Njia Mwafaka Zaidi Za Kutunga Mimba

Njia Mwafaka Zaidi Za Kutunga Mimba

Unapo jaribu kupata mtoto, tendo la kimapenzi huwa na maana zaidi ya kufurahikia. Unajaribu juu chini kuhakikisha kuwa unafanya mambo yote inavyo faa ili kuongeza nafasi zako za kutunga mimba. Unahakikisha kuwa unatumia njia bora zaidi za kutunga mimba.

Ila, hamna njia zilizo dhibitishwa kwa haki kusaidia kutunga mimba. Utafiti ulio fanywa kwa kina unadhibitisha kuwa mabadiliko machache kwa wakati na muda unao jishughulisha katika tendo la kimapenzi huenda yaka ongeza nafasi zako za kutunga mimba.

Njia bora za kutunga mimba: Wakati mwafaka wa kufanya ngono

kutunga mimba

Wakati bora zaidi wa kujaribu kutunga mimba ni muda wa mzunguko wako wa hedhi wenye rotuba ama fertile zaidi. Kwa kawaida huwa siku tano kabla ovulation ya mwanadada. Siku mbili kabla ya ovulation na siku moja baada ya siku hii huwa bora zaidi za kutunga mimba. Unapo fanya ngono katika siku hizi, huenda ukafanikiwa kutunga mimba. Katika wakati huu, ovari yako huachilia yai lililo komaa na kulielekeza kwenye fallopian tube na baadaye kwenye uterasi yako. Katika mwendo huu, manii yanapatana na kulirutubisha ama kufertilize yai lile. Manii yana uwezo wa kuishi kwa siku tano. Kwa hivyo iwapo lengo lako ni kutunga mimba, unalenga manii kuwa hai wakati unapo ovulate.

Ni muhimu sana kwa mwanadada kujua wakati anapo ovulate iwapo anajaribu kutunga mimba. Jaribu kujua cycle ama mzunguko wako ya hedhi, siku inazo chukua ili uweze kujua wakati bora zaidi wa kufanya ngono. Iwapo unakumbana na matatizo yoyote, hakikisha kuwa umemtembelea daktari wako ili akupe mawaidha.

Je, ni njia zipi bora za kupata mtoto?

Unapo jihusisha katika ngono bila kinga na mwenzako, mamilioni ya manii yana achiliwa na kuingia katika uke wako. Unapo fanya tendo hili wakati wa ovulation, huenda ukapata mimba.

Hamna njia maalum zinazo ongezea nafasi zako za kutunga mimba, ilhali njia zingine huenda zika hakikisha kuwa manii yanapata njia mwafaka zaidi ya kupatana na yai.

Kuna baadhi ya njia zinazo aminika kumsaidia binti kuongezea nafasi zake za kujifungua. Ila tutaangazia zinazo julikana kwa sana. Tizama mifano tunayo angazia hapa!

  • Njia ambapo mwanamme ako juu na mke chini (missionary)

Njia hii ni bora zaidi kwani manii yana achiliwa kwenye uke wa binti. Bila matatizo yoyote ya kupanda kuifikia kizazi. Ili kuboresha mchakato huu, uwekelee mto kwenye mgongo wa binti kusaidia manii kuogelea bila tatizo.

njia za kutunga mimba

  • Pale ambapo mwanamme ako nyuma ya mke (doggy style)

Njia hii pia ni bora ya kupata mtoto. Kwani sehemu nyeti za mke na mme zina uingiliano zaidi. Manii hayana tatizo kufika kwenye uke na hivyo basi kuufanya mchakato wa kutunga mimba rahisi zaidi.

  • Mke ako juu na kumtazamisha mume mgongo wake (reverse cowgirl)

Kuna baadhi ya wanawake wanao kuwa na uterasi iliyo tizama mbali (retroverted). Si rahisi kujua iwapo uterasi yako imo katika hali hii. Njia hii ni bora ya kupata mtoto kwani inatengeneza njia bora ya manii kuachiliwa kwenye uke. Jaribu njia hii, huenda ukatunga mimba!

