Katika wakati mmoja maishani, huenda ukatatizika na hali ya makovu kwenye uso ama sehemu zingine za mwili. Habari njema ni kuwa, unaweza kutumia vitu vinavyopatikana jikoni kwa urahisi kutatua hali hii. Tazama njia za kinyumbani tunazoangazia za kuondoa makovu kwenye ngozi.
- Asali

Hakuna utafiti dhabiti unaoonyesha kuwa asali huondoa alama za makovu. Hata hivyo, watu waliotumia asali kwa muda mrefu wamedhihirisha kuwa, mbali na kuisaidia ngozi kuwa bora zaidi na kupunguza alama nyeusi mwilini, inasaidia kupunguza kuonekana kwa makovu kwenye ngozi.
Utaratibu wa kutumia:
- Paka kiasi cha asali kwenye sehemu iliyo na makovu
- Ifunike kwa kijitambaa kisafi
- Iwache itulie usiku mzima
- Toa kijitambaa asubuhi kisha usafishe sehemu ile kwa maji ya vuguvugu
- Fanya hivi kila usiku kabla ya kulala
2. Ndimu

Kupaka ndimu kwenye ngozi kumesemekana kusaidia kupunguza alama za makovu na kusaidia kurekebisha ngozi.
Jinsi ya kutumia:
- Kata kijisehemu cha ndimu
- Paka kwenye sehemu unayotaka kurekebisha
- Baada ya dakika kumi, safisha kwa kutumia maji ya vuguvugu
- Fanya hivi mara mbili kwa siku
3. Mmea wa aloe vera

Mmea huu huwa na matumizi mengi, baadhi ya matumizi haya ni kama kuondoa alama za makovu mwilini.
Jinsi ya kutumia:
- Kata kipande cha jani la mmea huu, kisha uondoe ngozi
- Chota umaji maji ulio ndani
- Paka kwenye sehemu iliyo na makovu
- Iwache itulie kwa nusu saa
- Osha kwa kutumia maji ya vuguvugu
- Rudia utaratibu huu asubuhi na jioni
4. Mafuta ya nazi

Maji ya nazi yanasaidia kurekebisha ngozi na kuituliza. Kwa sababu hii, imehusishwa na kupunguza kuonekana sana kwa makovu mwilini.
Utaratibu wa kutumia:
- Pasha joto vijiko vichache vya mafuta ya nazi ili yawe majimaji
- Paka mafuta yale kwenye sehemu ya mwili iliyo na makovu
- Kisha uwache kwenye ngozi kwa lisaa limoja
- Rudia mara tatu kwa siku
5. Papai

Tunda la papai limetumika kuondoa alama mwilini. Unaweza kuongeza manjano na asali unapotengeza kisha upake kwenye sehemu iliyo na alama na uwache kwa lisaa limoja. Safisha kwa kutumia maji safi.
6. Viazi

Toa maganda ya viazi kisha utoe sharubati yake na upake kwenye sehemu unayotaka kupunguza makovu. Safisha baada ya dakika 30. Rudia utaratibu huu mara mbili kwa siku.
Soma Pia: Kuchubua Ngozi Na Mimba: Athari Za Kujichubua Ngozi Kwa Mtoto