Africaparent Logo
Africaparent Logo
EnglishSwahili
  • COVID-19
  • Becoming a Mama
  • Ages & Stages
  • Parenting
  • Health
  • Feeding & Nutrition

Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

3 min read
Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika UhusianoNjia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano

Una jukumu la kuzingatia malengo ya kiafya ya mchumba wako ili kusaidiana katika kupunguza uzito katika uhusiano na kuwa na afya bora.

Utafiti uliofanyika ulionyesha kuwa wanandoa walio na uhusiano mwema huongeza uzito pamoja. Na wale ambao hawakuongeza uzito pamoja wali kuwa na nafasi ya kuachana. Kulingana na utafiti uliofanyika katika Chuo Kikuu cha Queensland huko Australia  ulionyesha kuwa kwa wastani, watu katika uhusiano walikuwa na uzito wa kilo 6.8 zaidi kuwaliko walio kuwa bila wachumba. Watu wenye wachumba walio ongeza uzito wa wastani wa kilo 1.9 kila mwaka. Je, kuna njia ambazo wachumba wanaweza kutumia kupunguza uzito katika uhusiano?

Njia za kupunguza uzito katika uhusiano

  1. Pika nyumbani badala ya kula nje

ratiba ya chakula vya kukata uzito

Njia moja rahisi ya kuhakikisha kuwa hauongezi uzito sana ni kwa kukula nyumbani. Vyakula vilivyo tayarishiwa nyumbani huwa vyenye afya na haviathiri ongezeko la upana wa kiuno. Hii ni kwa sababu unafahamu na unadhibiti viungo unavyo tumia kutayarisha chakula hicho. Kesi huwa tofauti unapo kula katika hoteli kwani haufahamu kilicho tumika kutayarisha chakula na ikiwa kita kuwa na athari hasi kwa uzito na upana wa kiuno chako. Bidhaa zinazo changia kwa sana ongezeko la uzito ni chumvi nyingi, mafuta ya kupika kwa kiwango kikubwa ama sukari.

2. Kuichunga fizikia yako pamoja na mchumba wako kwa kufanya mazoezi 

kupunguza uzito katika uhusiano

Ni vigumu kujipata mbali na mchumba wako? Usiwe na shaka, fanyeni mazoezi pamoja! Utafiti umedhihirisha kuwa kufanya mazoezi pamoja na wengine hukufanya utoe jasho jingi na kukusaidia kutimiza lengo lako la kifizikia.

Kulingana na mtaalum wa lishe Kim Larson kutoka Chuo Cha Nutrition and Dietetics, ana shauri wanandoa kuketi chini na kujadili mambo ya kufanya wakati wao wa ziada. Kama vile kutembea, ama kufanya mazoezi pamoja.

Hata kutembea kwa dakika 20 baada ya kula husaidia. Ikiwa una watoto wachanga walio nyumbani, mnaweza fanya mazoezi kutumia video zilizo kwenye mitandao. Ama mtembee karibu na nyumbani. Kuzungumza kuhusu malengo yenu ya kiafya kuta wasaidia kuyatimiza pamoja.

3. Mtindo wa maisha wenye afya

kupunguza uzito katika uhusiano

Inapofika kwa kupunguza uzito, ni muhimu kukumbuka kuwa unapaswa kuzingatia maisha yenye afya: Ikiwa umeanza kupika nyumbani na kufanya mazoezi, pongezi! Lakini, hiyo haimaanishi kuwa unapaswa kukoma. Cha muhimu ni kuzidi kufuata haya.

Hakikisha pia una koma kula vyakula vya barabarani na vitamu tamu visivyo ongeza dhamana yoyote mwilini. Badala yake, kula matunda, njugu na mboga. Enda hospitalini kufanyiwa vipimo mara kwa mara kuhakikisha kuwa afya yako iko sawa.

Una jukumu la kuzingatia malengo ya kiafya ya mchumba wako ili kusaidiana katika kupunguza uzito katika uhusiano na kuwa na afya bora.

Soma Pia:Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

Got a parenting concern? Read articles or ask away and get instant answers on our app. Download theAsianparent Community on iOS or Android now!

img
Written by

Risper Nyakio

  • Home
  • /
  • Health
  • /
  • Njia 3 Bora Za Kupunguza Uzito Katika Uhusiano
Share:
  • Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

    Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

  • Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

    Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

  • Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

    Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

  • Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

    Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

  • Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

    Jinsi Ya Kupunguza Uzito Ukiwa Na Mimba

  • Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

    Wanandoa Wenye Furaha Huongeza Uzito Pamoja Kulingana Na Sayansi

  • Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

    Lishe Na Mazoezi Ya Kukusaidia Kupoteza Uzito Wa Mwili Kwa Kasi

  • Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

    Kupunguza Ufuta Kwenye Tumbo: Masharti 5 Ya Kufuata Kupunguza Uzito Kwa Kasi

Get advice on your pregnancy and growing baby. Sign up for our newsletter
  • Becoming a Mama
    • Pregnancy
    • Delivery
    • Losing a Baby
  • Ages & Stages
    • Baby
    • Toddler
    • Kids
  • Parenting
    • News
    • Relationship & Sex
    • Parent's Guide
  • Health
    • Allergies & Conditions
    • Vaccinations
    • Diseases-Injuries
  • Feeding & Nutrition
    • Breastfeeding & Formula
    • Latching & Concerns
    • Weaning
  • More
    • TAP Community
    • Advertise With Us
    • Contact Us
    • Become a Contributor


  • Singapore flag Singapore
  • Thailand flag Thailand
  • Indonesia flag Indonesia
  • Philippines flag Philippines
  • Malaysia flag Malaysia
  • Sri-Lanka flag Sri Lanka
  • India flag India
  • Vietnam flag Vietnam
  • Australia flag Australia
  • Japan flag Japan
  • Nigeria flag Nigeria
  • Kenya flag Kenya
© Copyright Africaparent.com 2022 Tickled Media Pte Ltd. All rights reserved
About Us|Team|Privacy Policy|Terms of Use |Sitemap HTML

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it

We use cookies to ensure you get the best experience. Learn MoreOk, Got it