Njia za asili za uzazi wa mpango zina zuia mwanamke kutunga mimba bila kutumia kemikali ama vifaa vya kuzuia mimba wanandoa wanapo fanya mapenzi. Ni muhimu kufahamu mbinu za kuzuia mimba ili kujiepusha na mimba isiyo tarajiwa.
Mbinu za kupanga uzazi kiasili

- Kunyonyesha. Mwanamke anapo nyonyesha, hasa miezi ya kwanza mitatu baada ya kujifungua, ana nafasi changa za kutunga mimba. Hii ni kwa sababu mwili wake unatoa homoni zinazo ufanya mwili usipevushe yai.
Kuna baadhi ya wakati ambapo mwanamke huenda kapata mimba hata anapo nyonyesha mtoto. Mbinu hii inategemea na mara anazo mnyonyesha mtoto kwa siku.
- Kutumia kalenda na siku salama katika mzunguko wa hedhi. Mbinu hii ni maarufu sana kwa wanandoa wanao ishi pamoja na hawataki kutumia kondomu wala hawako tayari kuwa wazazi. Mwanamke ana tumia kalenda kufahamu siku zilizo salama kwake kufanya tendo la ndoa bila vizuizi.
Katika wakati huu, ana nafasi changa zaidi za kutunga mimba. Wanandoa hawana shaka kuhusu kupata mimba wasipo tarajia. Mwanamke anaweza wasiliana na daktari ikiwa ana tatizika kufahamu siku zake salama.

Faida za kutumia njia asili kupanga uzazi
- Mwanamke yeyote anaweza kutumia bila hofu ya kupata athari hasi mwilini. Kama vile kuongezeka ama kupunguka kwa uzani wa mwili kwa kasi, ama kuvuja damu nyingi
- Hauna gharama yoyote ya kifedha
- Hauna madhara kwa afya ya mwanamke, mwili wake ama uso
- Ni nafuu ikilinganishwa na mbinu zingine za kupanga uzazi ambazo huenda zikamweka mwanamke katika hatari ya kukaa kabla ya kutunga mimba
- Mwanamke anapo taka kutunga mimba, ni kasi, ikilinganishwa na mbinu zingine za kuzuia mimba.
- Hauathiri umbo la mwanamke
- Kutumia njia asili haku athiri mzunguko wa hedhi ya mwanamke
Kwa mwanamke anaye tumia mbinu hii, anapaswa kuwa makini sana na mwili wake kufahamu mambo yanapo badilika. Mwanamke anapo karibia siku zake za rutuba, ute wake hubadilika na kuwa mwingi. Joto mwilini hubadilika na huenda akawa na chuchu laini. Kufahamu jinsi mwili wake ulivyo kawaida kutamsaidia kujua wakati anapofaa kujitenga na tendo la ndoa.
Njia za asili za uzazi wa mpango ni salama kwa wanawake wote!
Soma Pia: Mbinu 5 Kuu Za Kupanga Uzazi Na Kuzuia Mimba Baada Ya Ngono