanandoa

  • Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!

    Njia Za Uzazi Wa Mpango Kwa Wanaume Na Athari Zake!

  • Njia Za Kisasa Za Kupanga Uzazi Na Athari Zake Kwa Mwanamke

    Njia Za Kisasa Za Kupanga Uzazi Na Athari Zake Kwa Mwanamke

  • Je, Madhara Ya Sindano Za Uzazi Wa Mpango Ni Gani Kwa Mwanamke?

    Je, Madhara Ya Sindano Za Uzazi Wa Mpango Ni Gani Kwa Mwanamke?

  • Aina Tofauti Za Kupanga Uzazi Na Umuhimu Wake Kwa Jamii Na Wanandoa

    Aina Tofauti Za Kupanga Uzazi Na Umuhimu Wake Kwa Jamii Na Wanandoa

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2023 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it