  • Miguu kwenye mabega ya mme

Mke anapolala kwenye njia hii. Na kuiwekelea miguu yake kwenye mabega ya mumewe, manii yanayo achiliwa yanaingia kwenye uke wake kwa urahisi zaidi. Na kuongeza nafasi yake ya kupata mimba. Njia hii ni bora ya kupata mtoto.

Hali ambapo mke na mme wamesimama sio bora vile kwani sehemu nyeti za mke na mme hazina uingiliano mwingi. Ila hii si sababu ya kupunguza nafasi yako ya kupata mimba. Kwani, punde tu manii yanapo achiliwa kwenye uke wa binti, yanachukua muda wa dakika 15 kufika kwenye kizazi cha binti.

Kuna imani kuwa iwapo unataka kutunga mimba, unapaswa kuinua miguu yako kwenye hewa ili kuhakikisha kuwa manii yamefika kwenye kizazi. Jambo hili sio la kweli.

Je, unapaswa kufanya ngono mara ngapi?

Kuna imani kuwa kufanya ngono mara kwa mara hupunguza ubora na wingi wa manii yanayo achiliwa. Ila, utafiti unadhibitisha kuwa manii yanayo achiliwa baada ya siku 2-3 za kutofanya ngono huwa na ubora zaidi. Utafiti pia unadhihirisha kuwa wanandoa wengi wanao tunga mimba ni wale wanao jihusisha katika tendo la kimapenzi kila siku ama baada ya siku moja.

Kufanya mapenzi kila siku ama baada ya siku moja katika wakati mwanadada anapokuwa ana ovulate huongezea nafasi zake kutunga mimba. Tendo la ngono ni la kufurahisha na haswa ni bora zaidi katika wakati huu unapo tamani kupata mimba. Ila usijilazimishe kwa tendo hili. Huenda ukapata fikira nyingi ambazo si sawa wakati huu. Pia jiepushe na kutengeneza ratiba ya kufanya ngono.

Vidokezo vingine vya kupata mimba

Iwapo unataka kutunga mimba, sio ngono peke yake itakayo kusaidia kutimiza lengo lako. Kuna vitu vingine ambavyo unapaswa kuzingatia.

  • Angazia uzito wako wa mwili

Kuwa mzito zaidi ama mwepesi zaidi huenda kuka athiri juhudi zako za kutunga mimba.

  • Jiepushe na kuvuta sigara

Kuvuta sigara hupunguza nafasi zako za kupata mimba na kupunguza wakati ambao manii yanakuwa hai mwilini mwako.

  • Kupunguza kiwango cha kahawa unacho kunywa

Kiwango cha juu cha kahawa hupunguza nafasi zako za kupata mimba. Hakikisha kuwa unakunywa kiwango cha kawaida.

vidokezo vya kutunga mimba

Tamatisho

Tendo la ngono ni la muhimu unapotizamia kupata mtoto, ila wakati unapofanya tendo hili ni la maana zaidi. Hakikisha kuwa u-makini wakati unapojihusisha katika tendo hili. Kwani hakuna njia bora zaidi ya kupata mtoto, siri ni wakati unapofanya mapenzi. Ni matumaini yetu kuwa njia za kupata mtoto tulizo dokeza zitakusaidia katika lengo lako la kupata mtoto. Twakutakia mema unapo jitahidi kupata mtoto wako na mwenzio.

Iwapo juhudi zako za kutunga mimba zina gonga mwamba, usiwe na wasi wasi wala ukapata fikira nyingi. Kupata mimba huchukua muda hasa pale unapokuwa wa miaka 30 ama zaidi. Jipe wakati na usife moyo.

Iwapo njia zote za kutunga mimba zina hazina fanaka. Hakikisha kuwa unamtembelea daktari wako. Ataweza kukupatia vipimo vinavyo faa ili kudhibitisha matatizo uliyo nayo na kukupa suluhu ili uweze kutunga mimba.

Written by

Risper Nyakio